Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,601
- 34,760
Mkuu hili jambo lina mengi ndani yake na naomba niyapitie kwa mtazamo wangu baada ya kusikiliza Chadema na Zitto katika 'space' moja..wapinzani hawapaswi kutia " SUKARI " machungu yao kwasababu wanazungumza mbele ya Rais.
..waseme UKWELI kuhusu dhuluma wanazofanyiwa na watawala.
..Rais anazungumza lugha ya " MAMA NA MWANA" mbele ya wapinzani kwasababu ni wao wenyewe wamejifanya wadogo, dhalili, na ombaomba, mbele yake.
..Siasa za wapinzani kuwa sawa na chekechea, na CCM kuwa wazazi, au watu wazima, sidhani kama zina manufaa kwa wapinzani.
Zitto
1. Hakuna mahali aliomba msamaha, Picha na sauti zipo (Video)
2. Amekiri sauti aliyotumia pengine haikuwa sahihi kwa wakati na hoja
3. Kaeleza kama hiyo ni sababu basi ni maumbile yake ambayo si lazima yafanane na mwingie
4. Kaeleza kulikuwa na mabadiliko ya ratiba badala ya kutoa shukrani akaanza yeye.
Hii maana yake hakuweza kusema aliyotarajia kutokana na mabadiliko.
5. Aliongea kama Mwenyekiti wa TCD na akaona ni vema achomekee hoja hiyo
Kwa maelezo ya Zitto pengine yanaeleweka kwa baadhi na wengine hayajitoshelezi au ni prejudice tu. Hilo linabaki kwa kila mtu
Kitendo cha Zitto kukiri kuhusu ''tone and humility '' ni cha kiungwana kabisa! Kakubali kosa
Upande wa Pili
Kauli za kinyonge haukuanza na Zitto. Kule Mwanza Chadema walimuomba Rais aliponye Taifa. Zitto akamuomba Rais aliunganishe Taifa, tofauti ni nini ?
Wapinzani wajue tofauti ya haki (Rights) na fadhila (Privilege) na maana ya statement.
Mbele ya hadhra, mtu anatakiwa awe na Respect lakini haimuondolei haki ya statement.
Zitto alivyofikisha ujumbe haikuwa statement ndiyo maana watu wanaitafsiri kama ombi. Hakutakiwa kuwa na lugha kali au kufoka la hasha, alitakiwa kutoa statement.
Mfano, angeweza kusema '' Suala la Mbowe linaichafua nchi mbele ya dunia, linaharibu taswira ya serikali, linajenga mfarakano miongoni mwa wananchi! halifai na liondolewe mahakamani haraka''
Zitto alikuwa na ''extreme humility'' hivyo aka adulterate the meaning ya statement.
Humility and humbleness ilikuwa katika sura ya ''maombi'' na ndipo wengi wanapomjia juu.
Suala siyo nini kasema, ninajiuliza kulikuwa na sababu ya kuhudhuria mkutano ule ?
ACT wamepigwa sana chaguzi zote walizoshiriki na CCM, hivi bado wanaamini CCM inaelewa lugha ya kawaida!
Je ushiriki wa ACT umesaidia nini zaidi ya kutia mhuri 'viraka vya katiba'?
Hivi bado ACT wanaamini ushiriki wao na CCM utatoa matokeo tofauti na yale ya CUF?