Nani anauza gari kati ya TRA na Mjapan?

Nani anauza gari kati ya TRA na Mjapan?

Unadhani serikali haitaki pesa?

Wagonjwa watawaishwa hospitalini kwa barabara zipi kama kila mtu ana gari?
Japan yenyewe nasikia pamoja ya kuwa magari ni cheap ila kuna sheria ili umiliki gari. Wengi wanatumia public transport.

Nchi lazima iweke control ya importation ya magari vesus miundombinu iliyopo. Hapo dar na mibarabara kila kona ila foleni just imagine mikoani kusipo na miundombinu kila mtu akawa na ist.
Bro tunajilinganisja na Japan yenye viwanda vya magari(Toyota,Mazda,Mitsubishi,Nissan etc) huku wakiwa na matreni ya umeme kibao/public transport system yao ni wamejizatiti.
 
Kodi ni kubwa sana ndio maana wengi wanakimbilia magari madogo na ya zamani na usalama wake pindi likipata ajali ndogo tuu ni mdogo wakati gari zilizotumika za 2010 mpaka 2015 bei zake za kawaida tuu kuanzia Toyota hilux. d4d, Disco 3,4,Range Rover,Subaru,Mercedes-Benz, Bmw na yanakua na Life span ya muda mrefu mpaka lianze kuja kusumbua lakini kwa kodi hizi tunaagiza gari ya 2000 harafu kutwa kulalamika hizi gari ni mbovu...Serikali punguzeni kodi kidogo kwenye magari sio starehe ni chombo tuu hicho kama vyombo vingine tuu..
Ndio maaana mimi huwa nawashangaa watu wanaoshabikia serikali hii, unajua kwa ufupi kabisa serikali hii ni wezi, wanakusanya kodi kwa kuwanyonya wananchi maskini, na ndio maana watu hwa wanatafuta namna ya kukwepa kodi, ndio njia pekee, ukifanya biashara halafu ukalipa kodi ile wanayotaka serikali lazima utafirisika mapema sana, watu wengi hulazimika kukwepa kodi, umeona hapo juu mfano wa hizo kodi, wizi mtupu
 
Kwamba Gari mfano hiyo Subaru bei yake ni Dola ya marekani moja[emoji50]?? Tsh 2,350?? BUKU MBILI? Kwamba mchakato wa kuruhusiwa kulimiliki bongo unazaa MILIONI KUMI NA SITA??

Kwamba ningekuwa na uwezo wa kulinunua kiwandani na kulibeba kimiujiza hadi kijijini kwetu Kabulabula nitawaringia kwa gari niliyonunua kwa BUKU MBILI[emoji848][emoji14]

Kama ni hivyo basi tuwaandikie barua mabeberu warudi waendelee kututawala tu, hatujielewi kabisa!
Umesema vizuri
 
Bro tunajilinganisja na Japan yenye viwanda vya magari(Toyota,Mazda,Mitsubishi,Nissan etc) huku wakiwa na matreni ya umeme kibao/public transport system yao ni wamejizatiti.
Hatujilinganishi, hatuna barabara za kuweza kuhimili gari nyingi.
 
TRA ndo anauza gari,,MJAPAN yeye ni kama dalali tu [emoji16]
 
Hatujilinganishi, hatuna barabara za kuweza kuhimili gari nyingi.
Ila tuna Usafiri wa umma bora wa kuweza kutu accommodate sio mkuu?Cheki Mwendokasi inavyojaza watu na Costa/hiace zetu uniambie hali unaionaje mkuu.
 
Ila tuna Usafiri wa umma bora wa kuweza kutu accommodate sio mkuu?Cheki Mwendokasi inavyojaza watu na Costa/hiace zetu uniambie hali unaionaje mkuu.
Torque magari yakiongezeka mara mbili tu ya haya yaliyopo utaichukia serikali. Tunatakiwa tutatue tatizo la miundombinu kwanza. Usafiri wa uma bado ni tatizo linalotakiwa kutatuliwa.
 
Hatujilinganishi, hatuna barabara za kuweza kuhimili gari nyingi.
Tanzania tuna bara bara bora na nzuri ila magari bora mengi ni ya serikali sisi tupo na vipasso kutwa kuuliza naweza kufika nacho mbeya hiki kutokea daslm wangepunguza Kodi ili watu tuweze kumiliki magari ya ukweli sio hivi kila kukicha kigari kinagonga wakati hayo ya ukweli hayana bei na nachosikitika huko japan tunanunua gari unafanana nalo umri ila tunaliita jipya..
 
Nakubaliana na ww kuwa Tungepunguza kodi ya magari mapya ambayo kuyanunua huko nje ni gharama.

Still nchi haipo kwenye mazingira wezeshi ya kuhimili idadi kubwa ya wenye magari.
 
Nakubaliana na ww kuwa Tungepunguza kodi ya magari mapya ambayo kuyanunua huko nje ni gharama.

Still nchi haipo kwenye mazingira wezeshi ya kuhimili idadi kubwa ya wenye magari.
Unaongea kitu usichokijua network ya bara bara Tanzania ipo juu mno Kama unasafiri kwa nchi zingine za kusini hata East Africa sisi tupo juu ukiondoa SA na Botswana ila zingine hapo hakuna wa kutufananisha na mfumo wa bara bara mikoa mingi imeunganishwa na kiwango cha lami kasoro kipande kidogo huko kigoma kuitafuta nyakanazi na kuingia kigoma yenyewe...
 
Torque magari yakiongezeka mara mbili tu ya haya yaliyopo utaichukia serikali. Tunatakiwa tutatue tatizo la miundombinu kwanza. Usafiri wa uma bado ni tatizo linalotakiwa kutatuliwa.
Sawa mkuu acha tukubaliane kutokubaliana.
 
Unaongea kitu usichokijua network ya bara bara Tanzania ipo juu mno Kama unasafiri kwa nchi zingine za kusini hata East Africa sisi tupo juu ukiondoa SA na Botswana ila zingine hapo hakuna wa kutufananisha na mfumo wa bara bara mikoa mingi imeunganishwa na kiwango cha lami kasoro kipande kidogo huko kigoma kuitafuta nyakanazi na kuingia kigoma yenyewe...
Sawa mm sifahamu ninachoongea, tufanye ww upo sahihi maana mm nakueleza uwezo wa barabara zetu kama nchi kuhimili idadi kubwa ya magari ww unaongelea network ya barabara ukilinganisha na nchi zingine, Hatutaelewana.
 
Back
Top Bottom