mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Katika mahusiano na biashara za kimataifa upo ujasusi pia ambapo makala nyingi zimewahi kuuzungumzia pia hapa jukwaani. Kiongozi wa nchi anaweza kulishwa mawazo potofu na hata akayaamini, na bila kupepesa macho akajikuta kayatamka hadharini pasipo kujua athari zake.Katika siku za Karibuni, zimetolewa kauli mbili tofauti toka kwa viongozi wakubwa kabisa Katika Serikali yetu ya CCM.
Kwanza ilitolewa kauli na Makamu wa Rais, Dkt. Philipo Mpango, akiwa jijini Mwanza kikazi, ambaye aliagiza vyombo vyote vinavyozibiti maji ya kuoshea maiti yenye dawa ya chloroform, aliyodai kuwa yanatumika kuhifadhi samaki, kwa hiyo akaelezea wasiwasi wake kuwa, kuna ongezeko kubwa la wagonjwa wa saratani nchini, ambao kwa maelezo yake, ongezeko hilo linatokana na ulaji huo wa samaki, ambao wanahifadhiwa kwa kutumia maji hayo ya kuhifadhia maiti.
Baada ya siku chache, akaibuka Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, tena ndani ya Bunge letu jijini Dodoma, akikanusha vikali taarifa hiyo ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, aliyoitoa na kuiita kuwa ni ya uongo na ya kufikirika!
Watanzania tunataka kuujua ukweli, Katika hili jambo nyeti Sana, linalohusu uhai wetu, je ni Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, au ni Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, ambaye amelidanganya Taifa letu?
Kuliacha jambo hili hivi hivi tu, ni kuhatarisha uhai wa mamilioni ya watanzania, ambao ni watumiaji wa samaki hao, iwapo kauli ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango itakuwa ya kweli.
Mimi binafsi ninaamini kuwa, kauli iliyotolewa na Naibu wa Rais, Dkt Philipo Mpango, siyo ya kukurupuka na itakuwa na ukweli, kwani atakuwa amepewa taarifa za uchunguzi na wataalamu wa wizara hiyo ya Mifugo na uvuvi.
Kwa kuwa jambo hili ni kubwa Sana na linahusu uhai wa mamilioni ya raia wa nchi hii, wanaotumia bidhaa hiyo ya samaki, ninapendekeza kuwa iundwe Tume huru ya kulichunguza jambo hili na matokeo ya Tume hiyo, yatolewe hadharani kwa Umma wa watanzania na itakapogundulika mmoja wao, Kati ya Makamu wa Rais, Dkt Philipo Mpango au Naibu Waziri wa Mifugo na uvuvi, Abdallah Ulega, amelidanganya Taifa, basi awajibike kwa kujuzulu wadhifa wake mara moja, kwa kuudanganya Umma wa watanzania [emoji3064]
Mungu ibariki Tanzania.
Viongozi huzungukwa na wataalamu mbalimbali, miongoni mwao ni wapo wenye maslahi ya kimkakati na nchi za nje hasa zile zilizokuwa washindani wetu wa kibiashara katika nyanja za kimataifa. Wanajua fika ya kwamba tone moja la mafuta ya taa hutosha kabisa kuharibu maji yote yaliyopo katika mtungi.