Mimi kuna kipindi nilikuwa nafanya kazi sehemu fulani nikakutana na watu wengi sana wa TISS walikuwa na mission ene, walikuwa deployed na Magu. Baadaye nikakutana na mmoja ambaye anatokea mkoani kwetu, tukazoeana tukawa tunazungumza fresh tu.
Hivi karibuni nilipata changamoto kubwa sana ya kutapeliwa 17M nikajaribu kumshawishi kama angenisaidia, maana wale watu walionitapeli nilikuja kugundua siyo watu wadogo sana mtandao mkubwa sana wa utapeli serikalini na hawali peke yao. Nilipomwambia yaani akawa anatoa reasoning zero kabisa. Nikaona hakuna chochote hapa.
Nina demu pia kaka yake ni TISS lakini uwezo hakuna kitu.
Nilipokuja kufanya kazi Halmashauri nikawa na mazoea Tarafa mmoja anayekaimu nafasi huko kwa DC. Unajua chini ya DC kuna maakari was aina zote kama DSO (TISS), Magereza, JWTZ, RCO, nk nikawa nakutana nao hao TISS nikakonfirm akili zao ndogo sana.
Na kawilaya nilikopo ni kadogo nakutana nao kila wakati.
Yaani ukisikia imagination za watu zilivyo kuhusu hao TISS na ukiwaona unabaki kusikitika tu.