Nani kamtuma Zitto Kabwe kuomba Mbowe aachiwe huru?

Nani kamtuma Zitto Kabwe kuomba Mbowe aachiwe huru?

Zitto ana akili kawazidi upeo viongozi wengi wa Chadema. Zitto anajua power iko wapi na namna gani ya kuinyakua kidogokidogo. Viongozi wa Chadema wanadhani Mclyster atamtoa Mbowe Jela na kutupa tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. It doesnnt work that way

..unadhani wenye power hawajui hicho anachokifanya Zitto?
 
..unadhani wenye power hawajui hicho anachokifanya Zitto?
Sasa hao wenye power ni key players katika nchi hii kama ilivyo wapinzani. Kuna times inabidi ususe, kuna time inabidi uwaingage. at the end of the day hata ukigain kidogo, unakichukua kisha unaanza kudai tena.
All or Nothing strategy sometimes don't work
 
Mkuu Yericko Nyerere , kwanza hongera kwa andiko zuri, wewe ni mwandishi mzuri, una kipaji cha uandishi, tatizo lako ni dogo tuu, ambalo kwangu naliona kama ndio tatizo kuu la Chadema, kama mngelitatua saa hizi, siku nyingi Chadema ingekuwa Ikulu.

Tatizo lako wewe na wengi wenu mliopo Chadema ni kiwango fulani cha uelewa wa baadhi zinazohitaji kiwango fulani cha uelewa. Kwa kifupi uelewa wa wafuasi wengi wa Chadema ni uelewa fulani hivi, kama ilivyo baadhi ya wana CCM!, kumuelewa vizuri Zitto, kunahitaji kiwango fulani cha uelewa.

Umeandika bandiko hili refu refu lote kwa kushindwa kuelewa Zitto alisema nini!. Uelewa kama huu uelewa wako ndio uliotamalaki Chedema ndio mnakifanya Chadema kuendelea kuwa ni chama cha kiharakati badala ya chama tawala in waiting!.

Aliyezungumzia kusameheana kupo ni rais Mama Samia, usimlishe Zitto maneno!. Kama hukumwelewa Zitto, sema tukueleweshe!.

Ukipata nafasi, nunua gazeti la Nipashe la leo, nenda ukurasa wa 7, kuna kitu kinakuhusu.

Jumapili Njema.
P
Hujambo ndugu Paskali,

Bahati mbaya umechangia hoja hii huku ukiwa na majibu yako kabla ya kusoma kilichoandikwa na wala hujajishughulisha kuangalia video hizo tatu.

Kinachonisikitisha ni kuona mtu kama Paskali kujibu hoja kwa adabu mbovu kiasi hiki, Niwie radhi nashindwa kuchagua neno sahihi linalokufaa,

Kwamba Zitto hakumuombea msamaha Mbowe? Kwani umeharibikaje kiakili ndugu Paskali?I Ok, pengine ili ujue Zitto alimaanisha kuomba msamaha ni lazima umsikilize mpokeaji wa maombi ya Zitto ambae ni Mh Rais. Alichojibu rais ndicho alichomaanisha Zitto.

Mimi na ninyi akina Paskali mnaovizia huruma za watawala ili muishi nani ana IQ ndogo?
 
Yaani Chadema wameungana na Samia kuspin alichoongea Zitto.

Zitto kasema Mbowe aachiwe kwa mujibu wa sheria nyie mnasema eti kamuombea msamaha wakati. hakuna kitu kama hicho. Very unfortunate!
 
Hakuna mahali Zitto kamuombea Mbowe msamaha, acheni kuspin na kumlisha maneno.

Zitto ana hekima, kawazidi upeo viongozi wengi wa Chadema. Zitto anajua power iko wapi na namna gani ya kuinyakua kidogokidogo. Viongozi wa Chadema wanadhani Mclyster atamtoa Mbowe Jela na kutupatia tume huru ya uchaguzi na katiba mpya. It doesnnt work that way. Huwezi kusimama mbele ya raisi na kuvimba na kuleta uanaharakati uchwara, ukifanya hivyo rais anaweza kuamua kutunisha msuli wake, mtamfanya nini?
Kinachotakiwa ni many fronts one battle.
Tatizo la viongozi wa Chadema wana chuki kali sana kwa Zitto, ndiyo maana hata alivyokufa mama yake walijivutavuta kwenda kuhani msiba wakati marehemu alikuwa ni. mjumbe wa kamati kuu wa chama chao wenyewe!
Huu ndio ukweli
 
Yaani Chadema wameungana na Samia kuspin alichoongea Zitto.

Zitto kasema Mbowe aachiwe kwa mujibu wa sheria nyie mnasema eti kamuombea msamaha wakati. hakuna kitu kama hicho. Very unfortunate!

..uwasilishaji wa Zitto ulikuwa na walakini.

..Zitto hakuweka msisitizo usio na shaka kwamba Mbowe kabambikiwa kesi.

..uelewa wa SSH nao una walakini.

..hata kama SSH ameamua ku-spin, ni kauli, na uwasilishaji wa Zitto, ndio umemuwezesha ku-spin.
 
Yaani Chadema wameungana na Samia kuspin alichoongea Zitto.

Zitto kasema Mbowe aachiwe kwa mujibu wa sheria nyie mnasema eti kamuombea msamaha wakati. hakuna kitu kama hicho. Very unfortunate!
Kwamba Zitto hakumuombea msamaha Mbowe? Kwakukusaidia katika upembuzi yakinifu wa hoja, Ili ujue Zitto alimaanisha kuomba msamaha ni lazima umsikilize mpokeaji wa maombi ambae ni Rais Rais. Alichojibu rais ndicho alichomaanisha Zitto.

Mbona logic ndogo sana hii lakini mnaikwepa? Components ya hoja inaanza kwa Zitto ina malizika kwa Rais. Huwezi kusikiliza nusu kisha ukasema umeelewa. Ndio sababu nimekuwekeeni video zote hapo.
 
..uwasilishaji wa Zitto ulikuwa na walakini.

..Zitto hakuweka msisitizo usio na shaka kwamba Mbowe kabambikiwa kesi.

..uelewa wa SSH nao una walakini.

..hata kama SSH ameamua ku-spin, ni kauli, na uwasilishaji wa Zitto, ndio umemuwezesha ku-spin.
Sasa kama tumeanza kuargue juu uwasilishaji wa hotuba badala ya hotuba yenyewe ina nini ndani yake, maana yake ni kuwa sasa tunaanza kuargue "fani" badala ya "maudhui", kitu ambacho nakiona ni nonsese. Kila mtu ana style yake ya kudeliver speech, cha msingi message ifike!.
 
Kwamba Zitto hakumuombea msamaha Mbowe? Kwakukusaidia katika upembuzi yakinifu wa hoja, Ili ujue Zitto alimaanisha kuomba msamaha ni lazima umsikilize mpokeaji wa maombi ambae ni Rais Rais. Alichojibu rais ndicho alichomaanisha Zitto.

Mbona logic ndogo sana hii lakini mnaikwepa? Components ya hoja inaanza kwa Zitto ina malizika kwa Rais. Huwezi kusikiliza nusu kisha ukasema umeelewa. Ndio sababu nimekuwekeeni video zote hapo.
Wewe ulivyoelewa unadhani Zitto kamuombea msamaha Mbowe, Sisi tulivyoelewa ni kuwa Zitto anataka Mbowe atoke kwa mujibu wa sheria maana ile kesi ni ya kubumba.
 
Hatua yoyote itakayochukuliwa kwamsingi wa kauli ya Zitto mbele ya Rais haina tafsiri nyingine isipokuwa ni Mbowe amekiri makosa ya kubambikiwa ugaidi na hivyo kuununua uhuru wake. Jambo hili mimi sikubaliani nalo, Mh Mbowe hakubaliani nalo, Chadema haikubaliani nalo na yeyote mwenye akili timamu hakubaliani nalo.

Maridhiano katika siasa ni jambo muhimu na ni tunu kwa Taifa na Chadema tumeyatafuta maridhiano na tunaendelea kuyatafuta kwa kadiri tuwezavyo, Lakini Mbowe kuwa mahabusu ama kuachiwa sio maridhiano, tunataka Mbowe aachiwe huru bila masharti ndipo maridhiano ya kitaifa yakalike mezani pande mbili ziweke mezani mahitaji yao kwa nchi, na Upande wa Mbowe jambo letu kuu ni Katiba Mpya tu.

Mh Mbowe hana hatia, Familia, Chadema, Mimi na wengine wote tunafahamu Mbowe hana hatia, amebambikiwa kesi kwasababu tu anadai Katiba Mpya. Na msimamo wa sisi wote ni kuwa kesi ifutwe bila masharti yoyote, na wakikataa kufuta kesi iende hadi mwisho wamfunge Mbowe kwa namna wanavyoona inawafaa lakini sharti la teknlojia ambalo hawezi kulizuia, ni kwamba watamfunga hadharani sio gizani, watake ama wasitake dunia itatazama kwa macho na itasikia kwa masikio.

Kuomba msamaha sio chagua la Mh Mbowe wala sio chaguo letu, Kitendo hiki cha kuipigia magoti serikali kinachoshinikizwa na madalali wa watu wale wale waliomfanyia madhira kingefanywa hata tangu mwanzo enzi za utawala wa Magufuli uliomfanyia madhira ambayo hayaelezeki kabisa mbele ya umma, lakini pia angeomba msamaha huo kabla hata hajakamatwa na kufikishwa mahakamani na utawala rais Samia kama angeamua kuwasaliti Watanzania wasidai Katiba Mpya.

Na tunafahamu kuomba msamaha ni kukiri kosa na msamaha kwa asili huambatana na masharti ambayo yataendelea kumfunga Mbowe akiwa uraiani na kwamba akiyavunja atawajibika nayo. Si kwamba ushauri wa kumtaka Mbowe akiri na kukubaliana na watesi hatukuupata mapema, Madalali wa jambo hili wameanza muda mrefu na wamemfikia kila wanayeona atafanikisha hili. Hiki kitendo tulikikataa tangu awali. Mtindo wa kununua uhuru tumeukataa. Waliposhindwa kwetu wameamua kumtumia Zitto kwamgongo wa TCD, nae kwakujua wazi anahujumu juhudi za kupata Katiba Mpya ameingia king na kujipua.

Approach za kisiasa zinazofanywa na chama chetu kama taasisi kuwakabidhi file la kesi (Comito) wadau wa kisiasa TCD na wajumbe wake akiwemo Mzee Mbangula ambae ametajwa na Zitto katika utetezi wake tulipomhoji kwanini anamdhalilisha Mh Mbowe, Zitto akijibu hoja hii amesema aulizwe Katibu Mkuu kwanini alipeleka nyaraka za kesi kwa Mzee Mangula? Ukweli ni kwamba Zitto amepotosha kusudi la nyaraka za Comito kufika kwa TCD (Mangula).

Nyaraka hazikuwa na maana ya "kuomba msamaha" kama Zitto alivyoamua kupotosha umma mbele ya Rais, Approach ya Chadema mbele ya Wajumbe wa TCD ilikuja baada ya kuwaambia wajumbe wa TCD kwamba hawatahudhuria mkutano kwasababu hoja ya tangu awali kwamba Mbowe aachiwe bila masharti haijatimizwa, ndipo mmoja ya wajumbe (Mzee Mangula) akaomba kufahamishwa juu ya kesi hii kiundani, Chadema ikachukua jukumu la kitaasisi na kuwapatia wajumbe wote nyaraka za Comito akiwemo Zitto mwenyewe ambae ni mwenyekiti wa TCD, lengo lilikuwa wadau wa siasa wote wajue kwaundani (in details) kuwa kesi hii ni ya kubambikizwa haina mashiko ya kisheria bali ni siasa.

Zitto anajua vema hili na alijua tangu mwanzo, alichoamua ni kwenda kufanya kile ambacho tulishakitakataa tangu mwanzo kabisa kabla Mbowe hajakamatwa. Yaani ameamua kukiharibia chama chetu na kumharibia Mbowe atafsirike ni gaidi aliyeomba msamaha kwa Rais na rais amemsamehe. Naamini Mbowe kaumia sana na kakasirika sana kwa hili.

Huku ni kumdhalilisha na kutweza utu na msimamo wa Mh Mbowe, huku ni kuidhalilisha Chadema na vyama rafiki vinavyounga msimamo wa Mh Mbowe (NCCR MAGEUZI). Zitto ameamua kushirikiana na dola kumlazimisha Mbowe awe na hatia na ajutie. Mbowe hajamtuma wala chama hakijamtuma. Ninachoamini ametumia mwanya huu wa mvutano kati ya dola na Mbowe, Wakati serikali ikipambana kujinasua kwenye kesi ambayo wao ndio waliifungua na sasa dunia imewakalia vibaya, upande wa pili Mbowe ameweka msimamo wa kutopiga magoti, Zitto amejichomeka na kumsemea Mbowe bila kutumwa.

Naamini msimamo wa Mbowe na Chadema uko pale pale kwamba kesi ifutwe, na sio ifutwe kwa neno msamaha wa Rais ambao kimantiki alishaweka masharti pale aliposema Mbowe "afuate sheria" kauli inayohalalisha kwamba Mbowe ni mkosaji na sio mtuhumiwa tena kama sheria za nchi zinavyosema kwamba mtu hatahesabika kuwa na hatia hadi pale Mahakama itakapotamka. Je ni sheria ipi ambayo Mbowe amevunja hadi akawa mahabusu? Kudai Katiba Mpya ni kuvunja sheria? Kudai haki za kisiasa zilizozuiwa kinyume cha katika na sheria ni kuvunja sheria?. Lipi kosa la Mbowe hadi aombe msamaha?.

Kwa minajiri hiyo, Zitto kuomuombea msamaha Mbowe ni kumtia hatiani mbowe bila kosa, Zitto ameshirikiana na dola kuhalalisha kesi ya kubumba ya ugaidi dhidi ya Mbowe na dola imefanikiwa kumtumia Zitto kwa hili mbele ya watu wachache, lakini tumuulize Zitto, Je Msimamo wa Mbowe ni kukiri kosa ambalo hajatenda? Mbowe amefilisiwa biashara zake zote Tanzania na kubaki sifuri kabisa hadi miamala ya simu ikafungwa ili asipokee hata pesa ya vocha tu toka kwa wajukuu zake yaani M-pesa, Airtel Money na TIGOPESA na Utawala wa Magufuli, Utawala huo ulimvunjia club Bilicanas, ukamfungia Account zake zote za Benki na kupora mabilioni ya amana zake zote katika account hizo. Ukaharibu Mashamba yake na Biashara zake za mahoteli nk, Ukamvunja Miguu, Ukavuruga Uchaguzi jimboni kwake Hai kwakumtumia Jambazi Ole Sabaya aliyeteka, kuumiza na kutia vilema wanachama wenzake, Mbowe hakupiga magoti kamwe. Sasa utawala wa Rais Samia umempa kesi ya Ugaidi. Kisha Mnamuambia aombe msamaha! MSAMAHA?
Mbowe huyuyu ambae utawala wa hayati Magufuli umemdhuru kwa viwango vyote na hakupiga magoti aje apige magoti kwakuwekwa mahabusu au kwakufungwa?

Tukatae aina hii ya manunuzi ya uhuru wetu. Haki itendeke, kesi ifutwe bila masharti yoyote, na wakikataa kufuta, basi wamfunge vile watakavyo lakini watambue watamfunga kweupe huku dunia inaona, kazi yetu itakuwa kuzuia wasimfunge gizani tu.

Na Yericko Nyerere

View attachment 2048448

View attachment 2048449
Mbowe ni shujaa

Tutamtoa_Mkoloni_Mweusi_Soon_on_Instagram%3A_%E2%80%9CMwenyekiti_wa_Chadema_Taifa_akisalimiana...jpg
FB_IMG_1589397986327.jpg
 
Kwamba Zitto hakumuombea msamaha Mbowe? Kwakukusaidia katika upembuzi yakinifu wa hoja, Ili ujue Zitto alimaanisha kuomba msamaha ni lazima umsikilize mpokeaji wa maombi ambae ni Rais Rais. Alichojibu rais ndicho alichomaanisha Zitto.

Mbona logic ndogo sana hii lakini mnaikwepa? Components ya hoja inaanza kwa Zitto ina malizika kwa Rais. Huwezi kusikiliza nusu kisha ukasema umeelewa. Ndio sababu nimekuwekeeni video zote hapo.

una chuki kwa zitto, na unaifanya iwe kubwa kisa unajikomba kwa Lema, Lissu na Mbowe

SO FAR, sidhani kama washahi kukusaidia kitu

ACHA KUDHANIA!!! kasema rais atumie njia za kisheria zote, kufanikisha kengo

Hivi hao huko nje mabalozi na mataifa wanayosema mbowe aachiwe, kwa sheria gani? mbona haujawahi kuwashukia??

wanafiki sana nyie
 
Kesi iko mahakamani, option ni mbili tu, kufuta bila masharti yoyote, au kuacha iende hadi mwisho. Nje ha hapo ujinga wote hautapokelewa....
 
Hivi unadhani Mbowe akifariki dunia tatizo litakuwa la Chadema? Unadhani watu wataamini kuwa amefariki kwa sababu tu wakati wake umefika?
Makaburu wa Afrika Kusini walifika mahali walifanya kila mbinu ili Mandela atoke jela kwa kuhofia watakavyohukumiwa kama angefia mikononi mwao.
Kwenye hili mzigo uko zaidi kwa wanaomshikilia kuliko chama chake.

Amandla...

So,unataka kusema kitu gan kwa mfano,

Mbowe akirud uraian km kawaida na kuendelea na maisha yake,kikimkuta kifo lawama utazipa SERIKALI?hata kama akifa kwa malaria??yeye ni mwanadam kufa ni lazima,sasa chadema bila mbowe mmeweka succession plan ya aina Gani?? answer that question comrade,mbona swali rahis tuh,ukijibu please note that electronic calculators are not allowed in examination room,and this question is compulsory,you may use four figure if you want, please observe time n punctuality....
 
Kesi iko mahakamani, option ni mbili tu, kufuta bila masharti yoyote, au kuacha iende hadi mwisho. Nje ha hapo ujinga wote hautapokelewa....

Huo ndiyo ukilaza sasa anaousema mayala,

Masharti hayo ya kumpa mtawala eti afute case bila masharti yyte Tena case ambayo Iko mahakamani yanaingia akilin?ile ni mihimili tofaut ya Dola,unataka aingilie Ili ionekane anaingilia uhuru wa mahakaman??mmeshapeleka kina kibatala Wacha battle iendelee
 
So,unataka kusema kitu gan kwa mfano,

Mbowe akirud uraian km kawaida na kuendelea na maisha yake,kikimkuta kifo lawama utazipa SERIKALI?hata kama akifa kwa malaria??yeye ni mwanadam kufa ni lazima,sasa chadema bila mbowe mmeweka succession plan ya aina Gani?? answer that question comrade,mbona swali rahis tuh,ukijibu please note that electronic calculators are not allowed in examination room,and this question is compulsory,you may use four figure if you want, please observe time n punctuality....
Sijibu maswali ya kijinga. Na sipendi kulazimishwa kitu chochote. Hasa na watu wasiojua kiingereza lakini wanakilazimisha.

Amandla...
 
Back
Top Bottom