Nani kuondolewa kwenye Baraza la Mawaziri lijalo?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Mwigulu Nchemba atazimudu siasa za wizara ya ulinzi kama tetesi zinavyosema au ndo atakwenda kupeleka siasa za wizara kwenye Jeshi? Kwangu mimi huyu si mtu sahihi kwa wizara ya ulinzi. Mzee Mkuchika anatajwa pia kwenda Ulinzi, yes will be chaguo sahihi lakini Bado tunaamini ana health strength yakuhudumu Kama Waziri? Kwangu mimi Mzee aachwe apumzike tusimchoshe. Anatajwa Simbachawene kwenda Ulinzi na Masauni kwenda Mambo ya Ndani. Masauni No, Simbachawene Yes. Kwa muktadha wa bla bla zinazoendelea naomba niseme mabadiliko yafutayo yanaweza kuleta tija

Bi. Stergomena Tax Waziri wa fedha, Charles Kimei Naibu Waziri wa fedha. Kwangu hii chemistry haina siasa nyingi na itajenga nidhamu ya kitaasisi ndani na nje endapo watapewa uhuru.

Simbachawene wizara ya Ulinzi, akisaidiwa na Masauni. Ndugulile Afya huku January Makamba akienda Mawasiliano.

Mwigulu Nchemba uwekezaji huku Kitila Mkumbo, DOROTH GWAJIMA wakisubiri bench kuona kama kidogo gurudumu litasogea.
 
Yaani Mkuchika umpeleke Ulinzi ni sawa na hii kauli maarufu ya diblo dibala hapa chini👇🏻👇🏻👇🏻

 
She obtained her Bachelor of Commerce degree in Finance from the University of Dar es Salaam in 1991. She thereafter obtained a Master of Philosophy in Policy Management and Development Economics and a Doctor of Philosophy in International Development from the University of Tsukuba in Japan.


Huyu Bi Tax, CV yake ikoje ? Ni mwanauchumi??


Au jina lake "Tax" ndio sababu??
 
Habari za ndani sana za uhakika ni kuwa January Makamba anarudishwa kwenye baraza la mawaziri sasa, huenda akawa ni waziri wa Afya. Dr. Tax anaingizwa baraza la mawaziri (lakini sio wizara ya Fedha!). Wizara ya Ulinzi anapewa Mnzanzibar. Na huenda Ummy Mwalimu akawa waziri wa fedha.

Hizo ni tetesi rasmi.
 
Sawasawa, Kielimu Yupo Vzuri.

Bila shaka pia Ana uzoefu mkubwa .
 
Kwann mwanasheria awe waziri wa Fedha?.

Makamba asirudi.
 
Nani kuwa waziri Mkuu ?
 
Kumtoa mwigulu wizara ya fedha ni kosa kubwa sana mama atafanya.......angemwacha kwanza amalizane na hili la tozo. Hili wazo la tozo ni muhimu sana kwa nguvu ya serikali, for what a government without money?!!

Kumleta makamba barazani ni jambo jema sana na naomba litokee haswaa. Tukiongea ukweli, makamba yuko njema sana kichwani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…