Nani kachora Nembo ya Taifa kati ya Ngosha, Kabati au Farahani?

Nani kachora Nembo ya Taifa kati ya Ngosha, Kabati au Farahani?

Watanzania ccm sijui imeturogaje yani kuhusu swala la kumbukumbu hatuna kabisa. Mfano kuna mchezaji kumbukumbu ya kupigwa kadi tatu mpaka leo imekuwa kitendawili? Maisha chini ya serekali ya ccm ni magumu ila siku ya kupiga kura watu watapotezaa kumbukumbu ya njaa wataipa kura ccm tena dah!
Mbona unakiuka kauli za viongozi wako? Lowassa na mbowe wanasema ccm haikushinda.
 
Kitu ambacho ni ngumu kuelewa ni kubuni na kichora. Lakini Mzee Ngosha nilimsikia akisema walichoa akiwa na mwe zake anaitwa Ally Pangani inasemekana yupo Tanga
 
Ni vigumu kujua who was who.. Kwa bahati mbaya waliokuwepo wakati huo ambao wangetupatia ukweli wa jambo hili hatunao tena..
Kwa bahati mbaya pia hatukuwa na uwezo wa kutunza kumbukumbu ya mambo mazuri kama haya.. Ubishani ukizidi na ukweli kukosekana bora ibuniwe nembo nyingine ili kuondoa utata..
 
Sijakupangia cha kuamini, halafu uwe na adabu...akafi ka ndope..
Mtoto kama ni matusi kamwambie bi mkubwa wako. Hivi wewe kama si utoto ni nini. Ushinde kuamini nyalaka iliyotolewa na katibu kiongozi Ikulu ya nchi yako. Ukaenda kuamini maelezo ya mpumbavu mmoja jf. Jamani tendeeni haki akili zenu hata mbwa hawezi kudanganywa kama wewe.
 
Kuna tatizo la wababa kujisifia nyumbani uongo hili ni shida sana. Farhani kaenda kajisifu nimechora mimi mpaka sketch kapeleka, Kabati nae kajisifu kwa Mkewe uongo.

Ngosha amechora na hadi sasa ni mchoraji hakuwahi kuongea
 
tunasikitisha ila ni rahisi kwa mtanzania kukutajia listi nzima ya kikosi cha Arsenal mwaka 1995.
Kikosi cha Arsenal mwaka 1995 ni juzi tu, waliopoteza kumbukumbu mi waliokuwepo mwaka 1960 ambao huwezi kuwalaumu umri umepindukia .
 
Rais ndiye alipaswa kuweka kumbukumbu hii??? Hebu fikiria vizuri aisee... Nadhani wazazi wako wangekuwa wameelimika wangekuwa msaada mkubwa pia na kuliona hili... Kiasi kwamba, leo usingekuwa wafikiria haya!

Sijaona neno "Rais" kwenye mchango wake.
 
Mtoto kama ni matusi kamwambie bi mkubwa wako. Hivi wewe kama si utoto ni nini. Ushinde kuamini nyalaka iliyotolewa na katibu kiongozi Ikulu ya nchi yako. Ukaenda kuamini maelezo ya mpumbavu mmoja jf. Jamani tendeeni haki akili zenu hata mbwa hawezi kudanganywa kama wewe.
Ni punguani tu ambaye hutegemea matusi na kashfa kujenga hoja zake. Kuna wajinga kama wewe waliamini serikali haikosei wakapitisha sheria zilizoruhusu mikataba hatari kabisa kwa uchumi wa taifa. Wenzao walipowakosoa Nao walijinasibu vivo hivyo kuwa mnadhani ninyi mna akili na mnajua kuliko serikali. Leo yako wapi?
Na ukumbuke wanaolaumiwa Sasa si wananchi wa kawaida, ni kuanzia bunge la kipindi hicho na serikali nzima. Leo hii unataka kujenga hoja za kitoto kabisa kuhusu wa kumuamini!? Hata aliyeondolewa sio mwana JF Bali ni waziri wa serikali, ambaye alikuaa akiiwakilisha sserikali kwetu na tulimuamini lakini mkubwa wake kamuona hafai.
Halafu JF uusiichukulie kwa dharau hivyo, jiulize kwanza kwa nini wewe ni mmoja wa hao wana JF?
County yourself lucky kwamba nimepoteeza muda wangu kukujibu.
 
NGOJENI KWANZA NGOSHA ATIBIWE.MSIANZE KUTUCHANGANYA.BAADAE TUTAJUA NANI KACHORA PICHA YA KWANZA YA BABA WA TAIFA
 
Tanzania raha sana ntawambia Mimi ndo niliyetengeneza kitambaa na rangi ya bendera ya taifa nimepaka Mimi ngoja wandishi wa habari wanikute nimezidiwa
 
Ni punguani tu ambaye hutegemea matusi na kashfa kujenga hoja zake. Kuna wajinga kama wewe waliamini serikali haikosei wakapitisha sheria zilizoruhusu mikataba hatari kabisa kwa uchumi wa taifa. Wenzao walipowakosoa Nao walijinasibu vivo hivyo kuwa mnadhani ninyi mna akili na mnajua kuliko serikali. Leo yako wapi?
Na ukumbuke wanaolaumiwa Sasa si wananchi wa kawaida, ni kuanzia bunge la kipindi hicho na serikali nzima. Leo hii unataka kujenga hoja za kitoto kabisa kuhusu wa kumuamini!? Hata aliyeondolewa sio mwana JF Bali ni waziri wa serikali, ambaye alikuaa akiiwakilisha sserikali kwetu na tulimuamini lakini mkubwa wake kamuona hafai.
Halafu JF uusiichukulie kwa dharau hivyo, jiulize kwanza kwa nini wewe ni mmoja wa hao wana JF?
County yourself lucky kwamba nimepoteeza muda wangu kukujibu.
Kukosea na kupatia ni relative terms kwa hiyo si kitu cha kuniumiza kichwa. Kwa kuwa wengi wanaiunga mkono serikali ni wazi kuwa wengi wanaona hakuna makosa yaliyofanyika kwenye mikataba na sheria. Tatizo lililopo ni kwa wasimamizi kukosa uthubutu kusimamia mali ya umma kama wenye mali.
Mkataba hausemi kupunguza thamani ya mali iliyozalishwa. Nani wa kumuamini mwenye uzalendo wa kweli atakayesimamia maslahi ya umma zaidi kuliko maslahi binafsi. TMAA ndio jicho la umma. Kwa mazoea wamekuwa wakipima kimazoea na kuacha mali nyingi bila kutathiminiwa. Mbinu gani itumike? Kamati imependekeza kuwapo kwa timu isiyojulikana ya kufanya uchunguzi wa makinikia kwa kushitukiza kuhakiki walichokifanya TMAA.
Huwezi kunishawishi kuwaamini baadhi ya wasakatonge wa humu jf hasa huyo aliyenipa link yake na kuacha kumuamini katibu mkuu kongozi.
Mengine sijibu hasa ya huyo waziri umsemaye. Hana alichoharibu kama Nape. Tatizo ni kutokufanya kazi kama aliyewateua alivyotaka. Kutomridhisha rais si kosa iwapo kutokuridhika kwake ni kutokana na wewe kutekeleza majukumu yako kisheria.
 
Kama hatuna kumbukumbu za miaka ya hivi karibuni je tutaweza kujua aliyebuni jina la tanganyika!?
kunawatu hawataki kusikia kitu tanganyika
Nani Kachora Nembo ya Taifa: Mzee Farahani (Farhan), Ngosha, au Jeremiah Wisdom Kabati?

Kuna wanaosema Mzee Jeremiah Wisdom Kabati kachora nembo ya Taifa. Wengine wanasema Mzee Ngosha kachora. Kwa sasa mimi nipo upande wa Professor Elias Jengo anayesema nembo ilichorwa na Mzee Abdallah Farahani kutoka Zanzibar. Professor Jengo aliandika kwenye kitabu kwamba Mzee Farahani ndio aliyechora nembo ya Taifa. Inasemekana mtoto wa Mzee Farahani, Iddi Farahani alikuwa na sketches za baba yake za hii nembo. Mzee Farahani alisoma na Mwalimu Nyerere Makerere. Professor Elias Jengo kutoka Chuo Kikuu anaandika kwenye kitabu “East Africa Art Biennale” kwamba “As a designer, Abdallah Farahani will be remembered for his design of the national emblem. The emblem was recently criticized by a legislator for depicting barefooted human figures.” Ukurasa 44. Kaka Dominicus Makukula, msanii na mwalimu Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, anaamini kwamba Mzee Furahani ndio aliyechora ile nembo ya taifa. Anasema mjukuu wa Mzee Farahani yupo Music Academy Zanzibar na pengine anaweza kutoa majibu kama kuna atayeweza kwenda kuongea nae zaidi. Mpaka tutapopata habari zaidi, inaonenaka kwamba Mzee Farahani kutoka Zanzibar ndio aliyechora ile nembo. Tusubiri tuone kama serikali itafuta mavumbi na kufungua maboksi yenye nyaraka husika.

FACT NUMBER 2

Tukiangalia nembo hii ya Tanganyika 1961, ile ya Tanzania 1964 na ule mchoro usio na rangi uliopo katika nyaraka ya National Flag and Coat of Arms Act ya 1971, tunapata nafasi na sababu ya kudhani kuwa mchoraji na mbunifu halisi wa nembo ya Taifa si Ngosha wala marehemu mzee Jeremiah Kabati. Familia ya kabati inasema mzee alichora nembo hiyo mwaka 1960 na katika mahojiano na TBC Taifa, Ngosha alisema kuwa alisanifu nembo hiyo na mwenzake mwaka 1957. Prof. Jengo anathibitisha kuwa mchoro wa Farahani kwa ajili ya Tanganyika uliandaliwa mwaka 1961 na kuboreshwa 1964 wakati wa maandalizi ya nembo ya Jamhuri ya muungano. Swali la msingi, je yawezekanaje pasiwe na kumbukumbu hali miaka kumi baadae, marehemu Mwl. Nyerere alipatiwa mswada wa sheria ya nembo ya Taifa ileile ya mwaka 1961 pia 1964 (isiyonakshiwa kwa rangi) kwa ajili ya kuisaini ili iwe sheria kamili. Je walioandaa mswada walitoa wapi blue print ya nembo halisi mwaka 1971? Tatizo si kukosekana kwa nyaraka wala kumbukumbu, bali tatizo ni kukosekana watu wenye weledi kweye eneo la historia ya sanaa katika kuhifadhi amali hizi za Taifa katika mamlaka za kusimamia sanaa na utamaduni wa Taifa. mzee Mbughuni Sr. alifanya kazi kama Promoter of national arts miaka ya 1960s na hatimaye kuwa mkurugenzi wa idara ya sanaa miaka ya 1970s mwishoni, alianzisha Chuo cha Sanaa Bagamoyo mwaka 1981 baada ya kuvunja kikundi cha sanaa cha Taifa mwaka 1979 (Kelly Askew 2005:304-309), hawa ndio aina ya watu tuliowakosa katika miaka hii Tanzania...

Imechukuliwa kutoka bandiko la Azaria Mbughuni
May 26, 2017

Too bad serikali haina kumbumbu [emoji23]
 
Daa hili ni laajabu na aibu kabisa, nembo ni utambulisho wa Taifa hivi ni kweli hakuna taarifa ya aliye chora? Tunaitumia tu bila kujua Historia yake? Inakuwaje kila mtu anaibuka nakusema kuwa ndiye mchoraji? Ukweli Uko wapi?
 
It's a matter of time hata huyu Bashite kuna kipindi miaka ya mbeleni atakuja kutuambia kwamba wakati ni mkuu wa mkoa wa Dar es salaam alikua na elimu ya PHD.
 
tunasikitisha ila ni rahisi kwa mtanzania kukutajia listi nzima ya kikosi cha Arsenal mwaka 1995.
Hata serikali inatia aibu, kuna maktaba ya taifa, tuna makumbusho ya taifa, makavazi ya Mwl Nyerere, na taasisi kibao za utamaduni lkn hata waziri hajui yupi yupi kwenye hilo sakata.
 
Back
Top Bottom