Nani mpambanaji kati ya Mama Caren na Mama Grace? Chagua mmoja

that manzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
385
Reaction score
1,246
NAOMBA KUJUA KATI YA HAWA WANAWAKE WAWILI NANI MPAMBANAJI?
YANI NATAKA UMTAJE MMOJA TU UNAYEMUONA NI MPAMBANAJI SITAKI MAMBO YA OOO KILA MMOJA KWA NAMNA YAKE. NATAKA USEME NI MAMA CAREN AMA MAMA GRACE

ASANTENI.

*MAMA Caren alisomeshwa na wazazi wake akiwa binti nakuhitimu masomo yake vyema. Alisoma kwa bidii na kufaulu vyema masomo yake.
Kisha akafaulu vyema na akaenda kusoma nje ya nchi.
Akiwa na miaka 27 tuu akawa akipata mshahara mkubwa wa Mamilioni ya pesa.
Akapata mume akaolewa. Na akasomesha watoto wake ili nao wawe na elimu za juuu. Na sasa watoto wake wanne wote ni wasomi wa Elimu za juu na maisha yao ni supaaa.

*MAMA Grace baada ya kumaliza darasa la SABA kijijini alikuja mjini kufanya kazi za ndani. Hata hivyo alipoona umri wa kujitegemea umefika aliacha kazi za ndani na kuanza kufanya vibarua vya hapa na pale. Leo anauza sokoni. Kesho anauza bar mwezi ujao anafanya kazi viwandani. Mwisho akaishia kuponda kokoto. Na akaona ni kazi inayomlipa zaidi. Alifanikiwa kupata mume akaolewa. Na kubahatika kuzaa watoto 6. Aliazia kuwasomesha ili wasiwe kama yeye. Hakuwahi kula chakula kizuri wala kuvaa nguo nzuri mpaka akahakikisha watoto wake wanapata Elimu za Juu. Na wote wakapata Elimu za juu na maisha yao ni Supaaaa.

Mama Caren na MAMA Grace nani mpambanaji?
 
Huyo mama Yako Grace,alipitia bahati mbaya na hatuwezi kumsifu kwa Hilo na Wala haikuwa stahiki yake Bali bahati mbaya. Hatuwezi kujiita mashujaa kwakuwa tulipitia kwenye dhiki.Ilitakiwa viwepo halafu akatae aende kutafuta mwenyewe hapo sawa.Yeye hakuwa na namna nyingine,she was a victim of circumstances.
 
So angeamua ku accept kuwa ye ni victim then angebweteka tu ingekuaje ?
 
Kwenye mapambano kuna Heavyweight na lightweight.

1. Mama Grace ni Heavyweight.
Ni mpiganaji wa uzani wa juu Kabisa ambao huwezi fananisha na huyo mwingine Mama Careen ambaye ni Lightweight.

Mama Grace ni kama kina Mfalme Daudi, Diamond, na wengineo.
Ambao Watoto wao ndio huwa kama huyo Mama Careen.

Mama Grace ndiye mpambanaji na anajua vita ya Maisha ukilinganisha na huyo mwingine.
.huwezi fananisha Simba na Mbwa. Simba dume amekulia Maisha ya hatari na mapambano. Wakati Mbwa yeye kazoea kuwekewa chakula hapo na kubweka Usiku. Au akiwa Mbwa Koko aokoteze chakula kwenye majalala huko
 
I love that 😊😊😊
 
Mama Caren alitumia nafasi ya kusoma ili kujitengenezea maisha yake. Wapo wengine walipata nafasi ya kusoma na walishindwa kutoboa.

Mamam Grace alitumia nafasi ya kukosa shule kwenda kuanza vibarua na kazi mbali mbali. Wapo wengine waliishia darasa la saba na walishindwa kutoboa.

Hivyo basi, wote ni wapambanaji kwa nafasi zao. Kila mmoja ametumia fursa iliyo mbele yake kwa wakati husika. Mama Caren alitumia shule, Mama Grace alitumia vibarua/kazi ndogo ndogo. Wapo walioshindwa shule wakatoboa kwa vibaru, wapo walioshindwa vibarua wakatoboa shule.

Note: "Hakuna cheti cha kufanya kazi ngumu".
 
Asantee
 
Ili ufanikiwe inapasa kufanya kazi na kile ulichopewa/barikiwa. Wote wawili wamepambana kadiri ya uwezo wao na mwisho wa siku wamefanikiwa. Safari ya Mama Grace imekua ndefu kuyafikia mafanikio kutokana na ukweli kwamba hakua amebarikiwa sana ukilinganisha na Mama Caren.

Wote ni wapambanaji, ila kujibu swali lako naenda na Mama Grace.
 
Back
Top Bottom