Ndagullachrles
JF-Expert Member
- Jun 20, 2023
- 256
- 259
Wakazi wa kata ya soweto Manispaa ya moshi wanaoishi kwenye maghorofa sita ya Shirika la Nyumba la Taifa (HNC)kiwanja namba 89 Kitalu L barabara ya Arusha,wamepaza sauti wakipinga ujenzi unaoendelea kwenye makazi yao.
Wnahofia usalama wa maisha yao na mali zao endapo utatokea mlipuko wa moto huku wakihoji ni nani ameruhusu ujenzi wa kituo hicho cha mafuta kwenye makazi yao.
wamemwandikia barua Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati,Dotto Biteko wakitaka aunde timu ya uchunguzi kuchunguza ujenzi huo na kuchukua hatua kwa waliotoa kibali cha ujenzi wa kituo hicho.
Ujenzi wa vituo vya mafuta kwenye makazi ya watu kimekuwa ni kilio cha siku nyingi lakini hakuna anayesikiliza kilio hicho cha wananchi.
Mwaka 2004 Halmashauri ya Manispaa ya Moshi ilitoa kibali cha ujenzi wa kituo cha mafuta kwa mfanyabiashara Patrick Ngiloi kwenye Ploti namba 435 Block LLL eneo la Karanga.
Hata hivyo baada ya wananchi wa eneo hilo kupinga ujenzi wa kituo hicho kwenye makazi yao,Manispaa hiyo hiyo ikamlima barua mfanyabiashara huyo kufukua matanki yake na kusitisha ujenzi wa kituo hicho.
Manispaa hiyo chini ya aliyekuwa mkurugenzi wake Joel Shimbe ilisema ukubwa wa kiwanja hicho haukuruhusu kujengwa kituo cha mafuta kwani ukubwa unaotakiwa walau uwe mita za mraba 2,800.
swali linabaki je nani anatoa vibali vya ujenzi wa mafuta kwenye makazi ya watu?