Massinyori-mwakilishi wa papa anawazidi wote
Mwadhama kadrinali mjumbe katika conclave kikao mhimu cha kumchagua papa
Anahudhuria kikao cha kuchagua papa (conclave) akiwa na yeye ni candidate iwapo tu hajafikisha miaka 75
Kadrinali yoyote akiisha vuka miaka 75 ni mjumbe tu katika uchaguzi wa papa ila yeye siyo candidate(hawezi kuchaguliwa)
Tanzania kwa sasa kwa mjibu wa kanisa katoliki la Roma- mkubwa ni massinyori
Mkuu, unavyosema Monsinyori anawazidi wote sijui ni akina nani hao unaowalinganisha na Monsinyori na siyo Massinyori kama ulivyoandika labda kama unamaanisha jina jingine jipya!
But any way, hebu tuangalie baadhi ya matumizi ya maneno yanayotutatiza wengi, tunapoyasikia na hatujui yanatumikaje;
1.mwandamizi,
2.mwadhama,
3.mhashamu,
4.monsinyori
1.Mwandamizi
Maana yake ni mtu anayetarajiwa kurithi cheo au madaraka fulani. Hivi askofu mwandamizi ni yule atakayechukua cheo au madaraka moja kwa moja baada ya yule aliyepo sasa kutoka katika cheo hicho. Mfano kama ilivyokuwa kwa Askofu YudaThaddeus Ruwa'ichi kabla ya kumrithi Askofu Pengo.
2. Mwadhama
Maana yake "mheshimiwa sana" . Mwadhama hutumika kwa makardinali. Mfano Mwadhama Kardinali Pengo.
3. Mhashamu
Mhashamu maana yake "mheshimiwa".
Hutumika kwa maaskofu wakuu na maaskofu wa kawaida. Mfano Mhashamu Askofu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, n.k
4. Monsinyori
Maana yake ni "kasisi wa kipapa".
Ni cheo ambacho kwa sasa kinatolewa kwa mapadri wenye umri kuanzia miaka 65,(hii ni baada ya mabadiliko yaliyofanywa na Papa Francis, awali kilikuwa kinatolewa kabla ya huo umri) baada ya kufanya kazi ya kutukuka Jimboni mwake au katika baadhi ya ofisi muhimu za Kanisa, - ambapo matumizi ya jina Monsinyori limekuwa ni mila na desturi , kwa mfano katika ofisi ya Askofu, au Mwakilishi Mkuu wa Jimbo au Vika wa jimbo.
Vile vile"monsinyori" hupewa manaibu maaskofu kwa heshima ya nafasi hiyo.
Mfano kuna Monsinyori Deogratias Mbiku wa Jimbo kuu Dar es salaam ambaye ni msaidizi wa Askofu mkuu jimbo kuu Dar es salaam.
N.B: Kwa upande wa mapadre wa kawaida, tunawaita waheshimiwa tu.