[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu sifahamu lolote kuhusu namna Inflation inakuwa Exported, Tafadhali nijuze how inflation is Exported.
Nitashukuru[emoji120]
Sent from my SM-G920F using
JamiiForums mobile app
Ok iko hivi
Tuanze na inflation ya ndani ya nchi
[emoji116]
Mfano. Nchi ya tanzania pekee, ina mali( mazao, maji, nguvu kazi, entertainment, usafiri, etc) zenye thamani ya trilion 5. Lazima u print pesa iwe sawa na thamani ya mali na nguvu kazi ya uzalishaji.
Turudi kwenye basic concept.
[emoji116]
Kabla ya pesa watu walikua wanabadilishana vitu.
Bank kwa usimamizi wa serikali ika print pesa. Watu wakawa wanapeleka mali bank wanapewa pesa. Wengine nguvu kazi wanapewa pesa. Wengine walinzi wa pesa wanapewa pesa. Wengine wakawa viongozi wakawa wanapewa pesa.
Mwisho mpaka pesa yote ikaingia kwenye mzunguko na bank ikabaki na pesa "0". Lakini ikawa na mali za kutosha. Bank nayo ikajikuta kwenye mzunguko ule ule, ikawa inatoa mali kupata pesa. Na kutoa pesa kupata mali. Mambo yakaendelea.
Twende kwenye concept inayofuata
[emoji116]
Kwa mazingira hayo, mfano tuna serikali x, serikali x ikawa na matumizi mabaya ya pesa mpaka ikaishiwa pesa. Ikaamua kuprint pesa nyingi ili iendelee kua na nguvu. Lakini kumbuka pesa ya mwanzo ilikua na thamani sawa na uzalishaji na mali, unapoongeza mapesa mengi kwenye mzunguko, pesa inaanza kukosa thamani. Kwa sababu unatengeneza watu wengi wasiofanya kazi ila wanataka huduma za kijamii na mali. Kwa hiyo pesa itakosa thamani na uzalishaji utakua mgumu. Kwa sababi kila mtu ana pesa na ukishakua na pesa kazi haifanyiki unatafuta mtu wa kumnyonya na kumtuma. Lakini ingekua inaendana na mali na uzalishaji ingekua na thamani na ngumu kupatikana.
Twende kwenye kuhamisha inflation
[emoji116]
Mfano, serikali x ina uwezo mkubwa wa kucontrol serikali zote duniani, ikaamua badala ya hizi hela tulizo print kuziweka kwenye nchi yetu, tuziweke kwenye mzunguko wa hela wa dunia. Yani hela ya serikali x inaweza kununua kitu chochote kwenye serikali yoyote ila hela serikali yoyote haiwezi kununua kitu kutoka serikali x mpaka serikali x imruhusu na ikimruhusu inabidi alipie hiyo service.
Je umeelewa au umeshindwa kuelewa wapi?