Nani kati ya Makamu wa Rais na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi analidanganya taifa kuhusu suala la Samaki?

Katika mahusiano na biashara za kimataifa upo ujasusi pia ambapo makala nyingi zimewahi kuuzungumzia pia hapa jukwaani. Kiongozi wa nchi anaweza kulishwa mawazo potofu na hata akayaamini, na bila kupepesa macho akajikuta kayatamka hadharini pasipo kujua athari zake.

Viongozi huzungukwa na wataalamu mbalimbali, miongoni mwao ni wapo wenye maslahi ya kimkakati na nchi za nje hasa zile zilizokuwa washindani wetu wa kibiashara katika nyanja za kimataifa. Wanajua fika ya kwamba tone moja la mafuta ya taa hutosha kabisa kuharibu maji yote yaliyopo katika mtungi.
 
ALL AND ALL,TFDA SPECIAL SQUAD WAWEKE KAMBI MWANZA NA WA TRACE PROCESS ZOTE ZA KUANZIA UVUVI MPAKA UHIFADHI,PIA MALI KABLA HAIJA SAFIRISHWA NI LAZIMA IWE IMEPATA KIBALI MAALUM TOKA TFDA,NIKIMAANISHA SAMAKI WOTE WANAOLIWA NDANI NA NJE LAZIMA WAWE NA FORM YA INSPECTIONS.(wamekaguliwa na wako salama Kwa matumizi ya binadamu) au HALAL,
N.b,wafanyabiashara sometimes wanakosa utu.
 
Bila kujali ni kauli ya nani, iwe ni kweli au uongo, hiyo kauli haikutakiwa kuongelea hadharani.
Samaki ni biashara ya kimataifa, samaki kutoka Mwanza wanaliwa Congo mpaka Japan. Watanzania maelfu wameajiriwa kwenye sekta ya Samaki ambapo wanajipatia kipato hapo na serikali inapata Kodi.
Kama kiongozi anajua Kuna matumizi ya njia zisizofaa angetumia vyombo vya usalama kudhibiti Hilo, si kutangaza hadharani.
Hivi kesho na keshokutwa gazeti la nchi jirani (waibukia fursa) likiandika "Samaki kutoka Tanzania wakutwa wamehifadhiwa kwa formalin" tutamlaumu nani?
Watu wakishakosa ajira, yeye atapata wapi Kodi na tozo?
 
Naibu Waziri kajibu kisiasa, anafanya utani na mzaha kwenye uhai na maisha ya watanzania, nadhani Ulega must resign haraka sana, Mh. Rais aunde tume huru haraka kuchunguza hili suala, ni jambo hatari sana, huku Naibu Waziri akijibu kisiasa wala hajali kitu.
Mh. Makamu wa Rais atakuwa sahihi na najua ana taarifa zote, huku wizara na mawaziri wake wakikaa kimya na kula raha tu, mfano huyo Ulega ni bomu kweli huyo, hafai kabisa hata kuwa mbunge tu, yaani Naibu Waziri anajibu kirahisi tu kwa jambo hatari hivi tena anapinga alichosema Boss wake yaani Makamu wa Rais..
 
Huo ni mfano tu. Yapo mengi wanafanyia masihara sana
 
PM kapenyezewa chini ya kapeti na maafisa kipenyo
Sasa kama kapenyezewa taarifa, ameshindwaje kuweka kikosi kazi Cha kuwaondoa wanaoharibu biashara ya Samaki?
Akishasababisha kutetereka kwa biashara ya Samaki nje ya nchi ambayo imeajiri maelfu ya watanzania, atafaidika Nini?
Mwisho nikuulize, nani ana mamlaka ya kulidhibiti hito tatizo?
Ananiambia Mimi mwananchi wa kawaida nifanye nini, niache kula Samaki?
 
Utafukuza wahudumu wa mochwari si tutaozeana.wao ndio wafau wakuu wa hii biashara
 
Hili jambo ni "serious" Sana..............

Hata hivyo linajibiwa kisiasa tu!
 
Hawa CCM usiwaamni kabisa Kaka
 
Linapokuja suala la usalama wa watu, biashara inawekwa nyuma.

Dunia nzima inazungmzia transparency,wewe unaongelea mambo kufanyika gizani, kisa eti biasharara! Crap!

Kama Dr. Mpango ana taarifa sahihi, amefanya sahihi sana kuiweka taarifa hiyo public. Ni kweli ilikuwa inajulikana kuwa wagonjwa wa saratani, zaidi ya 60% wanatoka kanda ya Ziwa. Lakini sababu haijulikani. Huo ndio ukweli. Watu wa Kanda ya Ziwa, ambao ndio waathirika wakuu, wanatakiwa kujulishwa na mamlaka za Serikali, sababu ni nini?

Hypothesis ya kwanza imekwishatolewa. Utafiti wa kina unatakiwa kufanywa, lakini kwa kuwa matokea yanaweza kuchukua miaka, kipindi hicho, wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari. Kwa nchi zinazowajibika, kipindi chote cha kusubiria matokeo ya utafiti, ulaji wa samaki hao na biashara ya samaki hao, vingedhibitiwa kwa kiasi kikubwa mpaka uhakika wa jambo hili utakapopatikana.

Kwa sasa, tahadhari imekwishatolewa kinamna, unayesema mambo hayakustahili kuwekwa hadharani, endelea kula samaki hao bila tahadhari yoyote, wanaojali afya zao wachukue tahadhari.
 
Jukumu la kwanza la usalama wa afya yako, ni lako mwenyewe. Tangu ilipotolewa taarifa ile kuwa zaidi ya 60% ya wagonjwa wa saratani wanatoka kanda ya Ziwa, usidhani hakuna tafiti zinazoendelea. Bahati mbaya matokeo halisi ya magonjwa huchukua miaka, siyo sawa na kuchunguza chanzo cha ajali ya basi.

Aliyoyasema Makamu wa Rais, huenda ni matokea ya awali ya uchunguzi wa kitaalam ambao umekuwa ukiendelea.

Hingera VP kwa kauli ile kwa sababu inawapa nafasi wote wenye akili na wanaojali afya zao, kuchukua yahadhari.

Afya kwanza, kabla ya chochoye. Ndivyo wenye akili na jamii zinazojali uhai wa watu wake zinavyofanya.
 
Kwa ulimwengu wa kibepari, uhai ni kitu kidogo sana dhidi ya pesa! Ukiangali mataifa makubwa yanazalisha silaha kwa ajili tu ya kuuzia watu wakauane! Maana yake kwao wanathamini pesa kuliko uhai wa Raia.

Tanzania tuna ombwe la Ujasus katika masuala ya uchumi! hili ni tatizo kubwa sana. Wachumi wapo na wanaweza kuendelezwa kuwa wachumi wazuri tu.

Kikubwa hapa ni tatizo la mawasialiano ndani ya Serikali! ingawa taarifa ya Makamu wa Rais zina uhakika zaidi kwakuwa anazungukwa na taarifak kutoka vyanzo vingi vya usalama
 
ninapendekeza kuwa iundwe Tume huru ya kulichunguza jambo hili na matokeo ya Tume hiyo, yatolewe hadharani kwa Umma wa watanzania
Ohoo! Yaani unataka iundwe tume kuikosoa taarifa ya mhe makamu wa rais mwenye vyanzo vibgi vya taarifa?

Naibu waziri katumika kama kifuniko cha choo kufunika "ukweli mchungu" aliyousema mhe makamu wa rais.

Endelea kula Sato na Sangara at your own risk.
 
Kwani ni lazima kila jambo litatuliwe Kwa matamko kwanza? Mambo mangapi serikali inayadhibiti bila raia kujua?
 
Both
 
Ukiona mikanganyiko ya aina hii ndani ya serikali, basi juwa tuna hali mbaya sana kitaifa.

Tunaishi kwa kubahatisha tu!
 
Huyu Naibu Waziri ameamua kutudanganya watanzania, Ili kulinda soko la samaki.
Kwa manufaa ya nani?
Au tayar wajuvi wamempenyezea rupia na hivyo kumpofoa na kumpa ububu wa kuwatetea wananchi....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…