Nani unamtabiri kuwa Rais mpya wa TFF katika uchaguzi wa mwezi wa nane ?

Uchaguzi uliopita Karia aliweza kutwaa kiti cha urais kwa mara ya pili kwa kuengua wapinzani wote kisha yeye mwenyewe kubaki kugombea.

kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Karia kashamaliza muda wake wa mihula miwili, hawezi kugombea tena.

Je ni nani atakuwa Rais mpya ?
1749916429228.png
 
Ni vizuri Wallace Karia akawaachia watu wengine nao waongoze TFF. Aachane na hila zake za kuhonga wajumbe na wadau wengine wa michezo ili tu kuwashawishi kuendelea kula hela za TFF.

Watangulizi wake wote tangu TFF ilipoanzishwa (Injinia Leodgar Chilla Tenga na Jamal Malinzi) wamefuata katiba kwa kukaa vipindi viwili tu kwenye uongozi wao. Kwa hiyo na yeye afuate utaratibu huo! Aachane na uroho wake wa madaraka uliopitiliza! Aache kufikiri yeye ni bora sana kuliko wengine! Na hivyo kuturudisha kwenye ile FAT ya Muhidini Ndolanga, au hii TOC ya Filbert Bayi.

Ni wakati wake sasa na yeye wa kwenda kula kwa jasho. TFF siyo shamba lake. Ile ni taasisi ya umma wa wapenda mpira wa miguu wote nchini.
 
Uchaguzi uliopita Karia aliweza kutwaa kiti cha urais kwa mara ya pili kwa kuengua wapinzani wote kisha yeye mwenyewe kubaki kugombea.

kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Karia kashamaliza muda wake wa mihula miwili, hawezi kugombea tena.

Je ni nani atakuwa Rais mpya ?
Mnaangaika na uchaguzi kwenye mashirikisho ya mpira , Dunia ya mpira Haina demokrasia
Raisi wa fifa aligombea mwenyewe
Rais wa uefa aligombea mwenyewe
Rais wa CAF aligombea mwenyewe
Na uchaguzi huu karia atagombea mwenyewe na hakuna chochote kitatokea
 
Katiba waliibadili,atagombea tena!
 
Mnaangaika na uchaguzi kwenye mashirikisho ya mpira , Dunia ya mpira Haina demokrasia
Raisi wa fifa aligombea mwenyewe
Rais wa uefa aligombea mwenyewe
Rais wa CAF aligombea mwenyewe
Na uchaguzi huu karia atagombea mwenyewe na hakuna chochote kitatokea
Hahahahaha,mpira ni kichaka cha wahuni na gang mafia,usidanganyike na Suti zao zile wanazovaa
 
Uchaguzi uliopita Karia aliweza kutwaa kiti cha urais kwa mara ya pili kwa kuengua wapinzani wote kisha yeye mwenyewe kubaki kugombea.

kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Karia kashamaliza muda wake wa mihula miwili, hawezi kugombea tena.

Je ni nani atakuwa Rais mpya ?
Madai yake kama ya Nkurunzinza kuwa mabadiliko yataanza sasa kwa hiyo atagombea vipindi vingine viwili
 
Back
Top Bottom