Nani Ananufaika na kuwafundisha watanzania ujinga?

Nani Ananufaika na kuwafundisha watanzania ujinga?

Wakuu heshima kwenu.

Ukiangalia sura ya elimu ya taifa letu inatia kinyaa. Wanafunzi wanafundishwa juu juu sana na eti sera ya elimu inalazimisha wafaulu kwa wingi.

Lugha ya kufundishia ni kiswahili.
Hakuna mkazo wa kusoma science kwa undani na utafiti. Hakuna bidii ya kina kuwafananisha watanzania na wa nje.
Mitihani nayo imekaa kisiasa sana. Muundo mpya wa elimu nao upuuzi tuu bado hakuna nia ya dhati ya kuwapa elimu ya kweli watanzania.
Nani ananufaika na huu ujinga wa watanzania?
View attachment 2698381View attachment 2698413
CCM ndiyo inanufaika na ujinga wa Watanganyika
 
Ndo maana graduates wa kipindi hiki cha mwendokasi ni weupe hakuna mfano.......ni mwendo wa kufyatua vilaza.
 
Na ukitoka shuleni na ujinga

mtaani vijana wanaongezewa ujinga wa simba na yanga
 
Na ni majinga kweli kweli na mengine yanajivunia kabisa ujinga wao!
 
Mfumo wa watu fulani

Huoni sahvi ujingujing unapewa kipaumbele.....
Mtu anafanya maujingaujinga mwisho wa siku wanakuambia eti ni influencer
Na bungeni atakaribishwa

Ova
 
Moja ya kosa kubwa la karne ni viongoz wa ccm awamu zote kufanya kiswahili kuwa lugha ya kufundishia shule za msingi na awali huku watoto wao wakisoma shule za ama English Medium, International au nje ya nchi,hili limeongeza ujinga kias kikubwa kwa jamii na uelewa finyu wa mambo mengi ya kitaaluma na kimataifa,wengi ni wasomi wa kukariri sio wa kuelewa,Ningekuwa Rais on day one ningeanza mchakato wa kukifanya Kiingereza kuwa lugha ya kufundishia ngaz zote za elimu
 
Back
Top Bottom