Nani kamtuma Zitto Kabwe kuomba Mbowe aachiwe huru?

Ni jambo la ajabu kabisa kudhani kuwa hata rais hakumwelewa Zitto!
 

..kila kitu ni muhimu hapa.

..siwezi kuita hoja na maoni yako non sense.

..Raisi anasema Zitto kamuombea Mbowe msamaha.

..Chadema nao wanalalamika Zitto kaomba msamaha.

..ina maana SSH na CDM siku hizi wako upande mmoja na waliopanga tukio hili dhidi ya Zitto?

..I wish Zitto angezungumza kwa namna ambayo isingeleta mkanganyiko kiasi hiki.
 
Sawa kabisa!
 
Yaani Chadema wameungana na Samia kuspin alichoongea Zitto.

Zitto kasema Mbowe aachiwe kwa mujibu wa sheria nyie mnasema eti kamuombea msamaha wakati. hakuna kitu kama hicho. Very unfortunate!
Imani ya Chadema ni kuwa yale yalikuwa maigizo. Wanaamini Zitto alipangiwa cha kusema na Mheshimiwa Rais alijipanga kujibu kile ambacho Zitto angesema. Hili walilizungumzia mapema sana.

Kwa mtazamo wao ni kuwa Zitto ilikuwa amuombee msamaha Mbowe lakini akabadilisha maneno baada ya Chadema kugoma kabisa kuhudhuria kikao. Lakini kwa vile alibadilisha maneno dakika ya mwisho, Mheshimiwa akajibu yale aliyokuwa aseme lakini hakusema. Hapo ndipo kwenye mtihani.

Hata ukiyaangalia maneno ya Zitto bila bias utaona yana mushkeli. Kuachiwa kwa mujibu wa sheria maana yake nini? Aachiwe kwa sababu sheria inasema aachiwe? Sheria ipi hiyo? Alishindwa nini kusema kuwa aachiwe kwa sababu hana hatia? Au aachiwe kwa sababu kesi haina mashiko? Hivi kama Mheshimiwa Rais angesema amemsamehe Mbowe kwa hiyo aachiwe, Zitto angemsahihisha na kumwambia yeye hakumwombea msamaha kwa hiyo kumuachia kwa msamaha ni makosa? Au angesema kuwa ni ombi lake la msamaha ndio limefanya aachiwe?

Naamini kwa dhati kuwa Zitto alikuwa na nia njema lakini ni huko kutaka kusema bila kusema ndio kunafanya wengine wamtilie mashaka.

Amandla...
 

..Na Zitto alionana na Rais na kum-brief kuhusu suala la Mbowe kabla ya mkutano wa Msajili wa vyama.
 
..Na Zitto alionana na Rais na kum-brief kuhusu suala la Mbowe kabla ya mkutano wa Msajili wa vyama.
Ndipo hapo panapoleta mkanganyiko. Alitaka kupiga chenga nyingi mno ndio maana akaharibu. Inaelekea anapanga statements zake ili awe na pakutokea kama mambo hayataenda anavyotaka.

Alisema Mbowe hakumkatalia alipozungumzia suala la msamaha implying kuwa Mbowe alimkubalia bila kusema kwa uwazi kwa sababu anajua hakupewa go ahead. Sasa tunaambiwa kuwa Mbowe alimsihi asiende Dodoma. Kama hizi taarifa ni za kweli, hamna jinsi Mbowe angemkubalia akamuombee msamaha halafu akamsihi asiende kwenye mkutano ambamo ndimo angeombea huo msamaha.

Kwa mawazo yangu Zitto angeishia tu kwenye statement alizozitoa mwanzo baada ya kulaumiwa, kuwa ni unfortunate choice of words lakini nia yake ilikuwa safi.

Amandla...
 

Wanawaita opportunists. Kama kina Muzorewa, Sithole, Buthelezi nk. Huyu kama wale na kwetu wapo ..!
 
Akimshambulia hayati magufuli, zitto anakuwa anaaminika..kinyume chake anaitwa kigeugeu.

Dhamira ya zitto ktk kauli ile ni kumuona mpinzani mwenzake anarudi uraiani na ku-resume shughuli zake za kisiasa na kiuchumi.

Yeriko nyerere anapaswa kufocus kwny dhamira ya zitto..na aheshimu hilo.

Huwezi kuitwa fala kwa kuomba radhi
 
Rais kasema, na Siyo Zitto aliyesema
Sasa badala mchukue kauli kutoka kwa Zitto mwenyewe, nyie mnachukua kauli kutoka kwa rais akiielezea kauli ya Zitto!

Show me wapi Zitto kasema kuwa Mbowe asamehewe.

Msilete spinning za Samia kuspin kauli ya Zitto halafu mkaichukua hiyo spin na kumlisha Zitto
 
Kwanini aachiliwe wakati ana kosa! Siyo tu kosa ...kosa la UGAIDI!
Vipi raisi aombe namuachia gaidi? Tunataka kesi tuendlee hadi mwisho tujue ugaidi wa mbowe ni upi na alifanyiwa wapi?
 
Ingewezekana OSAMA BIN LADEN kuomba radhi kwa rais wa USA? ama mm ndo sijui maana ya kumba msamaha? Kuungama??
Unawezaje kuungama kwa jambo usilolitenda???
 
Msamaha unakuwa msamaha tu pale kunapokuwa na KOSA LIMETENDEKA NA LIMETHIBITISHW KUTENDEKA KWA USHAIDI USIOTILIWA SHAKA.
Sasa huyu kibaraka wa CCM Bwana M-Zito Kabwe-la kapata wapi ujasiri wa kuomba msamaha kwa kosa ambalo halijathibitika popote? Huu ni uzuzu.
 
Kule twitter alinipiga block ya nguvu kisa na mchallenge kutokana na upupu wake usiofuata kufikiri kabla ya kuandika.
 

..but Zitto was not unequivocal in his remarks that the charges against mwenyekiti Mbowe were bogus and should be dropped.

..lugha aliyotumia Zitto ndiyo iliyotoa mwanya kwa Rais SSH kuanza kuzungumzia suala la msamaha.

..hoja yako ni nzuri, na ungekuwa mahakamani ungeshinda. Lakini hapa unazungumza na watu wa mtaani, sio wanasheria.

..katika macho [ body language ] na masikio [ verbal] ya mtu wa mtaani, Zitto ameomba msamaha.
 
Zitto hakutaka kujifanya militant mbele ya rais, kaongea maneno mazuri, ya hekima, tone nzuri.

Kama mlitaka amuite rais Dikteta, Mvunja katiba na amuamuru aache kuvunja katiba basi well hiyo tone hakuichagua Zitto siku hiyo, na Chadema kama wanaipenda sana hiyo tone ya ukaliukali basi wanayo chance in the future ya kulipuka mbele ya rais wakitaka.

Binafsi sioni tofauti ya tone ya Zitto mbele Samia na tone ya Mbowe mbele ya Magufuli kule CCM kirumba
 

..wapinzani hawapaswi kutia " SUKARI " machungu yao kwasababu wanazungumza mbele ya Rais.

..waseme UKWELI kuhusu dhuluma wanazofanyiwa na watawala.

..Rais anazungumza lugha ya " MAMA NA MWANA" mbele ya wapinzani kwasababu ni wao wenyewe wamejifanya wadogo, dhalili, na ombaomba, mbele yake.

..Siasa za wapinzani kuwa sawa na chekechea, na CCM kuwa wazazi, au watu wazima, sidhani kama zina manufaa kwa wapinzani.

Cc Nguruvi3, Fundi Mchundo
 
Mbona Zitto mwenyewe kakiri kuwa alimwombea Mbowe msamaha lkn hakutumwa na mtu, mwenye IQ ndogo ni nani sasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…