kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,892
- 7,780
Nimeona clip za video za baadhi ya watu wanaodai kuteswa na Sabaya. Zaidi ya madai yao hawaelezi wameteswa wapi na kwa sababu gani. Sabaya alikua Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya. Kwenye kamati hiyo wako wakuu wa vyombo vya ulinzi. Clip za Sabaya akienda kukamata au kupeleleza zinaonyesha wakikuta muhalifu anawakabidhi wahusika kisheria kushughulikia.
Usalama kwenye upelelezi hakuna asiejua wanatumia pia mbinu ya kumpiga au kumtesa mshukiwa kupata ushahidi. Kwenye jimbo la Hai Sabaya amepambana na uhalifu mkubwa wa aina mbalimbali na ukwepaji kodi mkubwa. Hili ni jimbo Mbowe kiongozi wa upinzani alitaka kuonekana kama ni mfalme.
Kwa maoni yangu wengi waliyotiwa kibano kwa kushukiwa na uhalifu au fujo za kisiasa wanamuona sabaya ndio adui na mtesi wao wakati wamehusishwa na uvunjaji wa sheria.
Serikali hii ya samia imeliendea kwa papara swala la sabaya kwa kufuata fitna za chuki. Kuna wapinzani wanaamini yeye ni mtu wao aliyekua chini ya magufuli hivyo wamemletea fitna za uongo.