Nani anaratibu haya kwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan?

Nani anaratibu haya kwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan?

Mkuu

Ndege za mabwanyenye zimeanza kutua kwa fujo kiwanja kidogo cha Zinga, Bagamoyo ambako bandari bandari yenye utata inataka kujengwa. Ndege imetua wakashuka watu weupe kama saba na weusi wawili hivi!!!

Usishangae, kama waliweza kuchukua vipimo vya JPM na kupeleka Kenya kisiri kwa kutumia presidential code ili aonekane alipelekwa huko unashangaa nini mkuu? Nchi ya TZ ina viongozi hawapo sayari yoyote ulimwenguni hata UFOs wanawakataa!!!
Aliens 👽 ??!!! Sio kweli !
 
Hizi safari zake za mara kwa mara huko Arabuni tena za kificho hazina nia njema kwa Tanganyika yetu,Amkeni Watanganyika .
 
Rais ni mkuu wa Serikali na nchi. Rais ni nembo yetu; fahari yetu; kiongozi wetu na kiungo chetu. Lakini, Rais ni 'mwajiriwa wetu' nambari moja nchini. Ndiyo maana, akifanya vizuri tunamsifu na akifanya vibaya tunamkosoa na kumsema.

Tunapaswa kujua anakoenda na anachoenda kufanya. Labda kama anakwenda likizoni. Usirisiri kwenye mambo yamhusuyo Rais wetu unatutisha na hatuupendi. Ukomemeshwe hadi ukome. Huu ni ujumbe wangu kwa wahusika wote wa ulinzi na protokali za Rais wetu.

Ilianza kule Kenya. Raila Odinga, kinara wa upinzani nchini Kenya, alidai kuwa Rais Samia alikwenda nchini Kenya kwa ajili ya kujaribu kuwapatanisha Raila na Rais William Ruto. Habari hii ilishtua wengi. Iliwezekanaje Rais Samia, aliyekuwa na nia ya amani ya Kenya, kwenda sirini na kisirisiri?

Ikafuata kuonekana ndege ya Rais kule Uarabuni hivi majuzi. Kama watanzania, hatukutangaziwa wala kufahamishwa kama Rais wetu ana ziara Uarabuni. Iliwezekanaje ndege ya Rais wetu (iliyoashiria kuwa Rais alikuwa huko pia) iende kisirisiri Uarabuni?

Ratiba za Rais wetu ziwe wazi. Mambo yake kama Rais yawe wazi. Kufichaficha na kumsafirisha Rais wetu sirini hakuna faida. Tutaambiwa nini ikiwa jambo lisilovutia likimtokea Rais wetu huko anakokwenda kwa siri...hukohuko sirini? Nani anaratibu mambo haya hatarishi kwa Rais wetu?

Rais ni public figure. Tunapaswa kujua yote anayoyatenda kama Rais.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (Kilosa, Morogoro)
Lakini naye ana akili kweli? Inakuwaje anapelekwa kisirisiri na sirini..?

Yeye haioni hatari kweli?

Kwa taarifa yake anapaswa kujua kabisa kuwa yuko pale kwa hisani ya katiba tu, lakini in actual senses, hakupaswa kabisa kukalia kiti cha Urais cha watu wa Jamhuri ya Tanganyika na ndiyo maana tulizozana sana kukubaliana iwapo amu- replace Hayati Rais John P. Magufuli immediately baada ya kufariki kwake (JPM) au tuvunje katiba kwa kumweka mtu mwingine likiwemo jeshi hadi kutakapoitisha uchaguzi mwingine..

Lakini Kwa shingo upande, tukasema, basi acha tuheshimu katiba na kwa wakati sahihi naye mwisho wa siku aondoke Kwa mujibu wa katiba; kifo, kujiuzuru, ugonjwa wa muda mrefu au potelea mbali amalize muda wake...

Kwa hiyo achunge sana safari za kimya kimya hizi anazopangiwa na wasaidizi wake. Si ajabu wakawa na lengo la kumuwahisha kiaina kwa namna nyingine na halali na sahihi Kwa mujibu wa katiba ili waweke mtu wao..!

Mama una dhamana kubwa mno. Usitangulize starehe na bata ukiacha kuchunga uhai wako mwenyewe..!
 
Lakini naye ana akili kweli? Inakuwaje anapelekwa kisirisiri na sirini..?

Yeye haioni hatari kweli?

Kwa taarifa yake anapaswa kujua kabisa kuwa yuko pale kwa hisani ya katiba tu, lakini in actual senses, hakupaswa kabisa kukalia kiti cha Urais cha watu wa Jamhuri ya Tanganyika na ndiyo maana tulizozana sana kukubaliana iwapo amu- replace Hayati Rais John P. Magufuli immediately baada ya kufariki kwake au tuvunje katiba kwa kumweka mtu mwingine likiwemo jeshi hadi kutakapoitishwa uchaguzi mwingine..

Kwa hiyo achunge sana safari za kimya kimya hizi anazopangiwa na wasaidizi wake. Si ajabu wakawa na lengo la kumuwahisha kiaina kwa namn nyingine ili waweke mtu wao..?
Aisee...
 
Back
Top Bottom