Nani ndio super power wa ukweli ukanda wa maziwa makuu kudhibiti mikwara ya Rwanda na Congo

Nani ndio super power wa ukweli ukanda wa maziwa makuu kudhibiti mikwara ya Rwanda na Congo

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2021
Posts
796
Reaction score
2,026
Siku zote panapofuka moshi ujue kuna moto hivyo kila jambo linalotokea huwa halikosi sababu. Kenya ameonekana kujiandaa kupekeka mamia ya wanajeshi Congo baada ya waasi kupata nguvu mashariki ya Congo na kukua kwa uhasama kati ya congo na Rwanda.

Ikumbukwe mwaka 2013 Tanzania alipeleka battalion kuunda brigade ambayo ilijumuisha askari kutoka Malawi na south Africa. Kikosi kile cha kwanza kilikuwa cha moto kilisheheni makomandoo, maafisa wataalamu wa siliaha walikinukisha sio mchezo. Habari ya M23 hatakuisikia tena leo wamepata wapi nguvu?

Taarifa za ujasusi zinabainisha kuwa Kigali inahusika kulipa msaada kundi la M23 kama ilivyofanya mwaka 2002 na kudhibitiwa na majeshi ya Angola na Zimbabwe. Je Tanzania ushawishi wetu umeshuka? au ushwahiba wa kagame na aliekuwa jamaa flani umechangia Rwanda kutunisha misuli?, Je Kenya ndio super power kwa sasa naomba kuwasilisha hoja

Amini amini nawaambia huenda Rwanda na udogo wake wa eneo ndio super power.
Tanzania na ukubwa wake wa eneo imekosa critical thinkers, inaendeshwa na ulaghai na uchawi.

Rais anazunguka dunia nzima kuomba misada, misada inaliwa kizembe tu, hamna anayechukuliwa hatua.

Mnafuja hela, nchi itaendelea lini?
 
Kwenye kikao chao cha Jumuia mashariki,wakuu wote wamajeshi wameshakubaliana kufanya kitu kwa ajili ya kusaidia Congo,kwa sidhani Kama Ni Kenya pekee wataenda,au wameshapangiana ratiba zao,kwa Ni swala la muda
 
sasa urafiki wa yule jamaa na ulichokiandika mbona havihusiani kabisa
Ni udadisi tu sababu Rwanda na Tz hatujawahi kuwa marafiki kama ilivyo Congo mapedeshee. Tumewapa sana uraia , wapo maeneo mbalimbali nchini kwa wingi kama Dar es salaam na kigoma. Kumbuka mkwara wa kagame kwa jk kilichotoke kagame alijaza askari mpakani baada ya jk kwenda kagera siku ya mashujaa. Operations kimbunga maeneo ya kanda ya ziwa. Offensive battalion ya tz ndani ya goma ilikuwa mwiba mchungu kwa vikundi ambavyo vilikuwa backed na Kigali. Lakini kuanzia 2015 hali imekuwa tofauti.
 
super power my chocolate a$$, anashindwa na 'wanamgambo' wa Al-Shabab wanaopigana 'jangwani' hakuna pa kujificha

ataweza 'jeshi la kimapinduzi' linalopigana 'msituni' kweli ?
Vita ya msituni ni rahisi kufanya reconnaissance na kupunguza vulnerability kuliko urban combat, terrorist attack ni mbaya sana na unaweza usipate ground edge kwani hujui adui anatokea upande gani kwa mfano ni vigumu kuzuia suicide attack. Vijana wa Kenya wanaenda kutoa matumaini kwa raia wanyonge wa congo
 
Ila DRC Wanayumba Wenyewe
Kwa Mali walizonazo Zinatosha Kulifanya Jeshi lao Kuwa na Nguvu sana
Untapped resources za Congo zinakadiliwa kuwa na thamani $23tr ila kama tz hawana intellectual resources, poor institution, poor governance na corruption vinaitafuna jamii ya Congo.
 
urban combat

Urban ipi ? KDF iko na troops kibao kwenye jangwa za Somalia, unapaita Urban ?

KDF-Jeshi, linalotrainiwa na jeshi la kimarekani kila kukicha, na wenye vifaa vya kivita vya kisasa, kupambana na 'wanamgambo' wenye 'AK47' miaka nenda rudi ?

ujinga kiwango cha Bitumen kuiita Kenya super-power
 
Usiitaje Tz maana Haina nguvu kijeshi,haipo kwenye usuper power Hapa East Africa na haitakaa ije kuwa super power.
 
Siku zote panapofuka moshi ujue kuna moto hivyo kila jambo linalotokea huwa halikosi sababu. Kenya ameonekana kujiandaa kupekeka mamia ya wanajeshi Congo baada ya waasi kupata nguvu mashariki ya Congo na kukua kwa uhasama kati ya congo na Rwanda.

Ikumbukwe mwaka 2013 Tanzania alipeleka battalion kuunda brigade ambayo ilijumuisha askari kutoka Malawi na south Africa. Kikosi kile cha kwanza kilikuwa cha moto kilisheheni makomandoo, maafisa wataalamu wa siliaha walikinukisha sio mchezo. Habari ya M23 hatakuisikia tena leo wamepata wapi nguvu?

Taarifa za ujasusi zinabainisha kuwa Kigali inahusika kulipa msaada kundi la M23 kama ilivyofanya mwaka 2002 na kudhibitiwa na majeshi ya Angola na Zimbabwe. Je Tanzania ushawishi wetu umeshuka? au ushwahiba wa kagame na aliekuwa jamaa flani umechangia Rwanda kutunisha misuli?, Je Kenya ndio super power kwa sasa naomba kuwasilisha hoja

Wewe unafahamu kwamba Magufuli kabla hajafa akuwa na mahusiano mazuri na Kagame hata na Museveni vilevile urafiki wao ulibaki wa kinafiki tu.

Na unafahamu kwamba hata kwenye mazishi ya Magufuli wote wawili hawakuja japo wengine walitoka mbali zaidi kama Zimbabwe hata SA na kuhudhuria mazishi.

Msimamo wa Magufuli kwenye jumuiya ya Afrika Mashariki ulimfanya atengwe na marais wa Kenya, Uganda na Rwanda.
 
Tanzania kwa sasa haina kikosi imara cha jeshi kama waliyokuwa nayo wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, kikosi cha sasa kipo kisiasa zaidi na hawajajitenga na siasa, unakuta maafisa wa jeshi wanafanya kazi na watu wa ccm.

Unakuta afisa wa jeshi ni mkuu wa mkoa na anaamurishwa na mwenyekiti wa ccm wa mkoa. Hili jeshi ccm wameiua kabisa na kwenye vikao mbalimbali vya ccm unakuta eti baadhi ya maafisa wa jeshi nao wapo.

Siku ccm ikiondoka madarakani ndio itajulikana walivyoiharibu hii nchi.
 
“If you build an army of 100 lions and their leader is a dog, in any fight, the lions will die like a dog. But if you build an army of 100 dogs and their leader is a lion, all dogs will fight as a lion.”​

Napoleon

Tatizo sio udogo wa Rwanda bali ukubwa wa mtawala (kujiamini) wa Rwanda.
Kwa hali tuliyonayo sasa hatuna tofauti yeyote na Burundi kijeshi. Na si sababu hatuna jeshi imara bali..................
 
Tanzania kwa sasa haina kikosi imara cha jeshi kama waliyokuwa nayo wakati wa utawala wa Mwalimu Nyerere, kikosi cha sasa kipo kisiasa zaidi na hawajajitenga na siasa, unakuta maafisa wa jeshi wanafanya kazi na watu wa ccm.

Unakuta afisa wa jeshi ni mkuu wa mkoa na anaamurishwa na mwenyekiti wa ccm wa mkoa. Hili jeshi ccm wameiua kabisa na kwenye vikao mbalimbali vya ccm unakuta eti baadhi ya maafisa wa jeshi nao wapo.

Siku ccm ikiondoka madarakani ndio itajulikana walivyoiharibu hii nchi.
Umepimaje uimara wa jwtz ukaona siyo Imara?
 
Ni ajabu Kwamba neno Hili superpower linaendelea kutumika vibaya. Hata nchi ndogondogo zenye ubabe mdogomdogo wa kufadhili vikundi vidogovidogo na silaha ndogondogo Kama AK 47 na LMG eti nao wanaanza kuitwa superpower!
Hata nchi inayopeleka jeshi jirani na nyumbani nae superpower!
Mnajua superpower ninyi? Hata Russia na Uchina bado hawana hadhi ya U -super power. Hata EU hawana hadhi hii .
Nb.
Sifa mojawapo ya superpower Ni kuwa na uchumi mkubwa kuliko wengine wote.
Jeshi imara lenye teknolojia za juu Sana.
Nb.
Si kila mwenye sifa moja Kati ya hizi Ni superpower. Eg Qatar na Saudia Wana chumi nzuri i'la si superpowers.
Turudi kwenye topic. Katika ukanda huu sisi tuendelee TU kujijenga kijeshi kiuchumi na kijamii.
Tuwe na viwanda vya kutengeneza vifaru.
Makombora.
Bunduki, na hata mizinga.
Wataanza kutuogopa na kutuhara.
Mwisho kabisa Bado hatuna uchumi was kutuma jeshi na kuanzisha kambi ugenini tukaweza kuhudumia. Russia na Marekani wanashindwa tutaweza sisi? Tena dhidi ya vibaraka wa vibeberu?

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom