unafikiri kupindua nchi ni ishara ya uimara wa jeshi!!!
wacha nikupe shule fupi.
jeshi kupindua nchi na kutawala ni sawa na mtoto wa kwanza wa kiume kikiuka mwiko na kumlala mama yake mzazi,ndio sababu serikali hiyo haiwezi kutambulika na taasisi za kimataifa.
nchi yoyote ambayo ina mifumo imara ya kiusalama kama tanzania nk,haiwezekani jeshi kupindua nchi abadani,mfano wewe hujui kama inawezekana cdf,igp,na css wana kazi nyuma yao zinazowalazimisha kuwa watiifu kwa serikali,
nchi za kipuuzi puuzi ndio mapinduzi hutokea.
jeshi kuwa tiifu kwa serikali ni sifa njema kwa majeshi mengine ulimwenguni,na pia ni sababu ya kuheshimika zaidi.
iishie tu wewe kutaja silaha,ila swala la kuzitumia ni pana sana.ndio sababu kuna mwiko mwanajeshi anapoapa anasema"sitamgeuzia mtutu raia ninayetakiwa kumlinda"ikitokea hilo maana yake ni uasi tayari.
MWISHO:ili uelewe idara za kijasusi (usiwaze zile suti za walinzi)zinafanyaje kazi,kasome mapinduzi ya nkurunzinza 2014 yalivyo fail,au mapinduzi ya mwalimu nyerere na akina hanspop.yaani wakati unawaza jeshi limpindue rais na serikali yake,kuna wanajeshi wapo tayari wanakuongoza na kukupa kampani ili ukakamatwe.