Nani anayetajwa na Mwenyekiti wa CCM Mwanza, Dkt. Diallo kwamba ana faili Hospitali ya Akili Milembe?

Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr Anthony Diallo kwamba alikuwa na jarada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Je, ni TAL wa Chadema?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Unafiki wa wana CCM, mkumbuke aliyetoa haya matamshi ni Mwenyekiti wa CCM wa MKOA
 
Milembe mtu yeyote anaweza kwenda kwani ukichaa unaweza kuupata muda wowote na kwa umri wowote, so atulie asitupigie kelele, kama ndo ameanza kujipigia kampeni apate uwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza mwakani aseme!
 

Janja janja na wizi wizi ni mtindo wa maisha ndani ya uongozi wa CCM. Ndicho kivutio kikuu kwa anayefanikiwa kuipata nafasi ya uRais wa JMT na uenyekiti wa CCM pamoja na genge lake (timu ya ushindi).

Rais pekee aliyekemea ufisadi/rushwa kwa dhati ni JK Nyerere pamoja na udhaifu wake wa kutamani CCM itawale milele. Alikuwa mdhanifu (idealist) kweli kweli. Pamoja na janja yake yote hakuamini kuwa binadamu anayejithamini anaweza kuwa na lengo la maisha la kutafuta pesa/utajiri tu hapa duniani. Alikuwa akidai watu wa aina hiyo ni wapumbavu kabisa[emoji1787]. Alishangaa sana (genuinely) kuwa mtu anakimbiliaje Ikulu ambako ni “mzigo”?; Kuna biashara gani ambayo hakuwahi kuiona miaka 27 ya uwepo wake pale?! Huyo alikuwa JKN.

Awamu zote zilizofuatia ikiwemo ya JPM ni “kutesa kwa zamu”. Ufisadi mkubwa (wa kitisho) umekuwa ukifanywa kwa kuratibiwa/kuungwa mkono na Ikulu. Aliye madarakani ndiye anayewaita wengine wasio wa kundi lake: “mafisadi”, “wahujumu uchumi”, “wezi”, “wala rushwa”, n.k. Anaamua watu wa kukamatwa na kuwekwa ndani, wa kutoguswa, kesi za kwenda mahakamani, mwenendo wa kesi na hukumu zake. Kleptocracy ni kama imehalalishwa na kufanywa “haki ya Rais”!

JPM alipiga pin wengine lakini yeye na genge lake walikuwa wakijichotea na kutumia hazina ya taifa wanavyotaka na kujiita “wazalendo”. Vyombo vya habari vilibanwa. Serikali pekee ndiyo ikawa inaongea propaganda tupu ikiwa ni pamoja na uongo mwingi.

Serikali inabadilika tu tunaanza kusikia uozo wa awamu iliyotangulia na kuombwa “tuwe wavumilivu wakati Rais mpya anarekebisha mambo”! CCM ile ile, WTF!
 
Diallo amesema alimuuliza katelephone, raha yako iko wapi kuishi na mabunduki zaidi ya 20. Unawajua wameamkaje huko walikotoka?

Diallo ameonyesha kukerwa sana na mfumo wetu
 
Huyo mzee naye ni muoga sana anaongea sasa wakati mwendazake akiwepo alikuwa ameufyata!
Sio mtu wa kumtilia maanani.
 
Ni bora rais mwenye file mirembe anayeonesha njia kuliko wewe mwenye file muhimbili usiye na mbele wala nyuma
Siku mwenye file milembe akimbaka mamaako ndo utajua kupi ni kupi kati ya mirembe ns muhimbili
 
Binadamu unapoongea lazima uwe na kiasi. Lazima upime hicho unachoongea kitakusaidia nini katika hustle zako ama kitakughalimu nini katika mahusiano yako na watu wengine.

Diallo kateleza, matamshi yake yaweza kuwa na negative impacts kwake hasa mahusiano yake na chama chake. Sidhani kama atapata uenyeki wa chama pindi muhula wake ukiisha. Kaanzisha mgogoro usiokuwa na faida yoyote kwake.

Mark my words.
 
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr Anthony Diallo kwamba alikuwa na jarada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Je, ni TAL wa Chadema?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Kuna mgombea urais huko botiswana,baada ya mmewe kuteuliwa agombee, alisemaga wazi kuwa,"mmemchagua huyo kichaa.."
Yule mama hawakumsikia..
Leo botwaeana inaendeshwa na mental case..
 
Diallo naye nina mashaka na utimamu wa akili yake, kwa nini hataki katiba mpya
 
Hao wasio na mafaili afadhali maana wanaweza kupewa benefit of doubt. Hata wewe au Mimi mtu aweza kuangalia mambo yetu akaona ni ya kiendawazimu lakini akatupa benefit of doubt. Sasa issue ni zile confirmed cases tena zinazotuthibitishia tena kwa kutamba majukwaani kuwa ni confirmed mental cases za mirembe
 
Ndio maana alipata promotion, kazi yake ilitisha sana mkuu. Najua huko aliko, anaowaongoza kama alivyotabiri mwenyewe wanafurahia sana.
 
Ni sawa kabisa kwani hii ndio hulka ya CCM kuwamaliza wale wote wanaosema ukweli. Ile ahadi namba nane ya nitasema kweli daima uongo kwangu mwiko ilizikwa mwaka 1992 kule Zanzibar.
 
Bado najiuliza huyo mwanasiasa aliyetajwa na Dr Anthony Diallo kwamba alikuwa na jarada hospitali ya Mirembe ni nani?

Na kwanini mifumo ilimruhusu kugombea?

Je, ni TAL wa Chadema?

Nawasalimu kwa jina la JMT!
Mara hii umesahau au ndio kujifanya tu.?!
Mwendawazimu: mimi ni kichaa nateua vichaa kama mimi.
Ndugai: mimi ni kichaa ninafaili milembe.
CCM = VICHAA Washenzi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…