Habari wana JF,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 26, ni mhitimu wa Shahada ya Electrical & Electronics Engineering. Katika moja ya Chuo Kikuu hapa mjini Dar es Salaam kama ilivyo kawaida ya vijana wengi tukiwa vyuoni hujisahau kuwa kuna kumaliza masomo na kushindwa ku tafakari kukabiliana na maisha baada ya kumaliza chuo madhara yake ndio nayaona sasa.
Akili ilianza kuniijia nilipofika mwaka wa nne wa masomo yangu, nikawa ni mtu wakujiuliza sana inakuwaje nitaendesha maisha baada yakumaliza chuo na ukizingatia uchache wa ajira mtaani, nikawa mtu wa kujifariji muda wote nakusema nitafanya hata kazi ndogo ndogo za wiring installation maisha yataenda. Ilipofika August 2019 nilifanikisha kumaliza masomo yangu sasa hapo ndio ugumu wa maisha nikaanza kuuskilizia haswa haswa , nikiwa ghetto chakula kikaanza kuwa shida, madili yenyewe ya wiring installation yakawa machache kiasi kwamba kutegemea kunihudumia ikawa ngumu,
Nikawa ni mtu wa kuzunguka na barua za internship japo nipate hata hela ya kula tu, napo sikupata siku zikasogea mwenye nyumba nae anataka pesa yake hapo nakumbuka nimezidisha kama miezi mitatu , nilihisi kudata huku na kule nikakutana na mshkaji nikiwa nimesoma nae chuo course moja, akaanza kunipanga kuhusu forex kwa alivyonielezea tu nikajilaumu sana kuchelewa kuijua hii biashara nikauza vitu vyote ghetto kwa hasara nikapata kama 360tsh mwenye nyumba tukagawana nusu hasara nikampa 90tsh.
Mimi ni kati ya watu ambae nilikuwa na diss sana kukaa kwa ndugu ila nikasema siyo kesi kwakuwa nimeijua forex mwezi mmoja tu utanitosha kukusanya mkwanja wakupanga eneo zuri zaidi.
Bhasi kuanzia December nikaanza kukaa kwa ndugu na by January 2020 nikawa nimeingia rasmi kwenye ulimwengu wa FOREX kwa kile kiasi kilichobaki kutoka kwenye mauzo ya vitu vya ghetto ndio nikaanza nao kama mtaji na kujifunza kwa miezi nane mfululizo ni mimi na forex tu nikijipa matumaini nikiona baadhi ya wanufaikaji lakini kila nikijitahidi naishia kuchoma acc nakuanza upya tena kutafuta mtaji
Nimekuja kujitasmini toka January mpaka sasa August hakuna kitu nimefanya hata mia mbovu sina zaidi ya matumaini, Roho inauma sana sana nimefika point najihisi mfadhaiko moyoni, nanikifikiri nipo kwa ndugu umri unakimbia ndio nachanganyikiwa kabisa.
Naombeni mawazo yenu wandugu nianzie wapi ilihali sina mtaji.
Nakaribisha mawazo, maoni ,ushuhuda pia itapendeza Asante.