Nani kamtuma Zitto Kabwe kuomba Mbowe aachiwe huru?

Mkuu hili jambo lina mengi ndani yake na naomba niyapitie kwa mtazamo wangu baada ya kusikiliza Chadema na Zitto katika 'space' moja

Zitto
1. Hakuna mahali aliomba msamaha, Picha na sauti zipo (Video)
2. Amekiri sauti aliyotumia pengine haikuwa sahihi kwa wakati na hoja
3. Kaeleza kama hiyo ni sababu basi ni maumbile yake ambayo si lazima yafanane na mwingie
4. Kaeleza kulikuwa na mabadiliko ya ratiba badala ya kutoa shukrani akaanza yeye.
Hii maana yake hakuweza kusema aliyotarajia kutokana na mabadiliko.
5. Aliongea kama Mwenyekiti wa TCD na akaona ni vema achomekee hoja hiyo

Kwa maelezo ya Zitto pengine yanaeleweka kwa baadhi na wengine hayajitoshelezi au ni prejudice tu. Hilo linabaki kwa kila mtu

Kitendo cha Zitto kukiri kuhusu ''tone and humility '' ni cha kiungwana kabisa! Kakubali kosa

Upande wa Pili
Kauli za kinyonge haukuanza na Zitto. Kule Mwanza Chadema walimuomba Rais aliponye Taifa. Zitto akamuomba Rais aliunganishe Taifa, tofauti ni nini ?

Wapinzani wajue tofauti ya haki (Rights) na fadhila (Privilege) na maana ya statement.

Mbele ya hadhra, mtu anatakiwa awe na Respect lakini haimuondolei haki ya statement.

Zitto alivyofikisha ujumbe haikuwa statement ndiyo maana watu wanaitafsiri kama ombi. Hakutakiwa kuwa na lugha kali au kufoka la hasha, alitakiwa kutoa statement.

Mfano, angeweza kusema '' Suala la Mbowe linaichafua nchi mbele ya dunia, linaharibu taswira ya serikali, linajenga mfarakano miongoni mwa wananchi! halifai na liondolewe mahakamani haraka''

Zitto alikuwa na ''extreme humility'' hivyo aka adulterate the meaning ya statement.
Humility and humbleness ilikuwa katika sura ya ''maombi'' na ndipo wengi wanapomjia juu.

Suala siyo nini kasema, ninajiuliza kulikuwa na sababu ya kuhudhuria mkutano ule ?

ACT wamepigwa sana chaguzi zote walizoshiriki na CCM, hivi bado wanaamini CCM inaelewa lugha ya kawaida!

Je ushiriki wa ACT umesaidia nini zaidi ya kutia mhuri 'viraka vya katiba'?

Hivi bado ACT wanaamini ushiriki wao na CCM utatoa matokeo tofauti na yale ya CUF?
 
Asante sana kwa maoni mazuri na upembuzi huu yakinifu mkuu....!
 
Nimesikiliza debate ya Zitto na Lissu kule clubhouse, points alizoraise Zitto nimezikubali maana zinamake sense

1. Mosi suala la kuhudhuria kikao au kutohudhuria kikao ni uamuzi wa chama si matakwa y mtu binafsi, Chadema kupitia kamati kuu yao waliamua kutohudhuria wakati vikao vya ACT waliamua kuhudhuria. Kila chama kistick na maamuzi ya vikao vyake badala ya kunyooshea vidole wenzao

2. Huko Nyuma almost kamati kuu nzima ya Chadema imewahi kwenda kutafuta maridhiano na JPM huko mwanza, Chadema walipofanya hivyo vyama vingine havikuwanyooshea vidole kuwa wamesurrender.

3. Zitto ni mwenyekiti wa TCD, Wajumbe wake ni haohao akina Cheyo na wengineo, ingekuwa ajabu mwenyekiti wa TCD kwa utashi wake wa kisiasa asihudhurie mkutano ambao wanachama wake majority wanahudhuria

4. Zitto anaamini katika incremental approach ya kupata kitu, yaani you gain some and then you keep on claiming for the rest, wakati Chadema wanataka kitu chote papo kwa papo.

5. Chadema huwa wanapenda kusakama wenzao, lakini ni wao waliomchukua Lowasa, mtu waliyemuweka kwenye list of shame ya ufisadi, tena mtu ambaye alipokuwa CCM alikuwa akipinga katiba mpya na kisha kumfanya mtu huyo candidate wao wa kiti cha uraisi. Hii badili gia angani inawacost Chadema kutoaminika mpaka leo maana wanaonekana ni watu wenye kucomprise vitu vya msingi kwa ajili ya power. Kwa hiyo hata wanapomskama Zitto usaliti, hata wao walishawasaliti watanzania kwa kutaka kumuingiza Ikulu fisadi.

6. Zitto ana wisdom sana, upeo wake wa mambo ni mkubwa. Ni muhimu sana wanachadema wakaacha kujaribu kushambulia character yake kwa sababu kwanza hawaleti ushahidi wa usaliti wake, ni accusation tu za kimkakati za kujaribu kumuondolea Zitto credibility na imani kwa wananchi, kitu ambacho siyo haki, na siyo sawa. Kama ni mchezo wa kisiasa, Zitto anafanya siasa, Na siasa alizochagua Zitto ni engagement, siyo disengagement.

7. Ingekuwa ni ajabu kwa Zitto na ACT kutokwenda kwenye ule mkutano wakati makamu wao wa rais Othman Masoud ni mgeni mwalikwa.

8. ACT wameshawaingage CCM na hata rais Samia huko Zanzibar kwenye issues nyingi ikiwemo uchaguzi wa Konde, kwa hiyo wao kukaa chini na kudiscuss issues za kitaifa na CCM siyo falsfa ngeni kwao. Ndiyo njia wanayoona wao kama chama inafanya kazi. Sasa tusianze kumshambulia Zitto, wakati anachokifanya ni falsafa ya chama chao.

Zitto ni mti uzaao matunda, unapigwa mawe kila kona, ni kijana mwenye upeo mkubwa na anaonewa wivu na wengi
 
Leo kwenye hili napingana na Yericko na wote wanaomshukia Zitto. Mambo ya msamaha ameleta rais.
By the way, serikali imeshamdhulumu vya kutosha Mbowe. Ifike wakati tuseme inatosha.
 
CHADEMA WANAKOSEA

Badala ya kumshambulia Rais kwa hotuba ambayo ilijaa upotoshaji mwingi ambao hata haukufanana na alichokisema Zitto Chadema wanapoteza muda kumsakama Zitto ambaye alikuwa anawasaidia ili Mbowe aachiwe baada ya mbinu zao za kutumia mabavu kutozaa matunda.

Hivi mnafikiri Rais atafuta ile kesi na kumuachia Mbowe kwa namna inayowanufaisha Chadema kisiasa? Huko ni kujidanganya. Rais atamuachia Mbowe katika staili itakayomfaidisha kisiasa.

Zitto kaliona hilo kwa sababu akili yake ni ya kisasa. Haongozwi na chuki na visasi katika siasa zake. Hizo siasa za jino kwa jino Chadema hawana ubavu nazo sasa hivi.

Siasa hizo zinawezekana pale mnapokuwa na wafuasi madhubuti wanaoweza kuendesha migomo na maandamano. Chadema hamjafikia hapo. Hata kwenye mapambano kuna kurudi nyuma na kujipanga upya.

Chadema wajiulize toka wameanza kutumia siasa za mabavu walishanufaika na nani. Zaidi naona wanaendelea kupoteza. Msikimbilie siasa za mabavu ambazo kwa sasa hamna uwezo nazo kwa sasa. Mambo haya huenda hatua kwa hatua.
 
UKIUNGANISHA NUKTA UTAKUTA KANA KWAMBA LILE SWALI NA JIBU , VILIRATIBIWA MAPEEMA , NA ZZK NDIO MAANA HAAMINIKI KWANI ALIULIZA SWALI SAWA....!! LKN MBONA JIBU TOKA KWA SSH, LILIKUWA LIKO KWENYE MAANDISHI....................?? ALIKUWA ANAMJIBU KWA KUSOMA KARATASI , ULE NI MPANGO KATI YA SRIKALI NA VINAVYOJIITA VYAMA VYA UPINZANI . ukiondoa CDM). KIMSINGI NAHISI SERIKALI IMEBANWA NA INAUMBUKA HIVYO WAMETENGENEZA SHIDA BILA KUJUA MADHARA YAKE SASA KWA KUWA WANAUMBUKA WANATAFUTA KUUTUA MZIGO KWA KISINGIZIO ETI WAMEMSAMEHE MBOWE, NYAMBAAFU.
 
Ushauri wa bure, haipendezi kuandika kila kitu kwa herufi kubwa.

Amandla...
 
Kwanza wewe si mdudu wala sisimizi ndani ya chadema, hutambuliki na hupendwi chadema. Wewe ni mtu mwenye kiherehere sana na mpenda sifa na mlafi wa pesa, kwa hiyi ni hatari kwa chama chochote cha siasa, wewe unanunulika kwa bei ndigo sana, huaminiki, ndio maana unajikomba sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…