Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
NB: Nimeshazunguka kwa manabii, waganga wengi sana bila mafanikio,Hata huko Tanga Handeni wanakokusifia nimefika kwa waganga maarufu wawili nao wamechemsha hii kesi[emoji3064]Wadau
Naomba mawazo yenu wadau
Mimi ninabishara ya Real Estate na Logistics. Sababu niliwekeza sana kwenye advertisements,Hizi Kampuni zangu zimekuwa maarufu sana kiasi kwamba sasa siwatafuti wateja ila wateja wananitafuta mimi kila siku ili kupata huduma na bidhaa zangu. Sasa kimbembe ni pale wakisharidhika na kukubali kufanya malipo....wanapotea mazima....hii imetokea zaidi ya mara 100 mpaka sasa nimeshazoea.
Sasa nimefikiria sana nitafute msaada labda kwa watu wa Mungu au nipeni mawazo nifanyaje
NB: Nimeshazunguka kwa manabii, waganga wengi sana bila mafanikio,Hata huko Tanga Handeni wanakokusifia nimefika kwa waganga maarufu wawili nao wamechemsha hii kesi .Nafikiri waganga wa Tanga wanachoweza ni kuroga, na ishu za kijamii kama vile kurudisha mke,mme,nk na siyo biashara halali kama zangu
Naombeni mawazo yenu GTs
Tatizo limeanzia hapo
1. Umechanganya falme mbili kwa wakati mmoja sasa badala ya kusaidika zinapambana zenyewe kwa zenyewe
2. Umetumia madawa mengi sana mpaka yenyewe hayajui yatibu nini
3. Umeenda kwa waganga wengi sana kila mmoja kageuza mwili wako sehemu ya majaribio.. Mwili imekuwa kama punching bag
Kiroho, kinyota umeshachafuka sana.. Ushauri: Achana na hayo yote kwasasa.. Upe mwili nafasi ya kujitakasa urudi kwenye asili yake.. Tumia tiba ya chumvi kuharakisha mchakato