Ruge Opinion
JF-Expert Member
- Mar 22, 2006
- 1,838
- 705
Jibu la Mchumia Tumbo ndilo sahihi. Ofisi ya CAG inakaguliwa na kampuni ya ukaguzi wa mahesabu iliyoteuliwa rasmi kwa kazi hiyo. Na CAG anakagua taasisi zote za kiserilkili (wizara, idara, halmashauri, mashirika ya umma, n.k.) yanayopokea fedha kutoka kwenye hazina ya serikali na ambayo kisheria yana sifa ya kuwa taasisi za umma. Katiba ya TZ na sheria kama zilivyoainishwa na Mchumia Tumbo zinatoa ufafanuzi wote kuhusu hadhi na kazi za Ofisi ya CAG.