Elections 2010 Nani kuukwaa uwaziri mkuu?

Status
Not open for further replies.
Waungwana waziri mkuu jina halijabadilika Mizengo Peter Kayanza Pinda ndiye waziri mkuu kwa miaka mingine mitano, source ni za kuaminika
 
A serious gvt will do a serious analysis for the quality output, i.e. best PM for the good of Tanzanians. The opposite is also true.
 

Mizengo Pinda ana nafasi kubwa ya kurudishiwa u-PM ingawa kitendo cha kuchelewesha jina la PM bungeni kinaacha maswali mengi zaidi.
 
MAGUFULI ni bomba zaidi.
Kwan inji hii ilipo sasa, mtu aina ya Magufuli ndio anatufaa kama choice ni kwa hao wawili. Mambo yakinyooka then unaweza kumpa mama Tibaijuka.Tunahitaji mtu anayesema spoon spoon na sio kuzuga, pia some kind of a dictator!
 
Nionavyo mimi, uongozi wa juu tanzania ni mzigo mkubwa sana kwa walipa kodi, especially baada ya mabwana wakubwa hao kujihalilishia maslahi makubwa wawapo madarakani, na mafao ya makubwa mno wanaopotoka madarakani, achilia mbali yale wanayoiba. Kibaya zaidi wote huwa wana sifa hizi:

1. Hawana uzalendo wa kweli
2. Hawana uthubutu wa kukemea,kushauri na hata kupingana na wakubwa na hata ikibidi wajiuzulu kwa kukataa kushinikizwa kufanya maamuzi yanayowaumiza walipa kodi.
3. Wamejaa unafiki na kazi zao ni kusoma tu hotuba walizoandaliwa.

Mfano; ni nani mwenye ubavu wa kumkosoa, kumpinga rais endapo atatenda au ataenda kinyume na taratibu?? Kazi hiyo inafanywa na walio nje tu,especially wapinzani.

Kwa mantiki hiyo sioni sababu ya kuumiza kichwa kutafuta waziri mkuu mwingine, cha msingi hapo ni kulipungizia taifa hili limzigo la kuendelea kulea vigogo lukuki ambao wamepata kulitumikia taifa hili, na ndio maana ningekuwa na uwezo wa kushauri, nimemshauri kikwete amrudishe huyu mizengo pinda kwenye nafasi aliyoishika kwa miaka hiyo mitatu.kinyume chake tutaongeza tu idadi ya mawaziri wakuu wastaafu bila sababu ya msingi.
 

Pamoja na mapungufu ya wasomi wetu lakini jamani tukubali kuwa si wakati wote hao wasomi wanaganga njaa. Kwamfano kwenye project planning and mangement hasa kuna assumptions unazotakiwa kuziweka ili kurealize out put; one is political will. Sasa msomi yeyote yule anayetaka kuleta effective change lazima ahakikishe anakuwa na political influence kwenye constitutional level otherwise nguvu yake inaweza potea bure na kuonekana hafai zaidi. Tunawashangaa wasomi wenye hiyo opportunity na bado wakaonyesha kushindwa!

Mm huyu mama nakumbuka alikuwa anataka kufanya kitu kwa taifa hili lakini somehow somewhere akawa frustrated na hatimaye kujikuta akienda nje. Pengine wakati ule alijifunza kitu na this time akaamua kuja katika sura inayokubalika zaidi kisiasa ili atimize kile ambacho alikitamani kukifanya wakati huo; sina uhakika najaribu kumuelewa kwanini akagombee ubunge wakati status yake ni zaidi ya hiyo? Mimi will wait to see to prove my hypothesis kwasababu by then alini aspire sana na mambo ya BAWATA ambayo ili promote sana vijana wakike.

Like wise for Batilda Burian wengi wetu tumeona jinsi gani ameweza kuonyesha jinsi gani anauwezo wakufanya kitu kizuri if at all she would have been independent in mind. Tatizo naliona nikukosa confidence na kusimama kama yy na hivyo kuhusishwa na watu wengine ambao hawakubaliki kijamii (Maoni binafsi si lazima niwe sahihi).

As a gender activist ningependa kuwapongeza wamama wote waliothubutu na kusimama kwa miguu yao nakushinda bila kuhusishwa na huruma za watu wengine kuwabeba and for this case my sincere congrats to Halima James Mdee na wengine nisio wafahamu kama wapo; mazingira ya kugombea kwake yalikuwa magumu zaidi ya wanawake wengine wote walioshinda Ubunge kwani kuwa upinzani pekee ilitosha kumnyima confidence ya kusimama na kushinda vikwazo vyote vya gender issues na political monopoly iliyopo nchini mwetu.
 
Pinda amepita bila kupingwa hivyo ni mwakilishi wa Jimbo. Anna Tibaijuka naye si alipita bila kupingwa, tofauti iko wapi.

Achana naye huyu jamaa naona anajikanyaga!nafikiri ana ajenda ya siri na huyu mama!hivi huyu mama mbona mnampromoti sana?amelifanyia nini hili taifa?au kufanya kwake kazi umoja wa mataifa?au huo usomi wake?Kweli nimeamini watanzania tuna papala sana!!
 

... kwani the real presidaa (RA) anataka nani awe PM?
 

Lipi bora, kumhudumia huyo Pinda kama waziri mkuu mstaafu au kuendelea kua na serikali iliyolala?? Tunahitaji kichwa kama cha Magufuli kikae pale juu kiamshe watu...Mawaziri wote watashika adabu, wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, akishika Magufuli wataomba kuacha kazi, wamezoea starehe, Ila Magufuli basi akikosa ni bora japo wamtupe Mambo ya Ndani, au wamrudishe kwenye wizara yake ya miundombinu kazi iishe!
 
pinda hakumkampenia jk ndo maana jk ana mihasira

mtotot wa mkulima
 

Wewe usijidanganye CCM wote wamelala hakuna mtu ambaye ana nafuu, Ila Nyerere aliyetangulia mbele ya haki wengine wote ni mafisadi, Kwa sababu wewe kama siyo mwizi kwa nini uanze kumficha na kuwatetea wezi. Tena bora ya Mwakyembe kuliko huyu magufuli mnayemtaja.
 
Sioni umuhimu wa kuwa na Waziri Mkuu kwenye serikali yenye rais tayari. Nafikiri huu ni mfumo mbovu unaochangia wingi wa gharama kwa serikali pia, na ni dalili pia kwamba marais wetu hawajitumi kama inavyotarajiwa kwa kutegemea waziri mkuu ambaye ndio mtendaji mkuu wa serikali....kwanini rais mwenyewe asiwe mtendaji mkuu?! Kazi hasa ya rais ni nini ukitofautisha na wazir1 mkuu?! For me, in many ways rais wa Tanzania anakuwa kama ceremonial leader tu ambaye hana active function in a daily life of Tanzanians....labda ndio maana JK anatumia nafasi kutalii muda wote.
 
waziri mkuu is another big surprise...

Makufuli maneno mengi kazi kidogo, tunataka watu chapa kazi kama kina Prof Mbilinyi (sijui aligombania ubunge maskini)
 
Ni gharama kuwatunza mawaziri wakuu. Hivyo mp is likely. Binafsi ningepdelea w/m awe self oriented. Driver.
 
Waziri Mkuu ni Pinda jamani jina halijabadilika
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…