Nani atakuwa mbadala wa Maalim Seif kwa Siasa za Upinzani upande wa Zanzibar?

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Posts
3,858
Reaction score
5,101
Maalim Seif alikuwa mwanasiasa wa upinzani ambaye ameleta na kukuza upinzani huko visiwani Zanzibar na inasemakana ameshinda Mara kadhaa ingawa chama tawala hakikuwa tayari kumtangaza kuwa ndiye mshindi.

Jua lilichomoza na Sasa just limezama, Maalim nguvu na pumzi vimemuishia kiasi kwamba Sasa Uchaguzi uliofanyika mwaka ambao alishindwa vibaya kuliko miaka mingine yote, utakuwa Ni Uchaguzi wake wa mwisho kushiriki kinyanganyiro Cha Urais.

Je, ni nani mbadala wake ambaye ataweza kutikisa Kama au kuliko hata Maalim katika siasa za upinzani za Zanzibar?
 
Nasoro Mazrui na yule aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali akajiuzulu wakati wa bunge la katiba.
 
3678901.jpg
 
Ni zamu ya CHADEMA kuweka mizizi visiwa, naona kama Salum Mwalimu wa CHADEMA anaweza.
 
Hakuna aliyekuwa mpinzani mwenye mvuto na ushawishi kwa Wazanzibar kama huyu mzee.

Wazanzibar wamejenga imani na mtu huyu miaka sasa, hivyo kwa upande wangu naona atatafuta tu mbinu mbadala kuwaridhisha na ili imani yao kwake ibaki , japo haitakuwa kama hapo awali

Hivyo Seif naona bado ni mpinzani uchwara kama kawaida yake.

#jr
 
Hakuna aliyekuwa mpinzani mwenye mvuto na ushawishi kwa wazanzibar kama huyu mzee.

Very true
 
Sasahivi mzee anakula na kusaza hapati tabu tena
 
Maalim Seif alikuwa mwanasiasa wa upinzani ambaye ameleta na kukuza upinzani huko visiwani Zanzibar na inasemakana ameshinda Mara kadhaa ingawa chama tawala hakikuwa tayari kumtangaza kuwa ndiye mshindi.

Jua lilichomoza na Sasa just limezama, Maalim nguvu na pumzi vimemuishia kiasi kwamba Sasa Uchaguzi uliofanyika mwaka ambao alishindwa vibaya kuliko miaka mingine yote, utakuwa Ni Uchaguzi wake wa mwisho kushiriki kinyanganyiro Cha Urais.

Je, ni nani mbadala wake ambaye ataweza kutikisa Kama au kuliko hata Maalim katika siasa za upinzani za Zanzibar?
Kwani yeye kashift chama?
 
Ila Seif aisee 1995, 2000, 2015 watu walimpa heshima aliyostahili
Sasaivi umri unampa mawazo..
Zitto siasa za kula ndio maisha yake
CDM imngoe Jussa ikiweza
 
CHADEMA wanaitamani sana Zenji ila wapemba na wachaga hawawezi kaa zizi moja, wote wabinafsi na wakabila hivyo msitegemee kupata chochote huko.
Heche ni Mchaga,bulaya ni Mchaga,sugu ni Mchaga,Prof Safari ni Mchaga.? Chuki dhidi ya wachaga imeongezeka sana kipindi hiki.Social-cultural backround imewafikisha hapo walipo (Wachaga na wasambaa wa milimani wana hali almost sawa-Baridi kali,kufikiwa na wazungu mapema,shule za mwanzo lakini wasambaa wako nyuma mno ukilinganisha na wachaga.)
 
Dogo tu hilo,mbona mifano ipo mingi,akiondoka anaingia mwengine hata alshababu wanaweza kuingia na kuungwa mkono,kushinda anavyoungwa mkono Maalim Seifu.
mapenzi kama majani yanaota hata ndani ya maji au angani.
 
Hakuna aliyekuwa mpinzani mwenye mvuto na ushawishi kwa wazanzibar kama huyu mzee.
Wazanzibar wamejenga imani na mtu huyu miaka sasa, hivyo kwa upande wangu naona atatafuta tu mbinu mbadala kuwaridhisha na ili imani yao kwake ibaki , japo haitakuwa kama hapo awali
Hivyo Seif naona bado ni mpinzani uchwara kama kawaida yake.

#jr
Kuna mbinu nyingi zakumlegeza mtu na mojawapo ni kumpelekea ujumbe wa mtu anayemwamini sana.Hebu tuwaze hivi-Wapinzani wote wameweka nguvu katika mataifa ya Magharibi kuwa angalau yanaweza kukemea yaliyotokea katika Uchaguzi.Ghafla Seif anatumiwa ujumbe na balozi wa Marekani kumuelekeza (kwa lugha laini)kuwa ni bora aingie ndani ya seriakli haramu akapaginie anayoyataka ndani ya serikali kuliko kuwa j.Seif anahakikishiwa ya kuwa Marekani bado inam support na ina sympathise naye katika madhila yaliyomkuta.Je,Seif anaweza kukataa ushauri huo?
Nadharia ya pili ni kuwekwa kati na kuambiwa ukweli hasa kama hivi "Mheshimiwa kwa umri wako liwake jua lisiwake jua huwezi kupata U rais wa nchi hii.Pia Mheshimiwa ustawi na usalama wa nchi yetu ni muhimu zaidi kuliko wewe na katika uchaguzi uliopita una makosa makubwa manne ulifanya na ushahidi ni huu hapa (unaweza ukasoma na hata ukachukua kwani nakala zipo nyingi).Ni juu yako kuamua kushirikiana na serikali au la,Tutakuja Jumanne kuchukua majibu au ukiwa tayari tujulishe kwa namba hii hapa"
Kipindi cha Seif ndio kimefikia kikomo,anaingia serikali akiwa amevujika moyo ingawa itabidi aweke tabasamu la plastiki.
Haya ndiyo maisha yetu wanadamu.
Kwa raia wa kawaida kuna wakati tuatakiwa turudi nyuma tuache mambo yaende kama wanavyotaa wakubwa,kupimana nguvu na upepo hakuna faida kwa sasa.
Walio na mawazo tofauti na CCM wataendelea kuwepo na watatfuta njia nyingine ya kuonyesha tofauti zao.
 
Ni zamu ya CHADEMA kuweka mizizi visiwa, naona kama Salum Mwalimu wa CHADEMA anaweza.
Huzijui siasa za Zanzibar, labda ukipata muda wa kukaa na Lipumba muulize atakuelewesha vizuri.

Kama kuna Mtanganyika ambaye angeweza kuwa na influence Zanzibar ni Profesa Lipumba.
 
Maalim Seif alikuwa mwanasiasa wa upinzani ambaye ameleta na kukuza upinzani huko visiwani Zanzibar na inasemakana ameshinda Mara kadhaa ingawa chama tawala hakikuwa tayari kumtangaza kuwa ndiye mshindi.

Jua lilichomoza na Sasa just limezama, Maalim nguvu na pumzi vimemuishia kiasi kwamba Sasa Uchaguzi uliofanyika mwaka ambao alishindwa vibaya kuliko miaka mingine yote, utakuwa Ni Uchaguzi wake wa mwisho kushiriki kinyanganyiro Cha Urais.

Je, ni nani mbadala wake ambaye ataweza kutikisa Kama au kuliko hata Maalim katika siasa za upinzani za Zanzibar?
Fatma Karume
 
Back
Top Bottom