Nani hasa anastahili kubeba BALLON D'OR

Nani hasa anastahili kubeba BALLON D'OR

King Muhil III

New Member
Joined
Jul 23, 2018
Posts
1
Reaction score
1
Baada ya mashindano ya kombe la dunia kumalizika ambapo tumeshuhudia Ufaransa na Croatia wakicheza fainali na hatimaye Ufaransa kutawazwa mabingwa wapya,Bila ubishi nakubali walistahili.

Kwa sasa pamekuwa na mijadala ya nani anastahili kutwaa Ballon D'or.Majina yanayokamata ni Ronaldo, Mbappe, Modric, Neymar, etc.

Nashangaa vipi Mo Salah na Messi kwa sasa ni kama wanasahaulika kwa kipindi kifupi tu tangu ligi ya ya mabingwa kumalizika miezi 2 tu iliyopita ambapo Ronaldo, Messi na Mo salah ndio waliokuwa wakitajwa zaidi.

Kwangu mimi Ligi ya mabingwa Ulaya ni ngumu kuliko world cup ambapo takribani mechi 7 tu tayari bingwa anapatikana tofauti ligi ya mabingwa ambapo inaenda hadi mechi 16.

Nini maoni yako juu ya nani anastahili kutwaa ballon d'or kwa kuzingatia sababu za kiufundi na kitakwimu na uzito wa mashindano kwa wachezaji hao..?
 
Last edited by a moderator:
wampe griezman kabeba europa na world cup, ila kiukweli hakuna mchezaji aliefny vzuri sn kustahili hii tuzo km miaka mingne iliopita
Verane kabeba UCL na WC, sema mara nyingi vigezo vya Ballon d'or vinawabeba Messi na Cr7. usishangae Cr7 akabeba tena na mwakani kama Juve watachukua UCL
 
Verane kabeba UCL na WC, sema mara nyingi vigezo vya Ballon d'or vinawabeba Messi na Cr7. usishangae Cr7 akabeba tena na mwakani kama Juve watachukua UCL
Cr7 anasitahi, coz mechi nyingi yuko on fire. Wold cup peke haiwez kuamua best player, all competition inahusika sana
 
Mimi nikatika watu napinga sana zawadi za mtu mmoja maana mpira ni team hakuna mtu mmoja hizo zawadi za mchezaji bora wangepeleka Tennis huko au boxing. Football ni wachezaji 11 ndani. maana siku hizi uchambuzi umezidi mpaka umiliki wa mpira percentage sijui pass ngapi mambo mengi mengi mpaka imekuwa tunabishana nani kapiga pass nyingi badala ya nani kashinda. Mimi nitabaki tu magoal ndio mpira haya mengine sijui mchezaji bora sijui pass ngapi upuuzi tu. tumeona ya Messi akicheza Barca utasema huyu hatari lakini akienda kucheza team ina watu wa kawaida na yeye anapotea.
 
Back
Top Bottom