Nani kama Sugu?

Nani kama Sugu?

Bila Mange tungejuaje huyu jamaa CV yake alikuwa mlinzi wa wa BP? au O LEVEL AU FURAUNI?
chadema MNA MATATIZO thread zote tulizochangia zimefungwa basi bakini na hii yenu susu hatuchangii maana kuna sheria siku hizi zinawalinda ninyi wengine tutaumia
msitutafuti BUN km hamtaki kuingia kwa mange basi mmeshinda

We jamaa kweli ni mshamba kinoma,sugu katoa kitabu cha historia yake about 3yrs ago na kaeleza kila kila kitu halafu leo unasema bila mange usingejua km sugu kapitia life gumu,ni mabwege tu kama wewe ndio mnao muona mange bab kubwa kumbe na yeye poyoyo tu!
 
Mabishano hayana logic., yani kama wote mpo mna pampula kilabuni.
 
Pure recruitement ya Sugu ni Afande Sele, ila kama Balozi amekiri mwenyewe au Sugu amesema siwezi bisha maana kipindi kirefu kimepita na uzee unaanza kuninyemelea.

I respect that mkuu
I agree because almost 80% of wht u saying about this is true
Pure recruitment ya sug ni huyu afande
 
Kuna watu wamekuja kuchafua uzi, sio kila sehemu ni lazima tumalizie frustrations zetu za kimaisha. Tuwe positive sometimes kuaprishieti watu wengine ata kama atuwapendi.

Hapa nipo njiani natoka msibani kumsindikiza marehemu mzee mlingwa, babake na Mx. Nimejifunza mengi kuhusu maisha, maisha haya tunapita tu tutumie uhai wetu vizuri. Rip mzee mlingwa.
 
aisee umetisha sana nilikua nataka sana kuikumbuka hiyo mistari...kuna dada mmoja kipindi hicho alikua jirani na kwetu alidedi kwa lile gonjwa...dingi tuliyekua tunahisi ndiye aliemuua alikua akipita na gari yake kijiweni tunaanza kuimba hiyo chorus..

Hahahahaha nyie noma hahahah
 
Dah,
Hichi kichwa kweli hatari.
Nakumbuka vinega walikua wana tamasha lao pale chuo cha simu kijitonyama nyuma ya Chuo cha Ustawi. Dah jamaa alichana nyimbo zake yeye mwenyewe bila back-up ya mtu. Na alichana kuanzia verses mpaka korasi zote kachana mwenyewe na hakukwama kwama sauti wala kuishiwa pumzi.

Lile tamasha la ustawi wa jamii ni history nyingine aliyoiandika Sugu. Haijawai kutokea msanii wa ndani kukusanya nyomi kubwa kiasi kile tena wa Hip-hop huku akimshinda msanii wa kimataifa na wasanii wote wa Bongo fleva waliokuwa na show somewhere else.
 
Kuna watu wamekuja kuchafua uzi, sio kila sehemu ni lazima tumalizie frustrations zetu za kimaisha. Tuwe positive sometimes kuaprishieti watu wengine ata kama atuwapendi.

Hapa nipo njiani natoka msibani kumsindikiza marehemu mzee mlingwa, babake na Mx. Nimejifunza mengi kuhusu maisha, maisha haya tunapita tu tutumie uhai wetu vizuri. Rip mzee mlingwa.

Unataka kusema nini sasa?

Mi mwenyew nimeattend misba miwili leo.

Au ushaanza shusha vroba..!?
 
Hivi unanijuwa kama wewe ni falla? Hapa anajadiliwa Sugu msanii Legendary wa Bongo fleva na siyo Baba Faiza, wewe Pimbi huna cha kujadili hapa kipindi hicho ulikuwa upo huko kwenu mashambani au unanyonya, wewe nenda You turn kwa Mange na mashangingi wenzio ndio level yako.

Akiendelea baada ya ujumbe huu dole la Kati linamhusu.
 
Unataka kusema nini sasa?

Mi mwenyew nimeattend misba miwili leo.

Au ushaanza shusha vroba..!?

Nilitaka kujaribu kukumbushia maisha haya tunapita tu, tusichukie watu kiasi hicho mpaka unatumia siku nzima unatukana tuuu. Kuna watu naona wamechukulia siasa kila angle na ushabiki kila angle kiasi kwamba life inawatesa bila sababu ya msingi.

Kuhusu viroba, pombe niliacha rasmi mwaka 2014 mwanzoni sijawahi gusa tena na sitarajii. Mungu aniepushe!
 
Hayakuwa mapenzi ni the best hip hop love song of all time kwa hapa tz . Kwa mujibu wa mimi.

Mbona mnaisahau ile ngoma alofanya na Stara, yaitwa 'kiburi ' cjui jeuri?

Stara ana flow like ths:

'wanachotakaa , wanachotaka wewe upate taabu raha kidogo chuki bila sababuuu.'


kuna mistari mikali humo ndani inayonifanya nikomae ktk kazi.
 
Nilitaka kujaribu kukumbushia maisha haya tunapita tu, tusichukie watu kiasi hicho mpaka unatumia siku nzima unatukana tuuu. Kuna watu naona wamechukulia siasa kila angle na ushabiki kila angle kiasi kwamba life inawatesa bila sababu ya msingi.

Kuhusu viroba, pombe niliacha rasmi mwaka 2014 mwanzoni sijawahi gusa tena na sitarajii. Mungu aniepushe!

Nimekusoma. Amani itawale.
 
Hii inanikumnbusha mbali sana..!!

Enzi hizo gheto kumetapakaa magazeti ya wasanii mbalimbali kama kina 2pac Shakur, Westlife na B.I.G hapa Bongo ndo kina Sugu, Dola Soul wanasumbua balaa, Ukienda gheto na mtoto akute room lilmepambwa namna hiyo we ndo mjanja wa mjini. Mitoko ilikuwa ni Mashati ya drafti na tisheti nyeupe chini ukivalia suruali yenye mifuko pembeni usawa wa magoti almaarufu kama Timbarland yaani we utaogopwa mtaa mzima. Siku ukitoka na Visuruali flani hivi vinaitwa vinyelamumo, almaarufu kama Bigmark, pembeni unakiredio chako cha mkononi almaarufu kama Walkman, Yaani we unasumbua mji balaaa..!!

Enzi hizo kina Prof J ndo wanachipukia na Hard brothers crew yao, Sugu anasumbua Nchi na kitu chake "Anamiaka chini ya kumi na nane," kila Barbershop utakayoingia ni Sugu Sugu Sugu enzi hizo akijiita Mr II. Kina LadyJd ndo wananusanusa, pembeni hivi kina King Creiz GK wanasogea kwa mbaaaaali daaah...!!! Kweli tunatoka mbali sana.

Mr II alikuwaga na mpaka kesho anakisauti flani hivi cha ki-hip hop haswa.. Anakitetemeshi flani hivi wakati wa kutema mashairi. Yaani enzi hizo mziki ulikuwa ni hizi tunazoita leo zilipendwa na hip-hop kwa pembeni wakisindikizwa na Taarab kidogo. Na hiphop ilikua ni hiphop haswa, siyo kama leo wasanii wa hip-hop wanavisha pua zao vidani na kutoga masikio huku wakisindikizia na kusuka nywele na full make up..!!! Huu mziki ulikuwa wa wagumu kweli kweli.. Akaja jamaa mmoja hivi ambaye alishawishiwa na hawahawa kina Sugu kurudi kufanya mziki Bongo na si kung'ang'ania USA, huyu jamaa alikuwa akiitwa Cool James mtoto wa Dandu (Rip) ndiye mwasisi wa hizi tuzo za KTMA alitoa wazo la kuanzishwa kwa tuzo hizo (siyo KTMA) sijui aliziitaje. Bahati mbaya kabla hazijaanza rasmi akafa kwa Ajali.

Kipindi hicho mziki wa kunakili miziki ya wakongwe ilikuwa ikitamba haswa na style hii ndiyo iliyomtoa Mr Paul, aliimba wimbo wa Zuwena wa Mariajan Rajab. Hivi wakuu Matola, Deo Carlione na Ruttashobolwa mlikuwa wapi enzi hizo, Mnakumbuka nini?

Halafu kwa kumbukumbu zenu mnaweza kukumbuka mwanamziki wa kwanza kuanza mziki wa kuimbaimba (Siyo Kughani mashairi) almaarufu kama Bongofleva? Note, ninaposema Bongofleva R&B weka pembeni.. Tukumbushane wadau..

BACK TANGANYIKA

Hahahahahah umenikumbusha mbali sana mkuu, kipindi hicho matoz wananyoa panki za kina Shaba Ranks, Raba kubwa sana zakuitwa lakuchumpa unakuta ina tiki kubwa ya Nike.... Jeans za fubu, hapa unanoga ukipiga full jeans na koti lake... Ukionekana umebeba cd mkononi watoto wakali wote wako... Cd kipindi hicho uwe na ndugu kiwanja au ukaazime ushuani... Nakumbuka braza angu alikuwa anakanyaga mguu mpaka msasani kwa kina Roby kuazima tu cd za wakali wa mbele.
 
Last edited by a moderator:
Mbona mnaisahau ile ngoma alofanya na Stara, yaitwa 'kiburi ' cjui jeuri?

Stara ana flow like ths:

'wanachotakaa , wanachotaka wewe upate taabu raha kidogo chuki bila sababuuu.'


kuna mistari mikali humo ndani inayonifanya nikomae ktk kazi.

Ile inaitwa dawa ya jeuri kiburi.. Video yake kafanya na ndinga lake kipindi hiko alikuwa anauza nalo sana tu terano black hivi.
 
Back
Top Bottom