Nani atakuwa mbadala wa Maalim Seif kwa Siasa za Upinzani upande wa Zanzibar?

Tanzania kuna upinzani uchwara. Kazi ya upinzani imekuwa kutisha, kupinga, kutukana, kuongea hovyohovyo, siasa za chuki, kutokuaminika, kununuliwa, kutokuwa na msimamo, kutokuwapo kwa ustaarabu na kutia watu hofu.

Approach ya upinzani katika siasa ni mbovu ndiyo maana wanaifanya ccm iwe defensive sikuzote ikiogopa upinzani. Ccm inaamini kwamba upinzani ukichukua madaraka, wale wote waliofanya uovu ndani ya ccm watakwenda ndani na kutaifishwa mali zao. Kwahiyo, ccm haiwezi wapa nafasi upinzani kabisa maana ni threat kwao. Ebu fikirieni, chadema itawale alafu wakina Kikwete, IGP na Magufuli watabaki salama?

Mawazo yangu, Ili upinzani uwepo Tz inabidi ccm igawanyike mara mbili wapingane wenyewe kwa wenyewe kwa ustaarabu.

Sent from my SM-G981B using JamiiForums mobile app
 
Sasahivi mzee anakula na kusaza hapati tabu tena
Hatakama ningekuw mimi lazma ningekubali uteuzi. Kwanza umri umemtupa mkono then hata uhakika wa kushinda huo urais hana , so apige bata tu kwenye v8 ghost
 
Huzijui siasa za Zanzibar, labda ukipata muda wa kukaa na Lipumba muulize atakuelewesha vizuri.

Kama kuna Mtanganyika ambaye angeweza kuwa na influence Zanzibar ni Profesa Lipumba.
Watu wengi humu ni vitoto vya mwaka 95/2000.

Siasa za Zanzibar, ni siasa za damu, dini, utaifa, uarabu, uunguja na upemba.

Agenda yao kubwa ni utaifa.

Watu wanataka nchi yao.
 

Nilimjibu mwamba mmoja humu nadhani bado ni relevant:




Hii ikawa bakshish:

Vita sasa mumo mumo, hongera bwana Hamadi,
Walidhani huna kimo, wakuchomeshe mahindi,
Itahitajika Omo, kuusafisha ushindi,
Ndani sasa yuko Sefu, pa kuficha pawe papya!

Haya yote tokea hapa:


Umri Seif umeenda. Tuombeane uzima. Seif ni mwana halisi wa Zanzibar. Hakuna kuu au dogo litakalo ufifisha ukweli huo.
 
hatakama ningekuw mimi lazma ningekubali uteuzi. Kwanza umri umemtupa mkono then hata uhakika wa kushinda huo urais hana , so apige bata tu kwenye v8 ghost
Mandela angekuwa na mawazo kama yako mpk leo SA ingekuwa bado chini ya makaburu
 
Huzijui siasa za Zanzibar, labda ukipata muda wa kukaa na Lipumba muulize atakuelewesha vizuri.

Kama kuna Mtanganyika ambaye angeweza kuwa na influence Zanzibar ni Profesa Lipumba.
Salum Mwalimu ni mbara mkuu?
 
Mm hapa na mkiniunga mkono nitafanya mengi
 
Noted
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…