Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Nani anastahili tuzo ya Nobel katika marais 6 tuliowahi kuwa nao Tanzania?

Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
always nyerere ni best, akifuatia na fulan simtaji ili kuondoa kelele za wale majamaa wa upande ule, na kuna vikundi vyakipuuzi hupenda kumbeza nyerer kuwa alifanya mambo ya hovyo ktk sakata la.......,

Hawa watu wanasahau kuwa nyerer alipambana sana kuhakikisha hii nchi inafika ilpofika leo, wakat huo mababa na mababu wa hawa walalamikaji, walikuwa bize maporini wakikimbizana nusu uchi na wanyamapori, sasa matoto yao leo hii yanajiona yamestaharabika wala hayana shukrani kwa wapigania uhuru, yanatusi na kushusha samani ya uhuru na amani hii.
 
Mawazo ya Nyerere uliyokwoti, hayamo hayamo katika zile category sita za nobel: yaani Chemistry, Physics, Medicine, Literaturre, Economic Sciences na Peace. Kwa dunia ya leo Nyerere anaweza kushinda kwenye Peace lakini hana sifa kwa vile ni mfu.
Kitu gani alichofanya ambacho kingewafanya wazungu wampe tuzo ya Nobel ya amani?
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Nyerere alistahili lakini kwa sasa labda JK hakuna mwingine,Samia atakuwa na nafasi kubwa kupata tuzo ya Mo Ibrahim.
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Aliyezindua daraja la Mfugale anastahili...
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya mchango katika sayansi ya Uchumi?
Tuzo ya Nobel kwa Tz anapaswa kupewa Julius Kambarage Nyerere kwa sababu
1. Mwaminifu ambaye hakujitajirisha kwa pesa za masikini wavujajasho
2. Aliimarisha uchumi kwa kujenga viwanda vingi na kuongeza ajira
3. Hakuwa na upendeleo kwa familia yake, Kabila lake, Ukanda wake wala marafiki zake
4Alizikomboa nchi nyingi za Afrika zilizokuwa chini ya ukoloni.
5. Alituwezesha kuwa na dira ya maendeleo ya jamii kuwa ni ujamaa na kujitegemea. Leo haijulikani kama ni wajamaa au mabepari
6.Alikuwa na huruma kwa watanzania wote

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi?
Baba wa Taifa tu wengine hawastahili tuzo ya aina yoyote ile.
 
Drederik de Klerk na Mandela walipewa tuzo moja ya Nobel ya amani kama washindi wawili kwa pamoja.
Duh! hii mpya kabisa!

Najaribu kutafuta connection kuona inakaaje kwa kutumia case study ya Afrika Kusini ambapo Mandela na Desmond Tutu walipewa tuzo hii licha ya kikundi cha Mandela na Tutu kuwa na makambi ya kujifunza vita vya ukombozi Tanzania (kambi 3), Zambia (Kambi 1) ambapo wapiganaji walipewa mafunzo na kurejea Afrika Kusini kwa siri kufanya incursions ambapo vita hii ilishindwa kuleta ukombozi hadi tu pale Rais Frederik Willem de Klerk (Kaburu) alipoamua kuwatoa akina Mandela jela na kuruhusu kuanza mchakato wa kumaliza ubaguzi wa rangi. Sasa connection inanigomea hivi:-

1. Mwl. Nyerere ali-play central role kwa 90% katika ukombozi kuliko Askofu Tutu na Mandela aliyekuwa jela. Mwl. Nyerere ndiye aliyeiondoa serikali ya Makaburu kwenye Jumuiya ya Madola. Lakini tuzo wakaja kupewa Tutu na Mandela Mwl. Nyerere asiipewe hata baada ya kutoa ground kwa uMkhonto we Sizwe (MK) huku APLA cha akina Letlapa Mphahle ikiendesha vita nyumbani Afrika Kusini Transvaal.

2. Rais Frederik Willem de Klerk ambaye baada ya jitihada za ANC ya akina Oliva Tambo na Yusuf Dadoo, SAUF, SACP, SASO, AAM, SACTU, ARM ya akina John Lange, Monty Berman na Myrtle Berman, PAC ya akina Nana Mahomo na Peter Molotsi (kutaja lakini kwa uchache) kushindwa kuleta ukombozi akaamua kufungua ukurasa mpya wa ukombozi na kuiponya Afrika Kusini hakupewa tuzo hiyo wakapewa akina Chief Albert Luthuli, Bishop Desmond Tutu na Nelson Rhohlilala Madiba Mandela. Tanzania tumelogwa na nani? Mwl. Nyerere na Rais Frederik Willem de Klerk walikosea wapi?

Baghosha! Nobel Prize.
 
Tuzo ya Nobel ya Sayansi ya Uchumi haitolewi kwa wanasiasa, inatolewa kwa wanazuoni na mara nyingi ni hutolewa kwa Waahidhiri wa vyuo vikuu ambao huja na nadharia mpya katika uchumi.

Kwa nini Nyerere alistahili Tuzo ya amani?
No.1 itamfaa ametatua migogoro mingi Sana ya kikanda kama mpatanishi ndio maana hata majuzi kawapatanisha Wazambia.
 
Tuzo ya kimataifa ya Nobel iliyoanzishwa na Bw Alfred Bernhard Nobel, Mswidi mbobezi wa kemia, uhandisi, mvumbuzi, mjasiriamali na mdiakonia (matendo ya huruma (philanthropist)) imetoa tuzo hiyo kwa Wanafizikia watatu kwa mpigo.

Swali:
Katika safu ya marais 6 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unadhani nani kati yao angeweza kustahili tuzo hiyo maarufu?

Kwa sababu zipi?

Kwanini imeshindikana?

Afrika Kusini wana Laureate 3, Liberia 2, DR Congo 1, Ethiopia 1, Kenya 1, Tanzania tumekwama wapi na juhudi zote nzuri za #AMANI YA NCHI, #ULINZI WA AMANI YA DUNIA, #UKOMBOZI KUSINI MWA AFRIKA, #MIUNDOMBINU BORA, #MUUNGANO WA PEKEE DUNIANI, #OAU, #KUANZISHWA KWA NON ALIGNED MOVEMENT, #SOUTH SOUTH COMMISSION, #SADC, #EAC, na mengine mengi mazuri kimataifa. Ni Mwl. Nyerere ndiye aliingiza China kwenye kundi la mataifa yenye kura ya turufu katika Umoja wa Mataifa. Aidha alikuwa mmoja wa washauri wa Malkia wa Uingereza lakini hata tuzo ya heshima ya juu Uingereza ya "Sir" hakuwahi kuipewa. Naomba nikope maneno ya Paulo Mtume aliyeuliza hivi "Enyi Wagalatia mmerogwa na nani? Wagalatia.3:1"

Yote hayo na mengine mengi mazuri ya Tz bado Kamati ya Nobel haizioni tu?

Angalizo:
Changia mawazo yako kwa kutuonyesha hekima na busara zako ili tufaidike na maarifa yako, usichangie jazba za kuonyesha kejeli, dharau na matusi, utakuwa umetunyima maarifa yako.
Nyerere, JPM, Mama Samia👍
 
Tuzo ya Nobel ya Sayansi ya Uchumi haitolewi kwa wanasiasa, inatolewa kwa wanazuoni na mara nyingi ni hutolewa kwa Waahidhiri wa vyuo vikuu ambao huja na nadharia mpya katika uchumi.

Kwa nini Nyerere alistahili Tuzo ya amani?
Shuleni nilifundishwa kwamba Mwl. Nyerere alikuwa Political Economist (ambayo ni sehemu ya Sayansi ya Uchumi) na Roving Lecturer. Somo la siasa A-Level (sikusoma civics) ilikuwa na sehemu mbili za elimu ya uraia na uchumi-siasa (Political Economy). Mkuu Yoda, mimi wakati fulani ninahisi Kamati ya Nobel ina majuto kwa Nyerere kwamba kwanini hawakuchukuwa hatua akiwa hai.
 
Tuzo za za Nobel ziko sita, unaongelea tuzo gani ya Nobel?

1.Ya Amani?
2.Ya Fasihi?
3.Ya Biolojia/madawa?
4. Ya Physics ?
5. Ya Kemia?
6. Ya Sayansi ya Uchumi
Feel the force- Yoda 🤣 🤣
 
Back
Top Bottom