Al Watan,
Historia isingemfahamu
Ali Mwinyi Tambwe kama si kule
kwake kwanza kutajwa katika
Nyaraka za Sykes na mimi
kueleza historia yake.
Lakini mimi nilimwandika kama mzalendo na mmoja wa
viongozi katika Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na katika
TANU.
Hii ndiyo ilikuwa historia yake kama ilivyokuwa katika nyaraka
hizo.
Mwaka wa 2012 katika mazungumzo na marehemu
Kitwana
Kondo ndipo akanifahamisha kuwa
Ali Mwinyi Tambwe alikuwa
jasusi katika Special Branch.
Mzee Kondo na Mwandishi hii ndiyo siku aliponisomesha kuhusu Ali
Mwinyi Tambwe ilikuwa tarehe 12 September 2012 kabla ya mahojiano
ya TV Imaan
Historia hii nikaifungulia uzi hapa Majlis.
Inaelekea hii imekupita hukuisoma.
Sasa kichwa cha uzi huu ni kutoka makala ya
Ezekiel Kamwaga
nami nikaiongezea maneno.
Ukimsoma
Ali Mwinyi katika uzi wangu uliopita na ni audio utamjua
huyu mtu alikuwa nani.
In Shaa Allah nitakuwekea link.
Hapa ni Elimu tu Bila Khiyana chembelecho
Maalim Faiza.
Al Watan ingia hapo chini:
Mohamed Said: KISA CHA ALI MWINYI TAMBWE NA KITWANA SELEMANI KONDO 1950s
<iframe width="560" height="315" src="
Kisa Cha Ali Mwinyi Tambwe - YouTube" frameborder="0" allowfullscreen></iframe>