Nani khasa huyu Ali Mwinyi Tambwe...Mzalendo, jasusi, shujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar 1964?

Nani khasa huyu Ali Mwinyi Tambwe...Mzalendo, jasusi, shujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar 1964?

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KUTOKA RAIA MWEMA: ALI MWINYI TAMBWE NI NANI HASA? MAKALA YA EZEKIEL KAMWAGA
Mohamed Said July 05, 2017 0


Chini katikati waliokaa ni Sheikh Kassim Juma
Nyuma kushoto ni Sheikh Hassan bin Amir, Al Habib Sheikh Omar bin Sumeit na Abbas Sykes
Nyuma katikakati ya Al Habib Sheikh Omar bin Sumeit ni Ali Mwinyi Tambwe

Raia Mwema limemwandika Ali Mwinyi Tambwe katika moja ya makala zake katika toleo la Julai 5 - Julai 11, 2017. Binafsi nimemfahamu Ali mwinyi Tambwe toka utoto wangu. Nilikutana na Ali Mwinyi Tambwe katika Nyaraka za Sykes wakati wa utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes na hivi ndivyo nilivyomwandika Ali Mwinyi mzalendo aliyefanya mengi lakini yeye mwenyewe hakupenda kuyaeleza:

1954
''Kumbukumbu zinaonyesha kwamba Idd Faiz Mafongo alihudhuria mkutano wa uzinduzi wa TANU katika Ukumbi wa Arnautoglu. Haifahamiki kwa hakika hasa ni lini Idd Faiz alijiunga na TANU kwa sababu kadi yake ya kwanza ya uanachama ilipotea na akapewa kadi nyingine iliyokuwa na namba 915 iliyotolewa tarehe 28 Agosti, 1954. Lakini kwa kukisia tu kutokana na kadi ambayo Idd Faiz mwenyewe aliitoa kwa kaka yake Idd Tosiri ambayo ilikuwa kadi namba 25 na yenye saini yake kama afisa aliyetoa kadi hiyo, inaweza kuchukuliwa kwa uhakika kuwa Idd Faiz alikuwa miongoni mwa wale watu wa mwanzo kabisa kuingia TANU na huenda akawa miongoni mwa wanachama ishirini wa mwanzo. Ukichukua katika fikra ukweli kwamba Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya aliingizwa TANU na Mtemvu katikati ya mwezi Agosti, 1955, huenda Ally Mwinyi kama katibu wa Al Jamiatul Islamiyya na Idd Faiz akiwa mweka hazina, wote wawili waliingia TANU wakati mmoja.''


Kushuto: Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu, Dodoma. Idd Faiz Mafongo alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pi Mweka Hazina wa TANU chama kilikpoasisiwa 1954. Yeye ndiye aliyeaminiwa kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO, New York 1955



''Ilikuwa wakati Nyerere yuko Musoma ndipo John Hatch kutoka Chama cha Labour cha Uingereza alipokuja Tanganyika kama mgeni wa TANU. Chama kilifanya mkutano mkubwa sana Mnazi Mmoja na Hatch akawahutubia wananchi. Inakisiwa takriban wanachama wa TANU na mashabiki wake jumla yao kiasi watu elfu ishirini walijitokeza kwenye mkutano huo. Ali Mwinyi Tambwe alikuwa mkalimani wa Hatch. Denis Phombeah pamoja na katibu mkuu wa TANU, Oscar Kambona vilevile walihutubia halaiki ile. Hatch akiwa anaunga mkono ukombozi wa watu weusi aligundua kuwa TANU haikuwa na tawi la akina mama. Katika dhifa ya chai iliyoandaliwa na TANU kwa heshima yake, Hatch alilieleza tatizo hili kwa Schneider Plantan na John Rupia.Hatch alimwambia Schneider kwamba ili kuwa na chama chenye nguvu TANU isiwaache akina mama nyuma. Hatch alimwambia Schneider kwamba huko Uingereza Chama cha Labour kilikuwa kimejikita kwa wanawake kama moja ya nguzo yake kuu.''




1955
''Mkutano mkuu wa mwaka wa TANU ulifanyika katika ukumbi wa Hindu Mandal mjini Dar es Salaam. Siku kabla ya mkutano TANU ilimwalika Gavana Edward Twining kwenye tafrija katika Ukumbi wa Arnatouglo lakini alikataa kistaarabu na akamtuma Chief Secretary, Bruce Hutt, kumwakilisha. Baada ya mkutano, wakati wajumbe wengine wanaondoka kurudi kwenye majimbo yao, Mpunga na Mnjawale walibakia nyuma kukutana na uongozi wa makao makuu wa Julius Nyerere, Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe, Said Chamwenyewe, Oscar Kambona na wengineo.Mpunga na Mnjawale waliwafahamisha viongozi wa makao makuu kuhusu hali mbaya ya siasa Jimbo la Kusini. Mbali na kampeni za kuipinga TANU zaMponda, katika ziara yake Lindi Gavana Twining aliwatahadharisha Waafriika wa Tanganyika wasijihusishe na ‘’wafanya fujo wanaotaka kuzusha vurugu.’’ Twining alikuwa akitoa onyo hili akiikusudia TANU ambayo ilikuwa imeanzishwa mwaka uliopita. Hotuba hii ya Gavana iliwatisha wananchi kujiunga na TANU. Mpunga na Mnjawale walisisitiza kuwa kuja kwa Nyerere mjini Lindi kulitakiwa haraka sana kukabiliana na vyote viwili, kwanza ile hotuba ya gavana na pili zile kampeni za kupinga TANU zilizokuwa zikiendeshwa na Liwali Yustino Mponda.''

''Wakati huo Abeid Amani Karume aliyehudhuria ule mkutano alimwalika Nyerere afanye ziara Zanzibar. Kitu cha kustaajabbisha ni kuwa, Nyererealionekana kuiafiki zaidi ziara ya Zanzibar kuliko ile safari ya kwenda kusini kuiimarisha TANU. Mpunga alimsisitizia Nyerere umuhimu wa yeye kwenda Lindi ambako kunaweza kuwa ndiyo chanzo cha TANU kupata ufanisi Newala, Songea, Tunduru na Masasi ambako kulikuwa na upinzani mkubwa dhidi ya TANU. Kanisa lilikuwa likiwazuia Wakristo kujiunga na TANU. Sheikh Suleiman Takadir, Said Chamwenye, John Rupia, Ali Mwinyi Tambwe wote waliunga mkono ule ujumbe wa Lindi juu ya suala hili. Baada ya kufikia makubaliano, Mpunga na Mnjawale walipewa barua ya kuthibitisha safari yaNyerere. Ziara ya Nyerere ilikuwa ianze muda mfupi kutokea hapo kwa kuwa ilikuwa ndiyo siku za mwisho za kiangazi. Barabara sehemu ya kusini ya Tanganyika zilikuwa hazipitiki wakati wa masika, zikiitenga kabisa kusini toka sehemu zilizobaki za nchi. Ali Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani walifuatana na Nyerere kwenda Jimbo la Kusini kuondoa wasiwasi na woga uliozushwa na Gavana Twining na kibaraka Yustino Mponda.''

Abeid Amani Karume

''Julius Nyerere, Ali Mwinyi Tambwe na Rajabu Diwani waliwasili Mikindani kutoka Lindi siku ya Jumamosi. Kabla ya kuwasili ujumbe huo, kazi kubwa kuliko zote waliyokuwanayo uongozi wa TANU Mikindani ilikuwa kutafuta mahali pa kumlaza Nyerere. Walimwendea Ahmed Adam, Mnubi mmoja tajiri na mtu wa makamo, aliyemiliki nyumba moja ya fahari. Nyumba hii ilikuwa ya ghorofa moja na ilijengwa kwa mawe na chokaa. Ahmed Adamaliombwa awe mwenyeji wa Nyerere na ujumbe wake. Nyumba hii tayari lilikuwa na kisa chake. Ilijengwa na hayati kaka yake Ahmed Adam baada ya Vita Kuu ya Kwanza. Kaka yake alikuwa askari wa Kinubi aliyekuwa katika jeshi la Wajerumani. Huenda alichukuliwa Misri mwishoni mwa mwa karne ya kumi na tisa na Wajerumani kuja Tanganyika kama mamluki katika jeshi la Wajerumani wakati wa vita vya Maji Maji. Baada ya vita alilipwa kiinua mgongo na serikali ya Ujerumani na kwa kutumia fedha hizo alijenga nyumba hiyo. Katika Vita Kuu ya Kwanza yeye alipigana katika jeshi la Wajerumani dhidi ya Waingereza. Baada ya vita Wajerumani wakiwa wameshindwa vita, Waingereza waliitikadi nyumba hiyo kama mali ya adui wa himaya ya Kiingereza na kwa hiyo ilibidi itaifishwe. Hii ilikuwa ndiyo nyumba pekee iliyokuwa nzuri yenye kumilikiwa na Mwafrika na kwa ajili hii haikuweza kukosa kuhusudika.''

...imeandikwa kwa msaada wa mada iliyowasilishwa na Aisha Daisy Sykes katika semina ya historia Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam mwaka wa 1968. Daisy aliandika mada hii kwa msaada wa baba yake Abdulwahid Sykes, kutokana na mswada ulioandikwa na Kleist Sykes. Angalia A.D. Sykes ‘’The Life of Kleist Sykes,’’ University of Dar es Salaam Ref. No. JAN/HIST/143/15). Habari nyingine kuhusu Al Jamiatul Islamiyya zinatokana na mswada ulioandikwa na Tewa Said Tewa, ''A Probe Into the History of Islam in Tanganyika,'' (haujachapishwa). Habari nyingine zinatokana na maelezo ya Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika miaka ya mwanzo ya 1940. Historia ya Nyerere na siasa za Jimbo la Kusini (Lindi) 1955 maelezo kutoka kwa Ali Mwinyi Tambwe, Yusuf Chembera na Salum Mpunga. Taarifa nyingine kutoka kwa Nyaraka za Sykes.
 
SYKESIOLOGY
Alfa...
Hakika umesema kweli.

Kisa chake kilianza na makala aliyoandika Joseph Kasella Bantu na ikachapwa
na New African (London) March na May 1985.

Katika makala ya Kasella Bantu iliyochapwa mwezi March na gazeti hili alisema
kuwa yeye aliisaidia TAA na TANU kwa kutoa fedha zake mfukoni kuendesha
mambo.

Mimi niliposoma ile makala nikaona kuwa kama suala la fedha wapo waliotoa fedha
nyingi kuendesha TAA na TANU na kubwa ni kuasisi na hivyo vyama vyenyewe African
Association 1929 na TANU 1954.

Mbona wazee wangu hawa siku zote hizi wako kimya hadi anakuja Kasella Bantu
kutaka kuidai sifa ambayo si yake kamwe?

Ikiwa Kasella Bantu anafikia kujinasibu hivi, Abdul Sykes angesema nini ingekuwa
katika uhai wake angeamua kuzungumza au Ally Sykes mwenyewe angezungumza?

RhA8K08kSi5dP1531Mo9K9HOso1dSHHVWIHWFJzoKadLHG_81Et1MZSieZ6X9V_raZpwOIsMCqwpnKb7lw1c407AVmsxkuTDCuIP2DcUzjTbmxBlfUH53YtP10oqB2iauq1Tg-lKwgGMPxdSrg6gv8pIkuesH_hQEdPfef9OeNvLT-_QfhdIKT9aMBEEDiLKplrEk77nqP3PoN4NKWqIeMa4VJ7bjchZGzRjrL__P_YoT7T0wX4aanDZaXFtNLMNEXbOZJv-2yiFo1BdnFp8EIopRwgZtGKa-K-AenHI2Uyu_QunwvQGSw3URlDnaXKZtbI_QJYQ9SqPATkCjDXvksaZxG5R129-qdUnIESCcAzR03wdennNZMGuRkyqwg71TGfAHgvGJ0EjH4Cxx_36BpBn7V3h6ILSSpaSbn9mQpPQXz0pXLQJtCLprDTNadqF324KMUxWdeG6MiQWbLc1Sj1jDOEOoWx97yXB9BlywPJfa05albmNhZGsyl3dbnKEv0Gn1rLNQfAD902ejm6CFUxGYEQiDSeEtPbK5jQeK1anSWyJ2Eb43-H2yhbpt7ueZYdhuWWAVSUwP-N3i5EYQDo1XqfeiSMQZ3ePQwf3Dsf9_e0YT3U8=w480-h349-no


Nikaandika makala kujibu makala ya Kasella Bantu ambayo ilichapwa mwezi May.

Lakini mhariri wa gazeti akaniandikia ujumbe kuniomba nimpe picha yangu kwa
kuwa makala yangu kaipenda sana angependa aichape na picha yangu.

Nilimpelekea picha yangu na ikatoka pamoja na makala ile.

Katika makala ile niliishambulia picha ya waasisi wa TANU ambayo Kasella Bantu
kwenye picha ''original,'' iliyochapwa na makala yake hakuwepo katika picha lakini
akaja kuitia picha halisi mkono kwa kuingiza picha yake.

Katika picha halisi watu watatu walijitoa kwa hofu ya kufukuzwa kazi na serikali kwa
kuasisi chama cha siasa.

Hawalikuwa Ally Sykes, Tewa Said Tewa na Kasella Bantu.

Kwa ufupi katika ile makala nilisema mengi ambayo wengi wakati ule hawakuwa na
ujasiri wa kuyasema ingawa waliyajua.

Ally Sykes aliposoma makala ile aliniita ofisini kwake.
Hapo ndipo mimi nikamwambia kuwa ninataka sana kuandika historia ya kaka yake.

Ally Sykes akaniambia kuwa ana safe imejaa nyaraka nyingi sana za wakati wa
kudai uhuru katika 1950s lakini hajui funguo zake ziko wapi.

Akaniambia nirudi baada ya siku tatu na ikiwa hajaziona funguo hizo ataivunja ile ''safe.''

Nilipokwenda alikuwa kazipata funguo na akanikabidhi kilima cha mafaili na nyaraka
nyingine.

Akanambia, ''Mohamed kasome kisha rejea tuzungumze.''

Hizi nyaraka hakuna mtafiti yeyote kabla yangu aliepata kuziona na zilikuwa ndani ya
''safe,'' kwa karibu miaka 30.

Sikuweza kuamini macho yangu kwa kile nilichokuta katika majalada yale.

Barua kutoka kwa Rashid Kawawa, Julius Nyerere, Chief Marealle, Kenneth
Kaunda, Zuberi Mtemvu, Peter Colmore, Lady Judith Listowel, Dr. Michael
Lugazia
, Dr. Wilbard Mwanjisi, Kasella Bantu, Japhet Kirilo...

Nilikesha nikisoma yale mafaili na nilikuwa kama mwendawazimu kwa mshawasha
niliokuwanao kila nyaraka ilikuwa ni kisa tosha cha kuandika sura nzima.

Vipi babu yake Sykes Mbuwane alivyotoka Mozambique kuja Tanganyika kama
mamluki wa Wajerumani chini ya Herman Von Wissman, vipi walikutana na
Julius Nyerere 1952, mambo lukuki ya kusisimua.

M_W4ZdLTlKb4l1WFw3v6BX7VkUSuev9xY_59L8qDwvJiNMhDG9D9jAjiHkaklM-twEnTlPqB_SkH6tws5FS0S1-7n-VhK_HN8pPgT6Cfqj5XqX5YuCI3l3ADzQ1oD_sjHClUQFF_YKCCxoTC7AGk0irDfQ1oEusw_WunHp7DSnbBPrKuBOkVPNQC1JFS8wT16al_M2wrRHfPwJ718Jkk8ayG4CCoHR6Tgjmug4MXl8NCFHCQj6CqJyShKV64nXvhuhpmv4tGn8wjB386Gy3h6km1aB9ny9nCUn8-NY4UiCwO4RjCfkruKBJjE9MQF3R2WIHU9NH4C95KWeMpmaWAUbHTMtsNiWMGjUB8ENCdcIE2K1ikAS27dPS7pMAbc3G1rsXG56_hKMfMjWWnoTGmIILtRq7D-cVkYRtvTLca1qvrSnUuBfB9RfeKwPBCGP3ekjeQbUfIw6D3T7sXlPZGi51qYT5fdHA93YriG0wmxJKDGd6-0ogkPn0Rr8mrBYPk3-2Y4IcWdyF52XxzU2mEFmfuYZ-CwwZzYZBuL4GKc68grdPGvzBqnfZN30v5Ofal_1jUtzrCjJt7IJFWPkla8LsobApK_1_HpuUneS-koxp-n-K9Ag=w493-h657-no

Moja ya Nyaraka za Sykes nilizowapa Kavazi la Mwalimu Nyerere

Nyaraka hizi, na mahojiano na wazee wangu niliowahoji kwingi na yale niiyoyajua kwa
kuzaliwa Dar es Salaam, Gerezani ndiyo yaliyoniwezesha kuandika historia hii ya TANU.

Kitu kimoja hakikunipitikia nilipokuwa naandika kitabu kile.
Sikutegemea kama kalamu yangu itachoma nyoyo za wengi.

DSCN0073.JPG


Alfa,
Nina mengi ambayo ningeweza kuhadithia lakini haya yanatosha kwa sasa.
 
Tukisema tuandike historia.
Itakuwa ndeeefu yenye kusisimua...
 
Tukisema tuandike historia.
Itakuwa ndeeefu yenye kusisimua...
Alfa...
Hakika kama ni ''script,'' kali sana mabingwa wa kutengeneza senema kama
Richard Attenborough, David Lean na Oliver Stone wanatengeneza picha
iliyo na sifa ya kuwa, ''Blockbuster.''

Hii historia nimeiandika si suala la kusema kama, ''tukisema tuandike historia...''

v_P3x3SKzwPpe0MWoGmk5K8a62VWgB7JjXRT552DHZprtDPw1-4E5Ctn5VhFUrh3uyGE4-4bKtLAXb1aF0PTz9sluw3ROIVPN6bKqqv3jOkNWAH2p9DfH6ZCAvpI-283wDu8ccJCcrG2olWvBecP7nKk9981-8YOKdm9HdrptMdfHd7cKeXmPWfMKn3KMDn1HC8KRR1PTKz-qm9DoN2CNWY7P3mXW8Uvhf7zNeC59Medt7FebEg0xtYcZ65D2UozCO7zbSiL3ByCqOQ0L49g3WtAbyoXoVsuWFn4TdFNXE-ONcKFGhDSbPqphMob4HmjlAlPOdv3JsIujQoDkLjb5ZQnNmHTkpJ1tBC-SX5CM8kYgoBWOIt4k96fP_RUfVOLEJUDqMc7YHAy9LGCIL1Qg94BiQjW5pxsj9wfPvbWrhv9Rg7-Ccgb2QRqHB0eZB2NsDQ8iDJ0sIj38qLLsIWmqLWnRjKuWed8JFRYlpigt6fdW8VURlfCR7V-OADCjUt37O9s72g6TcPvdFIWMKNNlmq8_a01-6eXPd3t9W6ViEpXBlZlHszsZhQxsLKEFGOA3ietLBwTAPBiCB0I2wS-c-MC7Mx9h_2HLReHjLmpvzY-BfUI=w852-h629-no


fuorZRmysnkU7cmnK9FGdRubYiIzoAjm7C08rUOiKfhJFm0oCBptldDruxAvQHX_TtLlcbh-NGmGCAUWQfbRlILZ_lofA4FXwvYVjaX6Yc68gp3Z31PMXMC42oKLOjMnWRhyIPIPRrpgHIO0vyBTs6n_VNFMTWGs0LJZq73Pn8-g1VAqhhuDDB8MNPy8SD5G2JsrtrvUjqyX2GeyRH8WaBcxiTPCrLoPcME61RPZMoQB3EaS9vrjKqQyQ_I-J3LGiY37HYSx1YUwZEREUbWzsAykb0yoWen0anXdLELi6Q87mmb4CnHmI25LObgXKRS2qMGDgs3W4mNYH0EA0r7ov0moDAmbNC2swMkUeZVM91cM5oGFY1SOOaeK9DKrp9RU4cB7e8hoUUP_xYl1ISomXseE9w_lNlF81R0HkOCFjBZKFjiA2gRQorZfN0P3ZwtxcGCWNmLsEexwl0qvI1bA4A3rswy7UTNv3sImLtfAFvZ3HKQ15P57g0GxCbHcVmxeuDJtz8gYowppidypCOJNQgt5i6jrM9ErXS6KuCyy7hgxBe3FZ17qAvykQNvG0ubpRPE_CL49p3CIrm2eFKrHPEZTIY_RJGJfPt7F4zzweNchMEVh=w857-h629-no
 
Al-Watan,
Ndugu yangu chakula cha rais kina uhusino gani na hoja iliyopo hapa Majlis?
Rais ni mtu wa umma na swali lolote la kumhusu mi halali hapa majlis ya wananchi, na wewe umepewa hishma ya kuulizwa swali.

Kama mwanahistoria kuna vizazi vitakuja kuuliza kama rais alijua kula chapati kwa mchuzi.

Una wajibu wa kutoa ujualo.
 
Rais ni mtu wa umma na swali lolote la kumhusu mi halali hapa majlis ya wananchi, na wewe umepewa hishma ya kuulizwa swali.

Kama mwanahistoria kuna vizazi vitakuja kuuliza kama rais alijua kula chapati kwa mchuzi.

Una wajibu wa kutoa ujualo.
Al Watan,
Bahati mbaya sifahamiani na Rais hata kwa mbali.
 
Hii mada ya Magufuli? Si kafungue uzi wake utapata majibu.

Au yanakuumiza unayo yasoma hapa sasa upo mbioni kuhamisha magoli?
Mada ya historia za viongozi. Kuna vingozi wengi wametajwa hapo juu.

Au unataka kumvunjia heshima Magufuli kwamba si kiongozi anayefaa kujulikana historia yake, anayefaa kujulikana ni Sykes tu?
 
Kwani unaowaandika wote unafahamiana nao?
Al Watan,
Naam.
Historia hii nimeandika baada ya kufanya utafiti wa muda mrefu.

Wengi wa wazalendo nilioandika historia zao nimewajua wao binafsi
na wale waliokuwa wametangulia mbele ya haki nimefanya mahojiano
na watu waliokuwa karibu na wao.

Angalia mfano wa picha hii hapo chini na ''caption,'' yake:


Kushuto: Idd Faiz Mafongo, Sheikh Mohamed Ramia, Julius Nyerere, Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu, Dodoma. Idd Faiz Mafongo alikuwa Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na pi Mweka Hazina wa TANU chama kilikpoasisiwa 1954. Yeye ndiye aliyeaminiwa kukusanya fedha za safari ya kwanza ya Julius Nyerere UNO, New York 1955

Idd Faiz nilifika nyumbani kwake Magomeni baada ya juma moja toka afariki.

Nilibahatika kuzungumza na bint yake, Biti Idd na alinieleza mengi kuhusu
baba yake kama alivyomsikia mwenyewe akihadithia siku zile za kupigania
uhuru wa Tanganyika.

Nilizungumza pia na mwanae wa kiume Faiz ambae nilimfuata Dodoma na
ndiye aliyenipa hiyo picha hapo juu.

Mwalimu Julius Nyerere mtu wa kwanza kunifahamisha alikuwa baba yangu
na aliniambia alimjua Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes 1952.

Mwalimu Nyerere ni mtu maarufu na mimi nimesoma kila kitabu na kila
''paper,'' inayomuhusu.

Alipofariki Mwalimu Nyerere mimi nilikuwa mmoja wa watu waliomwandikia
taazia iliyochapwa na gazeti la Mtanzania.

Sheikh Mohamed Ramia alikuwa sheikh maarufu sana Bagamoyo na Dar es
Salaam na mengi yake yanafahamika na wengi katika wanachama wa TANU.

Lakini nilipata historia yake kwa ndani kutoka kwa mpwa wake marehemu
Yusuf Ramia ambae alikuwa mbunge wa Bagamoyo katika miaka ya 1980
vilevile katika kitabu, ''Islam and Politics in East Africa,'' cha Augustus Nimtz.

Nimtz amemwandika sana sheikh katika kitabu hiki.

Vile vile nilipata mengi ya Sheikh Ramiya kutoka kwa rafiki yangu toka
utoto Maulid Tosiri, mtoto wa Idd Tosiri ambae ni mmoja wa wanachama
wa mwanzo wa TANU.

IwAL35axxlK5oQvZg1mu_TASqG0Ojb3TPgF67cJJdqyVmAuurtX49_iVso8MWRPLjsT_-WZy28WWhhrBGmKpnkf5AQ187fqyon_R25J4hWAbSkaR2FKZqp4Sdl8cH2J2j2tQG0LEb3ZiIrup0PFDdP7Ky4_AZSnZSPigcseW30-bZbEpzJ-hq83pyk6V2nDqbIQ5EYKyTjVyjtgIIaLE9WAfNkmJ4523rJV3ubGMaWLSFcoJYSHXFBERMS5OK0G58QzdmWhrs_FglVhq3-GKXLYA2BiNMai9qLwwdoet2ahzlMRKBD4I-Gf5XZeFqdfccFqoyoVoAzHOJjoTXOrMfizlHXWDbg1Vw8mxbiM2m-vlv2FLXqiAlBJ-YhpI2wA_eq8RIc28j6OlPs16A-EyHGXK6_HCfRb71Om769iPe5eivEj05kgo3i8qLec-IdE8J8sjnvejSY_auHyb2b-0iLPS6Ubi3-lSzDjdp4oOr2apBToOKA97d-PPIsSy4s1r0iUb7WspHK5FF7T15dI5IFl9cqFgQRrI-qHkjiq36xEz6DzlKfLTJRtHNqzLNyTmMP8En4hzJth4ckS8JWa-nuvs3GDFIQ1exwHAwMc4Jd4oawKfxA=w839-h629-no

Katikati aliyevaa koti jeusi ni Idd Tosiri na huyo mtoto aliyevaa pia koti jeusi ni Maulid Tosiri
(Picha kwa hisani ya Maulid Tosiri)

Idd Tosiri na Sheikh Ramia ni mtu na kaka yake na ilikuwa Idd Tosiri na
Idd Faiz ambao hawa ni ndugu ndiyo waliomjulisha Nyerere kwa Sheikh
Ramia
mwaka wa 1954 ili amuunge mkono TANU ipate wanachama katika
murid (wafuasi) wa Tariqa Qadiriyya ambayo yeye Sheikh Ramiyya ndiye
alikuwa Khalifa, yaani kiongozi.

Saadan Abdu Kandoro nilisoma kitabu chake, ''Mwito wa Uhuru.''

Haruna Taratibu
nilifanya mahijianonae ofisini kwake Dodoma mwaka
1987.

Alifurahi sana kusikia kuwa kuna kijana anaandika historia ya TANU.

Alinipokea kwa bashaha kubwa na tulikaa ofisini kwake Dodoma na kwa
kweli ilikuwa kama vile napigiwa hadithi.

Kalamu yangu ilikuwa inatoka mstari mmoja kwenda mwingine na mkono
wangu ulikuwa na kazi ya kugeuza kurasa moja kwenda kurasa nyingine.

Haruna Taratibu alikuwa mzungumzaji hodari sana.
Hivi ndivyo nilivyowajua wazalendo hawa waliopigania uhuru wa Tanganyika.
 
Mada ya historia za viongozi. Kuna vingozi wengi wametajwa hapo juu.

Au unataka kumvunjia heshima Magufuli kwamba si kiongozi anayefaa kujulikana historia yake, anayefaa kujulikana ni Sykes tu?
Al Watan,
Sijui kwa nini unasema maneno haya.
Sithubutu kumvunjia heshima rais au yeyote awaye yule.

Mimi nimeandika historia ya waliopigania uhuru wa Tanganyika na nimenza
kutokea enzi za African Association katika 1920s hadi uhuru ulipopatikana 1961.
 
Back
Top Bottom