Nani wapo nyuma ya Polepole? CCM wanamlinda?

Mkuu me mwenyewe siyo wa kanda hiyo ila nasubiri siku ifike!.
 
HAHAHA HIV NYIE MNAIJUA IDARA YA USALAMA WA TAIFA AU MNAWACHUKULIA POA ETI UHATARSHE CCM KUBAKI MADARAKANI
 
Punguza ukabila. Jina lako na fikra zako tu zinaonyesha wewe ni kundi lile la kanda ya ziwa. Hizi fikra zimeletwa na Magufuli, za kutaka kutugawa Watanzania. Mshindwe na nguvu zenu za kiza na mawazo finyu.
Mwenye akili ndogo hawezi kunielewa ila Great thinker atafikili nje ya box. Ova!
 
Polepole hana tatizo na Samia! Ila polepole anashida na watu wanaozunguka Samia! Ukifatilia futungo sijui nn mengi tu na mpaka leo anasema viongozi wajuu kuweni macho ao watu mtawajua nendeni ata TRA taarifa zao zipo jinsi wahun wanavyokwepa kodi.

Tafakri na Massoud Kipanya then mrudie Polepole
 
Polepole hana shida na Rais Samia! Ila Polepole ana shida na wale watu ambao wanamzunguka Samia! Hawa wengi wao ni wapiga madili.

Nimekumbuka katuni za Massoud Kipanya embu zitafakari
 
Kwani Polepole naye ni kama mr #dishlimetilt kwamba kuna midume imesimama nyuma yake ikimpumulia?
 
Huwaga ninapenda kusikiliza speech za kaka mkubwa, lazima achomekee vichekesho kidogo lakini havihusiani na ngono.
 
Kila kitu kina 2sides, ie: a&b.

Unaposema anaongea maneno ya hovyo, je ya hovyo kwa nani?

Na je kuongea hovyo si ni kuvunja sheria za nchi ambayo ni makosa ya jinai?

Hilo la kwanza, la pili u hovyo wake kwa sababu wewe ni msisiem usiyetaka kusikia lolote against nk nk?

Mada yako hii imenifikirisha mambo mengi sana ambayo nimekosa majibu.
 
Punguza ukabila. Jina lako na fikra zako tu zinaonyesha wewe ni kundi lile la kanda ya ziwa. Hizi fikra zimeletwa na Magufuli, za kutaka kutugawa Watanzania. Mshindwe na nguvu zenu za kiza na mawazo finyu.
Unaelewa maana ya Gwakikolo au Unafikir kila anayempenda Magufuli ni msukuma.
 
Chakubanga kapigwa ni kitu kizito 17 March 2021 kwasasa ana WENGE tu ndiyo linampelekesha.
 
Vyama vya Kisiasa vimewajenga na Kuwaaminisha kuwa yote yasemwayo au kufanywa na Viongozi wa Vyama vyao hawapaswi kuhoji wala kukosoa, Wanachopaswa ni kuitikia tu ndio hata Kama hayako Sawa, ndio ukaja ule Usemi wa Mjumbe Ndio na Zidumu fikra za Mwenyekiti.

Bahati Mbaya sana, akitokea Mmoja kati yao na Kukosoa au kuwa na mawazo tofauti, ataanza kupigwa vita na Hata kutishiwa kufutwa Uwanachama, Tabia hii imewajenga Wanachama kuishi kwa Unafiki kwa kujifanya wanakubaliana na kila Jambo huku Mioyoni Mwao hawakubaliana, Sio Sawa Kila Mtu awe huru pasipo kuvunja Sheria.
 
Hivyo hivyo sii mbaya Cha mwizi kikaliwa na mwizi🤔.
 
Mh.Samia ni muungwana anamuacha tu aongee, ikifika muda Rais akakereka, hutamsikia tena Polepole anaongea, usicheze na nguvu ya Rais.
 
Hu
jatuandikia hayo maneno ya hovyohovyo kaka.
Ni yepi hayo - Babdari ya Bagamoyo au kutojaza maji Bwawa la Nyerere kwa sababu ya winch?
 
Labda tukuulize wewe mleta hii mada ya hovyo kwamba ni nani yuko nyuma yako?

Kama uliona ameongea ovyo basi akili yako wewe pia ni ya kijinga na hujui kupambanua hoja zaidi ya kuwahi kuleta umbea humu JF.

Ebu wewe itisha hiyo press conference halafu uongee ya kwako pia ili tukupime?

Acheni siasa za majungu wana upinzani wa nchi hii pamoja na kundi la watumbuliwa wa JPM
 
Tunapo kusea ni pale ambapo tunawanyima watu uhuru wa kutoa maoni yao. Inabidi tufike mahali tuwe makini sana.

Tulianza kuminya haki za watu mdogomdogo tukidhani tunakijenga chama chetu kumbe tunakiua na kumjenga mtu binafsi. Sasa hayupo ameondoka msingi wa nyumba umeanza kuota nyufa. Tulipingana na wapinzani wetu hasa CHADEMA leo tumeanza kupingana wenyewe kwa wenyewe tunagombania mali ya uridhi aliocha baba.

Ndugu wakianza kufarakana wakigombea uridhi mwisho watauza mali ya uridhi walioachiwa na kubaki mafukara.

Malumbano tuliyokuwa nayo ndani ya chama ni matokeo ya ubaguzi uliokuzwa kuwa hawa walipendwa na baba, sisi baba alitubeza wacha tuwavuruge wapenzi wa baba. Kumekuwa na lugha inayoashiria kuwa kuna mpasuko kama vile: Sukuma Gang, Kundi la Msoga nk. Sijui ni vita kati ya Sukuma Gang na kundi la msoga?. Basi gombanani lakini katiba iheshimiwe na kila mtu hii itatuacha salama.

Makundi haya ya kusadikika hayana afya kwa taifa letu kama kweli yapo. Na kama yapo ya vunjwe kwa kupatanishwa ili tusonge mbele. Njia moja wapo ya kuleta mshikamano ni kuruhusu siasa huru CCM na vyama vya siasa viende kwa wananchi wakauze sera kwa wenye nchi wao waamue.

Viongozi wana kuja na kipita; Nyerere amepita, Mwinyi amepita, Mkapa amepita, Kikwete amepita, Magufuli amepita tena haraka, wengine watapita, Tanzania itaendelea kuwepo. Hivyo Tanzania ni kubwa kuliko mtu binafsi.

Tuheshimu katiba watakao baki karne hii ni wale watakao iheshimu katiba ya Tanzania na kuipenda Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…