Nani kamtuma Zitto Kabwe kuomba Mbowe aachiwe huru?

Nani kamtuma Zitto Kabwe kuomba Mbowe aachiwe huru?

Sikutegemea umri Kama wako ungetumia maneno makali Kama hayo...Ulichosahau Ni kuwa wewe Ni mgombea ubunge wa Cha mapinduzi aliyepata kura moja na sio mwandishi wa habari...

Note:Mimi sio mfuasi wa mwanasiasa yoyote.

..hiyo ni mbinu tu ya kumtoa Yerricko kwenye reli.

..ukiona hivyo ujue jamaa kashindwa kujibu hoja anataka watu waanze kutukanana.
 
Jela si pazuri na anaye umia ni mbowe na familia yake. Mbowe atoke jela kwa njia yoyote ile, kisha aendelee na siasa akiwa nje.

Ushabiki wa kijinga wakati mtu anaumia jela si mzuri wala si ubinadam.
 
Mkuu Yericko Nyerere , kwanza hongera kwa andiko zuri, wewe ni mwandishi mzuri, una kipaji cha uandishi, tatizo lako ni dogo tuu, ambalo kwangu naliona kama ndio tatizo kuu la Chadema, kama mngelitatua saa hizi, siku nyingi Chadema ingekuwa Ikulu.

Tatizo lako wewe na wengi wenu ni low IQ, kwa kifupi Chadema ina vilaza sana!. Umeandika bandiko hili refu refu lote kwa ukilaza tuu wa low IQ kushindwa kuona Zitto alisema nini!. Vilaza kama wewe mliotamalaki Chedema ndio mnakifanya Chadema kuendelea kuwa ni chama cha kiharakati badala ya chama tawala in waiting!.

Aliyezungumzia kusameheana kupo ni rais Mama Samia, usimlishe Zitto maneno!. Kama hukumwelewa Zitto, sema tukueleweshe!.

Ukipata nafasi, nunua gazeti la Nipashe la leo, nenda ukurasa wa 7, kuna kitu kinakuhusu.

Jumapili Njema.
P
Kweli unaona ni bora kuwa chama tawala in waiting kuliko chama cha kiharakati kinachopambana kuingia madarakani! Unadhani kuna kurithiana katika utawala. Halafu sio fair kusema Chadema kimejaa vilaza wenye low IQ. Mbona kwenye chama tawala wako wengi tu? Utawaita geniuses watu ambao wanapitisha sheria na maazimio bila kujua ndani kuna nini? Maneno uliyotumia ni fighting words na usishangae watu wakikujibu hivyo hivyo. Hayakuwa maneno ya mtu mwenye high IQ hata kidogo.

Amandla...
 
Jela si pazuri na anaye umia ni mbowe na familia yake. Mbowe atoke jela kwa njia yoyote ile, kisha aendelee na siasa akiwa nje.

Ushabiki wa kijinga wakati mtu anaumia jela si mzuri wala si ubinadam.
Kama hamkutaka aumie jela si msingemfungulia mashitaka?
Nape alionekana mtu mwenye msimamo aliposimamia suala la Clouds. Lakini hilo lilifutika pale alipoenda kuomba msamaha na kuchukulia video akijifuta jasho akielekea Ikulu.
Mbowe akiomba msamaha atafanyiwa hivyo hivyo. Atatakiwa aende Ikulu au hata kwa Shaka na aimbe pongezi kwa wema ambao serikali imemuonyesha. Akifanya hivyo atakuwa kama wakina Halima ambao walikubali kupiga picha ya pamoja na Spika baada ya uapisho feki. Hataweza ku recover kutoka hiyo humiliation. Muache akae na kama ataachiwa, atoke akiwa amesimama sio akiwa anatambaa.

Amandla...
 
Kweli unaona ni bora kuwa chama tawala in waiting kuliko chama cha kiharakati kinachopambana kuingia madarakani! Unadhani kuna kurithiana katika utawala. Halafu sio fair kusema Chadema kimejaa vilaza wenye low IQ. Mbona kwenye chama tawala wako wengi tu? Utawaita geniuses watu ambao wanapitisha sheria na maazimio bila kujua ndani kuna nini? Maneno uliyotumia ni fighting words na usishangae watu wakikujibu hivyo hivyo. Hayakuwa maneno ya mtu mwenye high IQ hata kidogo.

Amandla...
Kwa vile CCM imejaa vilaza inahalalisha Chadema kuwa na vilaza pia? I thought nyie ni bora kuliko wao? Lakini pengine upo sahihi, kwa sababu silaha kubwa ya CCM mtandaoni ni matusi na lugha zisizo za kistaarabu, na bila shaka nanyi mmeona "kama CCM wanatumia matusi mtandaoni, why not sie pia"?
 
Kama hamkutaka aumie jela si msingemfungulia mashitaka?
Nape alionekana mtu mwenye msimamo aliposimamia suala la Clouds. Lakini hilo lilifutika pale alipoenda kuomba msamaha na kuchukulia video akijifuta jasho akielekea Ikulu.
Mbowe akiomba msamaha atafanyiwa hivyo hivyo. Atatakiwa aende Ikulu au hata kwa Shaka na aimbe pongezi kwa wema ambao serikali imemuonyesha. Akifanya hivyo atakuwa kama wakina Halima ambao walikubali kupiga picha ya pamoja na Spika baada ya uapisho feki. Hataweza ku recover kutoka hiyo humiliation. Muache akae na kama ataachiwa, atoke akiwa amesimama sio akiwa anatambaa.

Amandla...
hujui jela. kuna mda unaomba ukuta zivunjike ili utoke.
Ingekuwa ni wewe au baba yako ndiyo wapo jela usinge sema hayo maneno.

Hata mbowe mwenyewe hapendi kukaa jela, ndiyo maana alilipaga faini kwenye kesi ya uongo.
 
Mkuu Yericko Nyerere , kwanza hongera kwa andiko zuri, wewe ni mwandishi mzuri, una kipaji cha uandishi, tatizo lako ni dogo tuu, ambalo kwangu naliona kama ndio tatizo kuu la Chadema, kama mngelitatua saa hizi, siku nyingi Chadema ingekuwa Ikulu.

Tatizo lako wewe na wengi wenu mliopo Chadema ni kiwango fulani cha uelewa wa baadhi zinazohitaji kiwango fulani cha uelewa. Kwa kifupi uelewa wa wafuasi wengi wa Chadema ni uelewa fulani hivi, kama ilivyo baadhi ya wana CCM!, kumuelewa vizuri Zitto, kunahitaji kiwango fulani cha uelewa.

Umeandika bandiko hili refu refu lote kwa kushindwa kuelewa Zitto alisema nini!. Uelewa kama huu uelewa wako ndio uliotamalaki Chedema ndio mnakifanya Chadema kuendelea kuwa ni chama cha kiharakati badala ya chama tawala in waiting!.

Aliyezungumzia kusameheana kupo ni rais Mama Samia, usimlishe Zitto maneno!. Kama hukumwelewa Zitto, sema tukueleweshe!.

Ukipata nafasi, nunua gazeti la Nipashe la leo, nenda ukurasa wa 7, kuna kitu kinakuhusu.

Jumapili Njema.
P
Pascal nasikitika kukuambia kuwa hata wewe uelewa wako ni wa chini mno.
Hua nashindwa kukuelewa unashindwaje kuielewa CCM jinsi inavyowatendea wapinzani kinyume kabisa na matakwa ya katiba na wewe unakaa kimya tu.
Unateteta vitu ambavyo havistahili kutetewa na mtu mwenye heshima katika jamii.
Pascal wewe sio smart kabisa kama ambavyo unajiona.
Kama ungekua smart wewe usingepata kura Moja ndani ya chama Chako.
Nakuambia hivi,ungeweza kugombea kupitia Chadema nakuhakikishia leo hii ungekua ni Mbunge uliechaguliwa na wananchi lakini ambae hukutangazwa na Tume.yaani ungeshinda.
Kwa hiyo kwa uelewa wako finyu ulitegemea ungepitishwa tu na CCM Basi ungeshinda kwa nguvu za tume.
Hauko smart bro.
 
Case yake Iko mahakamani,na chadema kama chama kimepeleka mawakili,ila let say mbowe akikutwa na hatia na kufungwa,au hata akifarik Dunia,je succession plan ya chadema ikoje??
 
Nadhani hiyo ni move imetengenezwa!"Jifanye unamuombea Msamaha kwangu nimsamehe isije kuonekana ni lile shinikizo la Mabeberu"ndiyo limefanya nimwachie.
Huenda lile shinikizo la Mabeberu(EU) halijamfanya Mama atulie.
Zitto ndiye main player of the move.
 
..hiyo ni mbinu tu ya kumtoa Yerricko kwenye reli.

..ukiona hivyo ujue jamaa kashindwa kujibu hoja anataka watu waanze kutukanana.
Pascal Ni mfuasi wa CCM anaetaka atengeneze katiba ya Chadema..Kuna muda anapenda Sana achangie nyuzi Kama mwanahabari huku akisahau kuwa yeye Ni kada mgombea ubunge CCM aliyepata kura 1...Kumuita mwenzake kilaza Ni Utovu wa nidhamu wa Mtu mzima...
 
..unatakiwa kuwapuuza watu wa aina hiyo.

..mtu akikutukana unapaswa kutambua kwamba umemshinda kwa hoja.

..lengo lake ni uache kujenga hoja uanze kujibizana naye kwa matusi.
 
Mpaka sasa Freeman hana hatia au makosa hadi itakapothibitika vinginevyo mahakamani. Hata huko kuachiwa huru ni pale itakapothibitika kuwa hana hatia kwa mujibu wa sheria na mwenendo wa mashauri yaliyoko mahakani.

Msamaha anaomba au anaombewa mkosaji, Freeman haba kosa lolote kwa sasa! Hapo ndipo Zitto alipaswa kusubiri au kukaa kimya kuliko kumwombea msamaha mtu asiye na kosa au hatia. Ni kama vile anamhukumu kabla ya kuhukumiwa kisheria!
Huenda Zitto ana uhakika kwamba Rais anaweza kutumia ushawishi wake hii kesi ikafutwa na Mbowe kuachiwa huru.
 
Kwa vile CCM imejaa vilaza inahalalisha Chadema kuwa na vilaza pia? I thought nyie ni bora kuliko wao? Lakini pengine upo sahihi, kwa sababu silaha kubwa ya CCM mtandaoni ni matusi na lugha zisizo za kistaarabu, na bila shaka nanyi mmeona "kama CCM wanatumia matusi mtandaoni, why not sie pia"?
Na nyie mkagundua kuwa matusi hayafai mlipoanza kutukanwa? Kwa nini mnaanza kulalamika pale tu mtu ambae amekuwa victim kwa muda mrefu anapoamua kujibu mapigo? Chadema wametishiwa mpaka kuuawa publicly lakini wote kimyaaa! Labda Chadema wamehesabu mpaka 490 ( 7 x70) wakaona u Mahatma hauna tija. Pamoja na hayo bado sijawasikia wakisema watamuua mtu kwa sindano, au wakiomba viongozi wao wawape kibali cha kuwaua wapinzani wao. Kuwalinganisha na wapinzani wao sio kuwatendea haki.

Amandla....
 
Nanyi mlitumwa na nani kuomba maridhiano na Magufuli, Desemba 9, 2021? [emoji849] View attachment 2049768

Sasa kuna kosa gani hapo watu kuomba maridhiano? Hapa kulikuwa na kosa gani? Mbowe anatakiwa kuachiwa huru sio kusamehewa kama Samia anaona anayo misamaha mingi basi akamsamehe jambazi Sabaya ambaye alishakutwa na hatia!

Yani mtu umemuitabgaidi na umeshatoa hukumu bado unaleta maigizo? Mbowe kamwe asikubali kuomba msamaha yeye sio gaidi!
 
hujui jela. kuna mda unaomba ukuta zivunjike ili utoke.
Ingekuwa ni wewe au baba yako ndiyo wapo jela usinge sema hayo maneno.

Hata mbowe mwenyewe hapendi kukaa jela, ndiyo maana alilipaga faini kwenye kesi ya uongo.
Hakuna mtu anapenda kukaa mahabusu. Angekuwa baba yangu yuko ndani na kaweka wazi msimamo wake nisingeupinga.
Mbowe alikuwa wa mwisho kutoka jela katika wale waliokipiwa faini. Na sasa hivi amesema wazi kuwa yuko tayari kubaki jela kuliko kuomba msamaha. Wewe ni nani kumpinga yeye, familia yake na chama chake?

Amandla...
 
Rais anaweza kuamuru Mbowe aachiwe (kumtumia Dpp maana ni mteule wake) hivyo Zitto hakukosea kuomba hivyo.
 
Back
Top Bottom