Nani ni mmiliki wa shule za Twibhoki na Graiyaki ziizopo mkoani Mara?

kyanyangwe

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2018
Posts
1,511
Reaction score
4,369
Habari za jumapili wakuu?

Naomba kufahamishwa, kwa miaka mingi sasa, kuna hizi shule mbili za Twibhoki na Graiyaki zilizoko wilayani Serengeti mkoani Mara, zimekuwa hazikosekani top 5 ya kwenye matokeo ya shule za msingi.

Ningependa kufahamu mmiliki wake ni nani?
 
Habari za jumapili wakuu?
Naomba kufahamishwa,kwa miaka mingi sasa,kuna hizi shule mbili za Twibhoki na Graiyaki zilizoko wilayani serengeti mkoani mara zimekuwa hazikosekani top 5 ya kwenye matokeo ya shule za msingi.ningependa kufahamu mmiliki wake ni nani?
Hizi shule zimekuja juu sana. Kwa mkoa wa Mara sasa zimeitoa Kowack girls kwenye namba moja. Nasikia ni za mtu moja (Twibhoki &Girinyakhi)

Odhis *
 
Mmiliki wa Twibokh anaeonekana kwa macho ya kawaida ni Mmama fulani hivi,ambaye inasemekana aliwahi hudumu wizara ya elimu,hiyo nyingine ni ya mtoto wake wa kike.Ukitaka undani tukupe number zao uwaulize

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
Mmiliki alikuwa wizara ya elimu,

Shule hazikosi top five.

Sawa.
 
Tanzania watu wanaangalia ufaulu wa mitihani na kudhani ufaulu ndiyo elimu bora. Hii imefanya baadhi ya shule kutumia njia harama ili mradi tu wanafunzi wake waonekane wanafaulu sana. Kuna shule zimejiingiza mpaka kwenye kutafuta mitihani na kuifundisha kwa ujanja (bila wanafunzi kufahamu) ili wanafunzi wafaulu kwa wingi na shule isifike.
 
Zina wanafunzi wachache sana hawazid 50 ndio maana wanafanya vzr
 
Tanzania watu wanaangalia ufaulu wa mitihani na kudhani ufaulu ndiyo elimu bora. Hii imefanya baadhi ya shule kutumia njia harama ili mradi tu wanafunzi wake waonekane wanafaulu sana. Kuna shule zimejiingiza mpaka kwenye kutafuta mitihani na kuifundisha kwa ujanja (bila wanafunzi kufahamu) ili wanafunzi wafaulu kwa wingi na shule isifike.
Kama ufaulu siyo elimu , basi vyuo vingechukuwa wa div. 4 & 0 . Lakini unaona wanachukuliwa waliofaulu kuendelea kuelimika na wasiofaulu wakirudishwa mitaani

Usaili ukifanyika kwa ujanja janja, viwango basi matokeo yanakuwa hayatoi hali halisi. Na ndicho kinachfanyika kwenye baadhi ya shule. Unajua unaweza kum-train kwa njia za short cut na haramu mtu ambaye ni darasa la saba akafanya mtihani na akafanya mtihani wa form four kwa ufaulu mzuri tu? Je anakuwa ameelimika japo atafaulu?
 
Bado "ufaulu" Macho mdiliko ni kigezo cha kujua na kuelimika. Vinginevyo viwepo vigezo vingine .
Ndiyo utaona wazazi wakifirisikia kutafuta elimu bora mpaka nje ya nchi. Hakuna siku vigezo vikawa tofauti.

Narudia. Ufaulu ni kigezo ambacho ni rahisi kutumika vibaya kama inavyofanyika Tanzania. Umebahatika kusoma nje ya nchi? Sidhani na nina uhakika kama jibu ni ndiyo usingekuwa unapingana na mimi.
 
Back
Top Bottom