HOJA Nani anaruhusu ujenzi katika maeneo ya Hifadhi ya Morogoro Road (Kimara–Mbezi Luis)? Je, tumesahau yaliyotokea 2017?

HOJA Nani anaruhusu ujenzi katika maeneo ya Hifadhi ya Morogoro Road (Kimara–Mbezi Luis)? Je, tumesahau yaliyotokea 2017?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
photo_2026-07-21_10-50-44.jpg
Takribani miaka 10 iliyopita, Watanzania walishuhudia moja ya operesheni kubwa za ubomoaji wa makazi na biashara zilizokuwa kandokando ya Barabara ya Morogoro, maarufu kama Morogoro Road. Kuanzia Korogwe, Kimara, Mbezi Luis hadi Kibamba, nyumba, maduka na vitega uchumi vilibomolewa kwa maelezo kwamba vilikuwa vimejengwa ndani ya eneo la hifadhi ya barabara.

Kwa wengi, halikuwa tukio la kawaida. Lilikuwa ni siku ya majonzi. Wapo walioona nyumba walizojenga kwa jasho la maisha yao zikigeuzwa kifusi ndani ya saa chache. Wapo waliopoteza biashara zilizokuwa tegemeo la familia zao, huku wengine wakibaki bila makazi. Ingawa wengi waliamini hatua hiyo ilikuwa kwa maslahi ya umma na utekelezaji wa sheria, waliamini pia kwamba eneo hilo lingeendelea kubaki kama hifadhi ya barabara na lisingetumika kwa shughuli nyingine zinazokiuka sababu iliyowafanya waondolewe.

Hata hivyo, siku za hivi karibuni, hali inayoonekana katika baadhi ya maeneo hayo imeanza kuibua maswali mengi. Katika maeneo yaliyokuwa yamebomolewa, sasa kuna majengo mapya ya biashara yanayochipuka.
photo_2026-07-21_10-50-44 (2).jpg

photo_2026-07-21_10-50-41.jpg
Nimefuatilia kwa karibu kipande cha barabara kutoka Kimara kuelekea Mbezi Luis, ambapo nimeona baadhi ya maeneo yakijengwa vituo vya mafuta, kiwanda, huku sehemu nyingine zikiwa zimezungushiwa uzio na shughuli za ujenzi zikiendelea.

Hali hii inaibua hoja nzito kuhusu uwajibikaji, utoaji wa vibali na usawa mbele ya sheria. Ikiwa maeneo hayo yalitangazwa kuwa ni hifadhi ya barabara na wananchi wakaondolewa kwa msingi huo, ni nani anayetoa vibali vya kujenga miundombinu ya kudumu katika maeneo hayo? Je, kuna mabadiliko ya matumizi ya ardhi yaliyotangazwa rasmi kwa umma, au kuna utaratibu unaofuatwa ambao wananchi hawaufahamu?

Maswali haya yanahitaji majibu ya wazi ili kuondoa hisia zinazoweza kujenga taswira ya upendeleo, rushwa au matumizi yasiyo sawa ya sheria. Sheria inapotekelezwa kwa wananchi wa kawaida, ni muhimu ionekane inasimamiwa kwa usawa kwa kila mtu, bila kujali hadhi au uwezo wa mwekezaji.

Aidha, iwapo siku zijazo Serikali itahitaji tena kutumia maeneo hayo kwa madhumuni ya miundombinu, je, itaweza kuwaondoa waliowekeza humo bila kuzua migogoro mingine? Na endapo hilo litatokea, je, hatutashuhudia tena malalamiko na sintofahamu kama ilivyokuwa wakati wananchi walipobomolewa makazi yao miaka iliyopita?
photo_2026-07-21_10-50-42.jpg
Mashaka yangu si kuhusu uwekezaji, bali ni kuhusu mwenendo unaojitokeza. Endapo hakutakuwa na uwazi na uwajibikaji katika matumizi ya maeneo haya, kuna hatari ya kuona ujenzi mwingine ukiendelea, na baadaye hata makazi kuanza kuibuka ndani ya maeneo yaliyotengwa kwa matumizi ya umma.

Ni wakati sasa kwa mamlaka husika kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu hadhi ya maeneo haya na utaratibu unaotumika kuyagawa kwa wawekezaji. Uwajibikaji na uwazi si kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi pekee, bali ni msingi wa kujenga imani kwa umma na kuzuia migogoro inayoweza kujitokeza siku zijazo.
 
Hata mimi nimekuwa nikijiuliza kuhusu hili,kama pale Kibanda Cha Mkaa uelekeo wa kwenda Mbezi pale ni kama imejengwa nyumba kabisa.

Ama la vituo vya mafuta linazungumzika labda uwekezaji wa muda but kujengwa majengo yanayoashiria makazi ya watu inatia shaka kidogo kiasi cha kudhani sasa hivi hakuna serikali
 
husu hadhi ya maeneo haya na utaratibu unaotumika kuyagawa kwa wawekezaji. Uwajibikaji na uwazi si kwa ajili ya kujibu maswali ya wananchi pekee, bali ni msingi wa kujenga imani kwa umma na kuzuia migogoro inayoweza kujitokeza siku zijazo.​
Wachina na wenye ma kampuni yao ya mafuta wanawekez yadi za magari na sheki
 
Hii nchi ina vurugu sana...so waliwaondoa wanyonge ili waweke vitega uchumi vyao
 
Back
Top Bottom