Nani kaipa mamlaka Israel ya kuishambulia Syria?

Nani kaipa mamlaka Israel ya kuishambulia Syria?

Wewe mwenyewe hujui bibilia eti Yesu atarudi, bibilia yenu inakiri Yesu harudi. Bibilia zenu zilidai kuwa Yesu alisema atarudi ndani ya maisha ya Mitume yenu wa kwanza Paulo je karudi, na walimwamini kama wewe atarudi, Mitume wote walikufa na Yesu hakurudi tena. Kwa hiyo Ukristo unapaswa kukataliwa. Kuna sehemu nyingi ambazo Yesu alisema wanafunzi wake hawataonja kifo na wangekuwa bado hai wakati, Ujio wa Pili ungetokea. kunakingine zaidi ya hayo, wanafunzi waliamini, wakitumia maneno kama, basi sisi tulio hai, tuliobakia hata kuja kwa Bwana, vilevile Paulo aliwaonya waamini kwamba wasiolewe, kwa sababu Yesu alikuwa anarudi upesi.Hata katika Ufunuo, Yohana alidai kwamba alipata maono kutoka kwa Yesu akisema anakuja upesi.

Mitume wote walikufa bila kurudi tena. Miaka 2000 baadaye hakuna kurudi tena.bibilia yenu inakiri kwamba Yesu alisema uongo. We baki US atabaki Super power mpaa Yesu arudi, hizo ni ndoto za vichaa.
Ungeanzisha mada ya kidini kwenye uzi mwingine
 
Kaongea hayo kwenye Hadith ipi au Sura ipi ,tuweke hapa tuchambue

Ujue uzushi sio mzuri
Mimi sizushi huwa naongea daima ukweli, nimeisha kuwekea mpaa video na hadithi bado unasema nimzushi, hebu we nenda kwenye Google kafanye searching utakutana na hadithi sa we ni mbishi tu

Mimi kwanza ni mtu huwa namini Qur'an tu. Nyie wakristo ndio mnamini hadithi sa mbona hi mnajidai hamjawahi kuisikia 🤣
 
Kama kawaida yenu waislamu,mnayaparamia maandiko ya biblia bila kuyaelewa ,

Kwanza, imani ya kurejea kwa Yesu ni jambo muhimu katika Ukristo. Ingawa baadhi ya Wakristo wa awali walidhani kuwa Yesu angerejea wakati wa maisha yao, Biblia inasema kuwa wakati wa kurudi kwa Yesu unajulikana na Mungu pekee, na si wanadamu. Hii inathibitishwa na Mathayo 24:36, ambapo Yesu anasema, "Lakini kuhusu siku ile na saa ile, hakuna ajuaye, wala malaika wa mbinguni, bali Baba yangu pekee." Hii inaonyesha kuwa kurudi kwa Yesu hakupaswi kutabiriwa kwa usahihi. Aidha, katika Matendo 1:9-11, Yesu alipokuwa akipelekwa mbinguni, malaika walimwambia mitume, "Huyu Yesu atakayeondoka kwenu aende mbinguni, atakuja vivyo hivyo kama mlivyomuona aende mbinguni." Hii inaonyesha kurudi kwa Yesu katika siku zijazo, lakini hakutoa ratiba maalum.

Pili, maandiko ya Paulo kuhusu kurudi kwa Yesu yanaweza kuonyesha kwamba aliona kurudi kwake kuwa karibu, lakini hakusema kuwa itatokea ndani ya kipindi kifupi. Katika 1 Wathesalonike 4:16-17, Paulo anasema, "Kwa maana Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni kwa kelele, kwa sauti ya malaika mkuu, na kwa tarumbeta ya Mungu; na wafu waliomo Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tulio baki, tutachukuliwa pamoja nao katika mawingu, ili kumlaki Bwana angani." Hii inaonyesha kurudi kwa Yesu kama tukio la baadaye ambapo wafu na walio hai wataungana naye.

Tatu, kuhusu usemi wa Yesu kwamba "hii kizazi halitapita," tunapaswa kuelewa kuwa Yesu alikuwa akizungumza kuhusu matukio yanayohusiana na uharibifu wa Yerusalemu katika mwaka wa 70 BK, na si kurejea kwa Kristo mwenyewe. Hata hivyo, hii haifanyi ahadi ya kurudi kwa Yesu kuwa batili, kwani Mathayo 24:34 inasema, "Amin, nawaambia, kizazi hiki hakitapita hata mambo haya yote yatakapofanyika." Hii inaweza kumaanisha utimizo wa baadhi ya unabii wa karibu, lakini si kurudi kwa Kristo.

Mwisho, katika Ufunuo 22:7, Yohana anasema, "Tazama, ninakuja upesi." Hii inaweza kuonekana kama kurudi kwa Yesu, lakini neno "upesi" linapaswa kueleweka kwa mtindo wa wakati wa Mungu, ambao ni tofauti na mtindo wa binadamu. Kama ilivyoelezwa katika 2 Petro 3:8, "Lakini, wapendwa, msiwe na shaka kuhusu hili, kwamba kwa Bwana siku moja ni kama miaka elfu moja, na miaka elfu moja kama siku moja." Hii inaonyesha kuwa mtazamo wa Mungu kuhusu wakati ni tofauti na wetu, na kwa hivyo, muda mrefu unaonekana kwa wanadamu inaweza kuwa muda mfupi mbele ya Mungu.

Kwa hivyo, hata kama mitume wote walikufa bila Yesu kurejea, imani ya kurejea kwake bado ina msingi thabiti katika Maandiko, na tunapaswa kuendelea kumngojea kwa imani, huku tukijua kuwa muda wa Mungu ni tofauti na wetu.
Umeiweka kitaalamu sana.
Ila tu kujadiliana na hawa wenzetu wa bimdogo utapoteza muda tu.
Mtazamo wa kiroho na mtazamo wa kimwili ni kama maji na mafuta, nuru na giza, hamwezi elewana.
 
Umeiweka kitaalamu sana.
Ila tu kujadiliana na hawa wenzetu wa bimdogo utapoteza muda tu.
Mtazamo wa kiroho na mtazamo wa kimwili ni kama maji na mafuta, nuru na giza, hamwezi elewana.
Ni kweli Hawa jamaa hata vitabu vyao vinasema hawana elimu na mambo ya kiroho
 
Mimi sizushi huwa naongea daima ukweli, nimeisha kuwekea mpaa video na hadithi bado unasema nimzushi, hebu we nenda kwenye Google kafanye searching utakutana na hadithi sa we ni mbishi tu

Mimi kwanza ni mtu huwa namini Qur'an tu. Nyie wakristo ndio mnamini hadithi sa mbona hi mnajidai hamjawahi kuisikia 🤣
Hiyo Hadith unayotembea nayo haijataja Israel,ni mnabahatisha ndio maana hukutoa Aya Bali ulileta video ya kukokoteza
 
Hiyo Hadith unayotembea nayo haijataja Israel,ni mnabahatisha ndio maana hukutoa Aya Bali ulileta video ya kukokoteza
Wapi video ilisema Israel? We kichaa kweli video na hadithi zinaongelea Syria atashinda vita sababu ndio yatakuwa makao makuu ya Waislam. Usiwe unajibu kama kicha wewe ndio yule mtengenza majina mengi. Sichelewi kukunada mana akili ndio zile zile.

Mimi ndio nilisema Israel kwa sababu na yeye ni mmoja wapo, taifa lake lipo against Waislam.
 
Acha kupaniki ,sasa kama ulisema wewe ni Israel unachopaniki ni kipi?

Hiyo Hadith ni uongo,
 
Wapi video ilisema Israel? We kichaa kweli video na hadithi zinaongelea Syria atashinda vita sababu ndio yatakuwa makao makuu ya Waislam. Usiwe unajibu kama kicha wewe ndio yule mtengenza majina mengi. Sichelewi kukunada mana akili ndio zile zile.

Mimi ndio nilisema Israel kwa sababu na yeye ni mmoja wapo, taifa lake lipo against Waislam.

Adiossamigo: Wewe ni Shia nini? Makao Makuu ya Uislamu yatakua Syria!! Kwa hiyo mtaihamisha Kaaba kutoka Mecca! Saudia itaawacha kweli! Maana Mfalme wa Saudia ndio "Custodian of the two Holy Mosque" Mtaanzisha vita vingine tena!
 
Sisi Waislam tunaelewa kinacho kuja wacha Israel afike mpaa Damascus, na pia usisahau hata Firauni alikuwa ana kiburi kuliko huyo Shetanyahu. Mimi navyo ona ni tofouti na mkristo na myahudi. Syria itabaki kuwa makao makuu ya jeshi la kislamu. Israel siku zake zimekaribia kuwiva, wacha waendelee kuota na ile map yao Greater Israel 🤣
Hii mada ipo juu sana ya uwezo wako, acha kujadili kitoto toto unafikiri tupo chekechea hapa tunasimuliana adithi za uwongo na ukweli hapa😕😕
 
Adiossamigo: Wewe ni Shia nini? Makao Makuu ya Uislamu yatakua Syria!! Kwa hiyo mtaihamisha Kaaba kutoka Mecca! Saudia itaawacha kweli! Maana Mfalme wa Saudia ndio "Custodian of the two Holy Mosque" Mtaanzisha vita vingine tena!

View: https://youtube.com/shorts/60n9LCuInws?si=wcFMMy0aNF6V0p0a

View: https://youtube.com/shorts/9lfOQhlaRws?si=kzeuYFTaRB0LKlAd

Hawa mbona Sunni sikia wanasema nini.

Nani kakuambia Makkah na Al Madina vinahusika hapo, hapo ni makao makuu ya jeshi yatakuwa sio Sehemu ya dini.

Mimi si Shia, ni Ibadhi lakini kila Sheikh naheshimu mawazo yake awe Sunni au Shia.
 
Hii mada ipo juu sana ya uwezo wako, acha kujadili kitoto toto unafikiri tupo chekechea hapa tunasimuliana adithi za uwongo na ukweli hapa😕😕
Mimi ukifikia robo ya elimu yangu kwenye dini na elimu ya kawaida utakuwa na bahati sana.

View: https://youtube.com/shorts/zme9dC3Ayhg?si=tOKebUAKtr-w7aQB

Hawa masheikh wote kumbe wajinga kama mimi sio 😄 🤣

We wachana na hadithi za masheikh nenda kasome Bibilia je Israel itabaki, kama itabaki basi njoo unifundishe uislam. Sababu hata bibilia huijui utaufahamu uislam wewe.

Israel itaondoka tu na kama Israel itabaki basi ni history tu.

Mtu anaye jita Mtoto kida the great kushindana naye ni ujinga tu.
 
Kwa hiyo Kenya ikipata taarifa za kiitelejensia inayo haki ya kuja kushambulia Tanzania na kurusha mabomu sehemu mbalimbali ?

Na hizo taarifa za kiitelejensia zielezee hapa sote tuzisome
Hata wale magaidi wa kibiti imelazimika kuwafuata Msumbiji sio kusubiri mpaka waje tena wakati una taarifa za kiintelijensia kuhusu mipango yao kukuhusu, Israeli haiwezi tena kusubiri yaliyo wapata October 7 wanawekeza sana kuzuia na kukomesha
 
Kuna baadhi ya mambo yana shangaza dunia hii hasa hapo middle east.

Mfano mgogoro huu unao endelea Syria baada ya aliyekuwa Rais wa Syria Bashar al- Assad kupinduliwa na wanaoitwa waasi au magaidi wa HTS.

Jambo la kushangaza baada ya Assad kupinduliwa jeshi la Israel lilianzisha mara moja mashambulizi ya anga katika vituo mbalimbali vya kijeshi Syria pasipo kuwa na sababu yoyote.

Wanaoitwa waasi/magaidi hawaja husika kwa namna yoyote ile katika kuishambulia Israel bali katika kuundoa utawala wa Assad na kuweka utawala wao mpya hivyo huu ni mgogoro wa ndani kwa ndani Syria pasipo Israel kushambuliwa kwa hata na bomu wala risasi yoyote ila kinyume chake Israel yeye ndie ameishambulia kwa mabomu Syria toka kuangushwa utawala wa Assad.

Pamoja na hayo yote jeshi la Israel limejisogeza ndani zaidi katika eneo la Syria toka kupinduliwa kwa utawala wa Assad.

Haya mamlaka ya Israel kufanya yote haya pasipo hata kuchokozwa na utawala mpya kapata wapi na je, siku huu utawala mpya wa Syria ukianzisha mashambulizi dhidi ya Israel kwa lengo la kulipa kisasi ni nani atahesabika mwenye makosa?
Ni kama tu Russia ilivyofanya Ukraine, sababu ni kwamba jirani yako akiwa ni adui na ana silaha hatarishi kwako ni lazima unyang'anye kwanza hata kama hajakushambulia kama kumyang'anya iko ndani ya uwezo wako
 
Nani adui yao ?

Unamuitaje mtu adui yako ndio kwanza utawala mpya ? Haujarusha hata risasi moja katika mpaka wako ?
Kwan wewe YAS wamekusamehe madeni ya iliokua TIGO? au umehama nayo??
 
Israel haijaanza kushambulia Syria baada assad kupinduliwa ni kabla kitambo huko na haijawahi kuhitaji ruhusa ya mtu yoyote kushambulia, mashambulizi ya sasa hivi wameyatolea sababu kwa nini yanafanyika
Kwaiyo ukitoa sababu zako tu unaruhusiwa kushambulia nchi iliyo huru!? Kwann binadamu tunajitoa akili Kiasi hiki!!!? hivi leo Iran iamke itangaze tuna taarifa za kiitelijensia Saudi wanataka kutuvamia aanze kuporomosha mabomu Riyadh nani atakayemuelewa kama hakuangushiwa mabom na Nato yote!? Tuacheni ushabiki maandazi Israel ni taizo kubwa sana katika dunia hii anafanya anavyotaka na dunia imekaa kimya kabisa
 
Mkuu, mbona kimya na Turkey! Dunia inapagawa na Israel, Turkey amefanya hicho hicho...!

Israel and Turkey conduct airstrikes on Syria's military bases​

View: https://youtu.be/t76lQNh0AY8
 
Back
Top Bottom