Nani kachora Nembo ya Taifa kati ya Ngosha, Kabati au Farahani?

Nani kachora Nembo ya Taifa kati ya Ngosha, Kabati au Farahani?

Ukisoma tafiti na maelezo ya watu wengi wanaodai ni wabunifu wa nembo ya Taifa la Tanzania utaona kuwa hakuna hata mmoja ambaye ushahidi unamhalalisha kuwa ndie mbunifu wa nembo ya Taifa.

Mfano

1957 Mbunifu ni Marehemu Francis Maige Kanyasu (Ngosha) pamoja na wenzake
1960 Mbunifu ni Marehemu Jeremiah Wisdom Kabati - ushahidi -= familia yake wakiri
1964 Mbunifu ni Marehemu Abdalah Farahani - Tafiti za Profesa wa Chuo Kikuu

Maelezo ya mzee Francis Ngosha
Mzee Francis Maige Kanyasu kujitambulisha kuwa yeye na mzee Ali Panga kuwa ndio waliyoichora nembo ya taifa,
Maelezo ya familia ya marehemu Jeremiah Wisdom Kabati
Familia ya mzee Jeremiah Wisdom Kabati mke wake na mtoto wake kujitokeza na kudai kwamba baba yao mzee Jeremiah Wisdom Kabati ndiye aliyechora nembo ya taifa wakiwa wanaishi Tabora na wakati huo baba yao akiwa ni mwalimu.

Utafiti wa Profesa Elias Jengo
Elias Jengo
ambaye ni Profesa Mshiriki Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akifundisha Historia ya Sanaa na Kuchora ambaye anaeleza:
“Kumbukumbu yangu ni kwamba kwenye miaka ya 90 hivi nilikuwa Zanzibar nikaonana na Iddi Farhan – mtoto wa Abdallah Farhan. Abdallah Farhan msanii mashuhuri sana…”
Profesa Jengo anaeleza kuwa zipo michoro ambayo mzee Abdallah Farhan ameiacha ambayo inaonesha kuwa yeye ndiye alichora Nembo ya Taifa ambayo aliiona kupitia kwa Iddi Farhan mtoto wake

“Akanionesha kazi za baba yake, nikamwambia hii michoro yote mpaka Nembo hii ya Taifa ni kazi ya mzee?

Akasema ‘ndiyo hii ni kazi ya mzee. Baba yangu ndiye aliyefanya kazi hii.’ Kwa hiyo, mimi nafundisha wanafunzi wangu kwamba mchoraji wa kwanza wa Nembo ya Taifa katika Tanzania ni mzee Abdallah Farhan.”

– Prof. Jengo.

Utata wa Nembo mBili

Hata hivyo Profesa Jengo anasema utata upo pale ambapo haijabainika mzee Abdallah Farhan alichora Nembo ipi kwa sababu zipo mbili:

“Ziko Nembo mbili – Nembo ya Uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 mpaka 1964

Nembo ya Tanzania baada ya Muungano tangu 1964 mpaka leo.

Ziko Nembo mbili tofauti. Je, Abdallah Farhan alichora zote mbili, ama hii ya Muungano?”
– Prof. Jengo.

Utata mwingine ambao Prof Jengo hakuona ni kwamba je kama Abdalah Farhani alikuwa na michoro hiyo kwa sababu alikuwa anafanya mazoezi kwa michoro ambayo imeshatokea? na tena ni mwaka 1964 wakati huo nembo ya kwanza ya 1961 ilishachorwa?

Swali akwa Serikali

Je serikali imepoteza kumbukumbu zote za zamani kwa matukio muhimu kama hili la Nembo ya Taifa? Maana kama mbunifu ni yule wa nembo ya Tanganyika lazima atakuwa huyo huyo kwenye nembo ya pili ya Tanzania kwa sababu hizo nembo mbili zimefanana kiubunifu

Ushauri kwa Serikali

Serikali ianze sasa kufuatilia mambo yote ya kale sio tu haya ya nembo ya Taifa. Matukio hayo na ushahidi wake uhifadhiwe sehemu moja kwa ajili ya vizazi vijavyo
 
Nani Kachora Nembo ya Taifa: Mzee Farahani (Farhan), Ngosha, au Jeremiah Wisdom Kabati?

Kuna wanaosema Mzee Jeremiah Wisdom Kabati kachora nembo ya Taifa. Wengine wanasema Mzee Ngosha kachora. Kwa sasa mimi nipo upande wa Professor Elias Jengo anayesema nembo ilichorwa na Mzee Abdallah Farahani kutoka Zanzibar. Professor Jengo aliandika kwenye kitabu kwamba Mzee Farahani ndio aliyechora nembo ya Taifa. Inasemekana mtoto wa Mzee Farahani, Iddi Farahani alikuwa na sketches za baba yake za hii nembo. Mzee Farahani alisoma na Mwalimu Nyerere Makerere. Professor Elias Jengo kutoka Chuo Kikuu anaandika kwenye kitabu “East Africa Art Biennale” kwamba “As a designer, Abdallah Farahani will be remembered for his design of the national emblem. The emblem was recently criticized by a legislator for depicting barefooted human figures.” Ukurasa 44. Kaka Dominicus Makukula, msanii na mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anaamini kwamba Mzee Furahani ndio aliyechora ile nembo ya taifa. Anasema mjukuu wa Mzee Farahani yupo Music Academy Zanzibar na pengine anaweza kutoa majibu kama kuna atayeweza kwenda kuongea nae zaidi. Mpaka tutapopata habari zaidi, inaonenaka kwamba Mzee Farahani kutoka Zanzibar ndio aliyechora ile nembo. Tusubiri tuone kama serikali itafuta mavumbi na kufungua maboksi yenye nyaraka husika.

FACT NUMBER 2

Tukiangalia nembo hii ya Tanganyika 1961, ile ya Tanzania 1964 na ule mchoro usio na rangi uliopo katika nyaraka ya National Flag and Coat of Arms Act ya 1971, tunapata nafasi na sababu ya kudhani kuwa mchoraji na mbunifu halisi wa nembo ya Taifa si Ngosha wala marehemu mzee Jeremiah Kabati. Familia ya kabati inasema mzee alichora nembo hiyo mwaka 1960 na katika mahojiano na TBC Taifa, Ngosha alisema kuwa alisanifu nembo hiyo na mwenzake mwaka 1957. Prof. Jengo anathibitisha kuwa mchoro wa Farahani kwa ajili ya Tanganyika uliandaliwa mwaka 1961 na kuboreshwa 1964 wakati wa maandalizi ya nembo ya Jamhuri ya muungano. Swali la msingi, je yawezekanaje pasiwe na kumbukumbu hali miaka kumi baadae, marehemu Mwl. Nyerere alipatiwa mswada wa sheria ya nembo ya Taifa ileile ya mwaka 1961 pia 1964 (isiyonakshiwa kwa rangi) kwa ajili ya kuisaini ili iwe sheria kamili. Je walioandaa mswada walitoa wapi blue print ya nembo halisi mwaka 1971? Tatizo si kukosekana kwa nyaraka wala kumbukumbu, bali tatizo ni kukosekana watu wenye weledi kweye eneo la historia ya sanaa katika kuhifadhi amali hizi za Taifa katika mamlaka za kusimamia sanaa na utamaduni wa Taifa. mzee Mbughuni Sr. alifanya kazi kama Promoter of national arts miaka ya 1960s na hatimaye kuwa mkurugenzi wa idara ya sanaa miaka ya 1970s mwishoni, alianzisha Chuo cha Sanaa Bagamoyo mwaka 1981 baada ya kuvunja kikundi cha sanaa cha Taifa mwaka 1979 (Kelly Askew 2005:304-309), hawa ndio aina ya watu tuliowakosa katika miaka hii Tanzania...

Imechukuliwa kutoka bandiko la Azaria Mbughuni
May 26, 2017
Mkitaka ukweli wa jambo hili tafuteni jina la aliyebuni coat of arms za Kenya na Uganda. Halafu mkimtaja ndipo tutaongea vizuri. Kwasababu nchi hii haithamini michango ya wabunifu, hasa kwenye sanaa.
 
Kwakua hatukujua kua jiwe anapenda sifa weng tuliamni kua ni ngosha lkn sasa hv tumeshamjua kwaio hio nembo aliyechora ni mzee Farahani
 
Francis Maige kanyasu "Ngosha"
View attachment 1776128
Ni Mbunifu na mchoraji wa nembo ya Taifa (yenye bibi na bwana).
View attachment 1776129
Francis Ngosha alizaliwa mkoani Mwanza mnamo mwaka 1931 na kufariki dunia mwaka 2017.
Je, serikali inamuenzi vipi mtu huyo aliye chora Nembo ya taifa?
Alifanya kazi ambayo hakulipwa?

Na kama atakuwa alilipwa, je ni stahili gani zingine ambazo alistahili lakini akanyimwa?

Je ni kanuni ipi inayofuatwa kwa msanii ama mfanyakazi yeyote anayekuwa kalifanyia taifa kazi ya kuonekana?

Embu fafanua kidogo, ni jambo gani alistahili taifa limfanyie kwa kazi hiyo ya sanaa?
 
Back
Top Bottom