Nani Ananufaika na kuwafundisha watanzania ujinga?

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Wakuu heshima kwenu.

Ukiangalia sura ya elimu ya taifa letu inatia kinyaa. Wanafunzi wanafundishwa juu juu sana na eti sera ya elimu inalazimisha wafaulu kwa wingi.

Lugha ya kufundishia ni kiswahili.

Hakuna mkazo wa kusoma science kwa undani na utafiti. Hakuna bidii ya kina kuwafananisha watanzania na wa nje.

Mitihani nayo imekaa kisiasa sana. Muundo mpya wa elimu nao upuuzi tuu bado hakuna nia ya dhati ya kuwapa elimu ya kweli watanzania.

Nani ananufaika na huu ujinga wa watanzania?

Your browser is not able to display this video.
 
Bwashee, hebu tuache kidogo tumalize hili la Bandari.

Samahani lakini
 
Wee angalia Samia alipoingia Madarakan, mwaka wake huohuo, watoto wakaanza kufaulu sanaaa si kidato Cha Nne, Si kidato Cha Sita.

Ukiuliza utasikia, Mama kajenga Madarasa , Mama kafanya hivi 🤣🤣🤣🤣.

Tunaenda kua na Kizazi Cha Ujinga Pro !!!!. ya Prof Mruma, ni madogo
 
Zanzibar mwaka huu wataongoza matokeo ya darasa la 7
 
Tulijenga kwa mabua tunaona muda umeenda hatutaki kufanya ujenzi imara na thabiti tunaishia kuyapamba mabua yavutie
Tunasahau chenye ubora ni bora tuu, nikifikiriaga mfumo wa elimu ulivyokaa nasema kabisa ndiyo sababu kubwa ya kuwa na taifa kama hili
 
Umetumia nafsi ya tatu kama vile wewe si mtanzania, ungetumia nafsi ya kwanza.

Haya matatizo ni yetu sote kama watanzania tuangalie namna gani tunatatua.

Kuanza tu kwa kujiengua tayari ni tatizo.
 
Umetumia nafsi ya tatu kama vile wewe si mtanzania, ungetumia nafsi ya kwanza.

Haya matatizo ni yetu sote kama watanzania tuangalie namna gani tunatatua.

Kuanza tu kwa kujiengua tayari ni tatizo.
Lazima nijiengue mkuu.
Mimi nikiangalia kwa mfano chekechea moja hivi wamerundika watoto kama 130... nikiangalia watoto wa darasa la tano unamuuliza mbuzi kwa kiingereza anaitwa nani mpaka awazeeee ndo anakujibu.
Mimi si sehemu ya ule upuuzi wanaita mtaala mpya . Mimi sio sehemu ya Necta
Sihusiki na huu upuuzi.
Kenya wenzetu wapo serious sana na elimu.
Usinilaumu ila kama vipi tuingie mtaani kupingana na huu umruma
 
Unaweza usiwe sehemu ya mfumo uliopo sasa hivi, lakini bado uko Tanzania mkuu. Kwa hiyo unaathirika kwa namna moja ama nyingine.
 
Kuna mwingine zaidi ya ccm mkuu?? Au na wewe ni kada unatuchora?
 
CCM ndio inanufauka UKITAKA kunufaika au Kutajirika CHEZA na WAJINGA
 
Kinachouma zaidi vijana wasiojitambua ni wale wanaokishabikia chama tawala sijui kwanini!
Hawataki hata kujua kesho yao ipo wapi, ni aibu sana na sijui wamelogwa na nani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…