Markmosh Ramadhani
New Member
- Jul 26, 2022
- 1
- 0
Dhamira yenye Matunda ya kheri huifanya dira iwe na muelekeo wenye matokeo chanya, naweza nisieleweke vizuri lakini wote tunakubariana kwamba panapokosekana amani pana kilomita nyingi ili kuufikia Upendo, umbali Kati ya amani na Upendo kati ya baba na mama waliotengana huweza kuwafanya wamama wanaolea watoto peke yao kuishinda imani ya watoto wao, kuonekana wao ndo Wema na wameonewa licha ya wakati mwingine wao kuwa kisababishi kikuu cha mambo kuwa yalivyo
Lazima tukubaliane nyakati tunazoishi tunaishi kwenye dunia ambayo imekuwa na ongezeko kubwa mno la wamama wanaolea watoto peke yao iyo haijatokea kwa Bahati mbaya, kutaka kuuondosha mfumo dume na usawa wanaoupambania mara zote ni moja ya chanzo kikuu cha ndoa na mahusiano yao kuvunjika, kujiona kila kitu wanajua na kutaka kuwa juu ya mwanaume hiki pia ni chanzo kingine nyeti chenye kutuletea wamama wanaolea peke yao
Lakini pia tabia za kutotulia na mwanaume mmoja huweza kuwafanya wanaume wengi kutokuwa na uhakika wa mimba au mtoto anapozaliwa, au mwanamke kumpa mtoto baba asiye halisi sababu tu ya baba halisi kuwa duni kiuchumi hii pia ni sababu nyingine inayochangia pakubwa, Bahati mbaya wanaume wengi wamekuwa wanakufa kijerumani yaani kufa na tai shingoni hata Kama alitendewa mabaya siri huwa wanabaki nazo wenyewe na hii imekuwa inachangia mzani kutoweza kubalansi ivyo kuonekana mama ndo alionewa, tunahitajika kwa pamoja kuwajibika, madawati ya jinsia hayahitajiki kupambania haki tu za wanawake vinginevyo "NANI KAMA MAMA" utaendelea kuwa mwiba mchungu kwa baba asiye na makosa.

Upvote
1