Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Well Pinda could be the ideal candidate anything can happen and may be Pinda could be weak in some areas as well
 
Magufuli mtendaji kweli,alimfunika JK ndo maana akatupwa kupambana na wakojani kwenye uvuvi!!
u no war i mean!!

Na isitoshe ilikuwa mikakati ya kumumaliza kisiasa apotelee kwenye vumbi, lakini kamanda bado anakamua kwa kwenda mbele! du mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!
 
hata akimnyima magufuli ....hawezi kumzuia kuwa rais 2015

Inamaana CHADEMA haitachukua madaraka 2015? Mmh labda kama mwenyekiti Mbowe atakuwa hajakamata usukani. Unamfahamu lakini vizuri huyu strategist wa CHADEMA au unadhani kuwa KUB ameenda kula tu bata? Subiri uone!
 

Kumbe source yenyewe ni kutoka kwa mbea wa Ikulu na sio mtu timamu alieko ikulu? Kimsingi ni taabu sana kumwamini mbea. Ila kama ni kweli huyo "mbea" kapatia na yuko sahihi basi mmhhh!!! kuna walakini. Mimi siamini sana uwezo wake wa kiutendaji ila nimesikikia sikia kele za 2015 na bwana Member ndani, sasa sijui. LETS WAIT AND SEE, TIME WILL TELL
 

umetumwa au umejituma?
 
So kwa hali iliyopo sasa hivi kwa jinsi watu walivyo bet hicho kiti cha uwaziri mkuu its between MAGUFULI, MEMBE, ANNA TIBAIJUKA, PINDA, MWANDOSYA maana haya ndio yamekuwa yakitajwa sana lakini lolote laweza kutokea na kuletewa mtu ambaye hatukumtarajia
 

Hata record ya kuanzisha BAWATA iliyokuwa tishio kwa UWT huikumbuki?
 
ni bado masaa machache tusubire tuone , lolote laweza kutokea hakuna sababu ya kupata homa

MZEE GOMEZI
 
Sasa kama hawasalimiani wanafanyaje kazi, magufuli alikua napelekaje ripoti yake kwa jk au lowasa alipokua waziri mkuu


mzee gomezi
 
Ahaa, hebu acha masikhara, Membe awe PM, kwa lipi alilotufanyia Wa TZ. Huyu jamaa ni too arrogance. Kujipendekeza kwa sana. Atakuwa kama yule mzee Fred Suluwali ambaye alikuwa vuvuzela la BM. Simpendi Membe, hana mvuto wa kuwa PM. Its better akarudi Mizengwe ya Kupindapinda:A S angry:.
 
Magufuli anafaa kuwa PM....................................................Lakini atamfunika mshikaji Presidaaa wa serikali yetu ya kishikaji..................
 
Kwakuwa Chama cha chaka chua matokeo kilishaanzisha mpango wa kuwajali wakina mama, mpango wa kumpa u PM mama Tibaijuka kilikuwa sahihi.
Mama huyu ana uwezo mkubwa sana ila sijui kwa mafisadi kama angefanya kwa amani.

Nionavyo mimi, hata wakimpa Magufuli atafurukuta siku mbili then kimya. CCM au chama ni system na sio individual element, system ni muunganiko wa elements kibao zinazofanya kazi pamoja ili kufanikisha au kutimiza lengo/malengo fulani. Hivyo mimi najaribu kuangalia elements zinazo unda CCM na serikali kwa ujumula napata kigugumizi kuamini kuwa kuna mtu anaaweza akasimama yeye kama yeye ndani ya CCM na kuleta mabadiliko ikiwa Mkubwa wake ni mchafu(hapa ni JK), wenzake ni wachafu ni ngumu kwake, kukuru kakara za Sitta zimeishiwa wapi?

Nadhani tuseme kweli tu, kuwa mambo yatakuwa yaleyale, mbona tunazunguka mbuyu? Kuzunguka Mbuyu sio kazi, bali kuukumbatia Mbuyu ndio kazi, hebu tukumbatiye Mbuyu.

Natoa HOJA
 
Sasa kama hawasalimiani wanafanyaje kazi, magufuli alikua napelekaje ripoti yake kwa jk au lowasa alipokua waziri mkuu

mzee gomezi

Lisilowezekana kwenye fikra zetu, kwa CCM na JK linawezekana.
 
Tibaijuka ni sleki sana, hii nchi inahitaji jembe ulaya ili iende. huyo mama aende wizara ya viwanda ambayo haina kazi, na viwanda tz hakuna. kilimo kwanza hakiwezi. she is too sleki for it, naye ataishia kulia tu bungeni bila kuchukua hatua kama Pinda. we are tired of it.
 

Jamani jamani sasa kumekucha. Hata Membe anapigiwa chapuo?????? Tumwagie sifa zake unazozifahamu hapa. Mimi namwona 'zero carrier'. Tangu uhuru, sijawahi kumwona waziri mwoga na asiyeweza kutetea hoja aliyoitoa kama Membe. Jamani, tuache kukurupuka, yaani mtu akijisikia kuachilia thread anaivumisha tu!!
 
Mnahangaika nini kumjua PM nani? Kwa nini msimuuliza Ridhiwani? Anavyopenda ujiko atawaambia tu, si mnajua yeye ndio mshika furushi la Hirizi za Baba yake? Baba yake hana ujanja na hilo 'toto tundu'
 
Wacha uongo hizo habari ulizozipata wewe kutoka huko dodoma si sahihi... kwa taarifa yenu jina halijabadilika Pinda Mizengo kanda Peter a.k.a mtoto wa mkulima anaendelea na uwari mkuu kwa kipindi kingine cha miaka mitano kama utaendelea kuamini hivyo basi sikilizia hiyo saa kumi na moja
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…