Nani Mkubwa kati ya Mkuu wa Majeshi na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa?

Nani Mkubwa kati ya Mkuu wa Majeshi na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa?

Ni state nyuma ya state ya kawaida unayoiona. Ukiona kiongozi fulani amefanya uhalifu mkubwa wa wazi ila hapelekwi au amepelekwa mahakamani kisha hakimu/jaji anapatwa kigugumizi ujue hao ndio wenyewe...

Ukiona mtu maarufu amegombana na wakubwa kisha akawekwa ndani isivyo haki ujue hao ndio wenyewe...
Je deep state ni nini?
 
Usalama wa Taifa sio sehemu ya jeshi. Ni idara ya kiraia.
Huwezi undermine power of intelligence service. Hili ni jeshi la watu wenye akili na waliobobea ktk ku silence pasipo kuonekana ktk mazingira ya kawaida. Ingekuwa jeshi lina nguvu kuliko hawa jamaa basi ni dhahiri shahiri ingekuwa rahisi kupinduwa nchi ila hawa jamaa wana network ndani ya jeshi kwa kazi moja tu kulinda usalama wa Nchi. Jeshi halina intelligence walio nayo Tiss. Na ndio maana hata jeshi wana depend on taarifa ya Tiss. Why ? Mifumo yakiusalama kwa Tiss ni mipana sana nayenye nguvu hawana majeshi kama ya jeshi letu ila wao wanasilaha hatari sana sana ambazo vault yake wanaijuwa wao. Usalama wa Taifa ukiwa weak nirahisi kuangusha nchi ila ukiwa imara sio rahisi kuangusha nchi. Ndio maana unaambiwa Mkurugenzi Nzena alikuwa moja ya makachero alizuwia mapinduzi ktk taifa hili wakati wa Nyerere na kama utakumbuka Hayati Kombe ndie mkuu wa idara ya usalama wa Taifa alie fanya maboresho mengi ikiwepo na kupenyeza Tiss Jwtz.
 
Idara ya usalama sio jeshi. Ni idara ya kiraia.
Aliyeongea kwenye msiba wa Magufuli kwa niaba yao ndio mkubwa wao, over. Au jiulize, wapi umesikia Idara ya Usalam imepinduq nchi?
 
Usalama sio sehemu ya jeshi, ni idara ya kiraia.
Diwani athumani msuya mpaka sasa hivi ni ndani ya jeshi la polis ana cheo cha CP wakati siro ni inspector generali kwa hiyo diwani bado mdogo kwa siro na wakati siro anampigia salute mabeyo kwa hiyo IDARA anayoongoza diwani ni ndogo kwa jeshi la wananchi wa tanzania.huyu anaongoza idara huyu anaongoza jeshi sasa unafikiri nani mkubwa
 
Uko sahihi
Hapa mtabishana mpaka kesho, ni lazima ujue kazi za hizo taasisi mbili yaani jeshi na idara ya usalama wa taifa. Kazi za jeshi zinajulikana na wengi, za usalama je? Ukisoma sheria iliyounda idara ya usalama wa taifa, Tanzania intelligence &, security services act ya 1996 section ya 1 mpaka ya 5 inaeleza majukumu ya idara. Na moja ni kutafuta, kuchambua na kutunza taarifa zote muhimu popote zilipo.

Hii ina maana kwamba TISS wanafuta information popote, iwe ni bungeni, kijiweni jeshini nk. Kazi hii inaweza kua kupitia 'deep cover' au 'undercover informers' kwahyo usishangae kuona wamepenyeza watu jeshini au sehem yoyote ile. Kwa sura ya nje ni kweli CDF ni mkubwa sana kuliko viongozi wengine wa ulinzi na usalama, hata kiprotocal pia. Ila ukiingia kiundani kdg utakuta hata uteuzi wa CDF ni baada ya file lake kupita Tiss na wao kutoa mapendekezo msidhani jeshi halina control, kuna watu wanaliangalia kwa karibu mno ili kulinda usalama wa nchi.

Tiss wanadominate kwenye kila kitu, iwe uchumi, siasa, utawala nk. Wao wanatakiwa kutambua na kuzuia athari yoyote inayoweza kuikuta nchi. Tiss wakifeli hapo na taifa linakua dhaifu.

Ukweli ni kwamba ile taasisi ni 'dubwana' kubwa sana lililojificha chini ya neno 'taasisi' lakini kazi zake zipo hata kwenye vijiwe vya bodaboda au kanisani. Wakati wa kumuapisha Diwani Athumani, kama DGIS mpya, hayati Magufuli aliongea statement tata kwa CDF kua ''kuna watu pale jeshini anawaona wadogo kicheo ila wanaweza kumzidi kimadaraka", na akamaliza kwa kusema "that's how government work"
 
Hawa wanaovaa earphones ndio wanazicheza idara na taasisi nyingine zote katika nchi ndio maana usipokuwa na watu smart huko kila kitu kinaenda mrama.
Jf utani umezidi ndo tumefikia hii kweli?

Yani hawa hawa wanaovaa earphone kama ma dj ndo mnawafananisha na comando?
 
Wakuu hope mko poa

Naomba kuuliza ni nani, Ni mkubwa, lakini pia nani anajua Siri nyingi, lakini pia nani yupo karibu mno na raisi Kati ya Mkuu wa Majeshi(CDF) na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa(DGIS)

Karibu mtujuze mnaojua

Kiufupi hakuna mmoja ambae ni mkubwa kwa mwenziwe, Kiprotokali anaanza CDF, anafuata IGP, ndipo anafata DG, kilichopo ni kwamba wanaheshimiana kulingana na umbele wa idara zao na vipaumbele vya majukumu ya taasisi zao wanazoongoza pia kulingana na mgawanyo wa kimajukumu.
Tukiongelea upande wa CDF (Ni kiongozi wa Jeshi), yeye akiwa kama M/kiti wa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, anajua siri nyingi kuliko kiongozi wa idara yoyote ile. Na pia yupo karibu na rais kwani swala zima la Ulinzi wa nchi lipo mikononi mwake. Na kwa upande wa Mkurugenzi wa usalama wa taifa DG (Ni kiongozi wa idara ya kiraia), pia kwa upande wake idara yake inahusika na Usalama wa nchi (Ushushushu) wote kila mmoja anawajibika moja kwa moja kwa rais kwa wakati wake, lakini DG anawasilisha taarifa zinazohitaji kufanyiwa kazi au mapungufu anayoyaona yanayohusu Ulinzi (Gaps) kwa Mwenyekiti wa Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama. Ulinzi na Usalama ni vitu vinavyotegemeana sana.
Maagent wa Idara ya Usalama wa taifa ni kama sensors, zinazotumika katika kutafuta habari mbali mbali zinazohusu maadui wa ndani, hivyo katika kurahisisha upatikanaji wa habari hizo ndipo wamepenyeza watu wao (agents) kwenye taasisi za serikali, taasisi binafsi, mashirika umma, mashirika ya serikali, mahoteli, asasi za serikali, asasi za kiraia, vyuo, na hata mitaani.
 
Mmoja anaitwa Mkurugenzi wa usalama mwingine anaitwa mkuu wa vikosi vya ulinzi na usalama.

Unafikiri Nani mkubwa? Uliwahi kuona Rais akimbatana DGIS kwenye hafla yeyote rasmi mfano ukaguzi wa gwaride.... Na mengine.

Bettle na Scania yote ni magari Yana kazi tofauti lakini mmoja linawwza kumbeba mwingine Ila mbebwaji hawezi kumbeba mwengine
Sio mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, ni mkuu wa majeshi ya ulinzi ambazo ni kamandi ya wanamaji, ardhi,anga na JKT.

Watu ambacho hatuelewi ni kwamba mfumo wa utawala ulivyo Tanzania. Hapa Tz huwezi kupata cheo cha madaraka hata ngazi ya halmashauri bila kuwa TISS. So kwa macho yako utaona CDF ndo yuko juu ya DGI ila nyuma ya pazia wenyewe wanajua.
 
Wakuu hope mko poa

Naomba kuuliza ni nani, Ni mkubwa, lakini pia nani anajua Siri nyingi, lakini pia nani yupo karibu mno na raisi Kati ya Mkuu wa Majeshi(CDF) na Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa(DGIS)

Karibu mtujuze mnaojua
Hakuna aliye karibu na Rais sababu wote ofisi zao haziko Ikulu

Hakuna suala la nani mkubwa wakati wanahudumu katika mifumo tofauti, mmoja ana rank ya kijeshi mwingine si mwanajeshi

Siri kila mmoja anazo znazohusu uwigo wa taasisi yake
 
Kwan ulisha skia wap nchi iko chini ya usalama wa taifa zaidi ya jeshi,,, swali lako Lina kaupuuzi kdgo japo unahitaji kufahamu. Jeshi linaongoza sekta zote za usalama ikiwemo
1. Askali Polis
2. Usalama wa taifa
3. JWTZ na majeshi yote unayo yafahamu yako chini ja jeshi. Hivyo CDF ndio amri jeshi mkuu wa majeshi yote ikiwemo na nchi kwan yeye ndie mwenye uwezo kisheria kuipindua na si mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa. Bytheway usalama wa taifa ni shushushu(chawa)

Duuh mkuu JWTZ wako chini ya jeshi lipi
 
Back
Top Bottom