Wandugu,kwa kauli na maneno ya hovyo anayotamka huyu Polepole inaonesha hayupo pamoja na CCM wala viongozi wa serikali.
Anaongea kwa kujiamini sana bila kujali chochote.
NI UTASHI WAKE AU KUNA KUNDI KUBWA LA WATU WENYE NGUVU NYUMA YAKE?
Sent from my TECNO CA7 using
JamiiForums mobile app
Tunapo kusea ni pale ambapo tunawanyima watu uhuru wa kutoa maoni yao. Inabidi tufike mahali tuwe makini sana.
Tulianza kuminya haki za watu mdogomdogo tukidhani tunakijenga chama chetu kumbe tunakiua na kumjenga mtu binafsi. Sasa hayupo ameondoka msingi wa nyumba umeanza kuota nyufa. Tulipingana na wapinzani wetu hasa CHADEMA leo tumeanza kupingana wenyewe kwa wenyewe tunagombania mali ya uridhi aliocha baba.
Ndugu wakianza kufarakana wakigombea uridhi mwisho watauza mali ya uridhi walioachiwa na kubaki mafukara.
Malumbano tuliyokuwa nayo ndani ya chama ni matokeo ya ubaguzi uliokuzwa kuwa hawa walipendwa na baba, sisi baba alitubeza wacha tuwavuruge wapenzi wa baba. Kumekuwa na lugha inayoashiria kuwa kuna mpasuko kama vile: Sukuma Gang, Kundi la Msoga nk. Sijui ni vita kati ya Sukuma Gang na kundi la msoga?. Basi gombanani lakini katiba iheshimiwe na kila mtu hii itatuacha salama.
Makundi haya ya kusadikika hayana afya kwa taifa letu kama kweli yapo. Na kama yapo ya vunjwe kwa kupatanishwa ili tusonge mbele. Njia moja wapo ya kuleta mshikamano ni kuruhusu siasa huru CCM na vyama vya siasa viende kwa wananchi wakauze sera kwa wenye nchi wao waamue.
Viongozi wana kuja na kipita; Nyerere amepita, Mwinyi amepita, Mkapa amepita, Kikwete amepita, Magufuli amepita tena haraka, wengine watapita, Tanzania itaendelea kuwepo. Hivyo Tanzania ni kubwa kuliko mtu binafsi.
Tuheshimu katiba watakao baki karne hii ni wale watakao iheshimu katiba ya Tanzania na kuipenda Tanzania.