Nani kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad?

Nani kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar baada ya kifo cha Maalim Seif Sharif Hamad?

Mbona sielewi Maalim Sefu Sharif Hamad amekufa?

Niko dunia gani mimi!
 
Ili siasa za Zanzibar zikae balance lazima mrithi wa Seifu atokee Pemba kwasababu wanachama na wafadhili wote wa ACT Wazalendo wanatokea Pemba, uongozi wa juu wote wa chama unatokea Unguja lakini chama pia lazima kiangalie uchaguzi wa 2025 kwa jicho la pili mtu pekee wa kupambana na Hussein ni Mansour Yussuf Himid au Nassor Manzurui wote hawa ni msumari kwa CCM, Duni umri umekwenda sana, Jussa ni rahisi kumchafua kwa siasa za maji taka.
 
Twende kikatiba zaidi...

Katiba ya zanzibar ya mwaka 1984 na mabadiliko yake toleo la 2010...
na utaratibu bado utasimamia UMOJA NA MUAFAKA hivo bado ACT wanayo nafasi kutoa jina litakalo rithi nafasi hiyo ili kuendeleza UMOJA NA MUAFAKA.
 
Juma Duni ndio natural Hair wa Maalim Seif. Japo kuwa Umri umekwenda, na pia amepoteza ushawishi kwenye chama na kwa wafuasi ukilinganisha na miaka ya nyuma. Lakini bado anabaki kuwa ndie most deserved one
Ningekuwa na maamuzi nisingeunga mkono jina la Babu duni,kwa sababu ya umri wake, Ni kweli amefanya mengi i'la anaelekea ukingoni Sasa,tupate kugroom damu mpya kabisa itakayokaa muda mrwfu kwenye siasa zetu, kwa sabbu Ni cheo Cha king'ora tu, tupate hata sura mpya ya kijana walau mwenye miaka 40 hiviii i'la tu tusiwe na mashaka na akili yake,uaminifu wake na imani yake ktk upinzani,wazee tuwalee vzr Sasa tuwahudumie wamefanya kazi kubwa
 
Maalim Seif alikua analeta balance kubwa kwenye siasa za upinzani Zanzibar, kiasi kwamba sasa wasipokua makini mambo yanaweza kuvurugika
Kwa Zanzibar ni ndoto ya mchana. Wazanzibari wote by nature ni wanasiasa. kila anaezaliwa anajuwa siasa na anafunzwa ni nini mission ya Zanzibar na umuhimu wake kwa ustawi wa Zanzibar in general. Kwa wale mnaodhani kufa kwa Maalim Seif ndio mwisho wa siasa za Zanzibar mnakosea sana!
 
Ni wazi kwamba Gwiji la siasa za Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki ( Apumzike kwa amani ) lakini ikumbukwe kwamba Zanzibar bado ingalipo na itaendelea kuwepo.

Sasa bila shaka Katiba ya Zanzibar inatambua uwepo wa Makamu wa Kwanza wa Rais, je imeeleza chochote jambo kama la kifo linapotokea? Na kama ACT Wazalendo wanaruhusiwa kujaza nafasi ya Maalim Seif unadhani ni yupi awezaye kuvaa viatu hivi?
SIna uhakika, ila kulingana na jinsi nafasi hiyo hujazwa, inaonekana kuwa ni kwa matakwa ya rais Mwinyi tu; anaweza kumteua mzanzibari yeyote kushika nafasi hiyo, siyo kwa ajili ya ACT-Wazalendo tu au chama chochote.
 
Makamu wa rais wa nini wakati nafasi hii ilikuwa imefinyangwa kumtuliza Seif kuepusha vurugu? CCM walifunika kombe mwanaharamu kupita. Japo Seif amesifiwa sana, alikuwa na tamaa kwa manufaa binafsi hadi kuhatarisha maisha ya wafuasi wake.

Nadhani suala la umakamu wa rais wa kupewa huu ndiyo mwisho wake. Walishindwa sawa na wenzao wa bara. Mnawapa umakamu wa rais wa nini wakati aliyekuwa king'ang'anizi keshaondoka? Najua maneno haya yatawaudhi wapenzi wa maalim ila ndiyo ukweli.
 
Kwa Zanzibar ni ndoto ya mchana. Wazanzibari wote by nature ni wanasiasa. kila anaezaliwa anajuwa siasa na anafunzwa ni nini mission ya Zanzibar na umuhimu wake kwa ustawi wa Zanzibar in general. Kwa wale mnaodhani kufa kwa Maalim Seif ndio mwisho wa siasa za Zanzibar mnakosea sana!

Mkuu unachukulia poa, nimekaa Zanzibar, nakufahamu vizuri sana. Muda mwengine watu wanaweza kuhasimiana hali ya kuwa wote wana malengo mamoja.
 
Kwa namna ya siasa ya Zanzibar ilivyo nawaza tu, Hivi mkimteua Shekh Mselem kuwa makamu wa kwanza wa Raisi ,haliwezi kuwa pigo kubwa kwa CCM?

Sioni kwa sasa kama kuna mtu anaweza kumzuia Mselem kwa ushawishi Zanzibar.

Juma duni, Mazrui, Jusa na wengine kwa sasa CCM hawawaoni kama tishio.

Wasicho kitaka CCM Zanzibar ni mtu wa kuwaunganisha wazanzibar, Na hapa Ndipo nnapomuona Mselem. Kwa huyu shekh Wazanzibar lazima warudi tena kuwa kitu kimoja.
 
Back
Top Bottom