Nani yuko nyuma ya hujuma dhidi ya Bomba la Mafuta la Kigamboni?

Media zimelala usingizi mzito pia.zinareport zaidi kandanda wanacha taarifa zenye maslahi makubwa.
Midia zinadokoadoka kidogo cha mfukoni ndo maana kimya
Ingekua yule anaitwa mwendazake wangetwaja na kutaifishwa kuanzia viwanja na vyote vilivyokutwa ndani
 
Hii nchi kuna watu wameiweka mfukoni huwezi amini wanafanya yao yani watanzania milion 60 wamefanywa wajinga
 
Umeuliza jambo la msingi sana mtoa mada..!! Tunashadadiwa habari za Sabaya wakati kuna mtu kajiunganishia bomba la mafuta since 2017 huko anapakua tu mzigo halipi kodi wala nini alafu Raia Mwema na wengine kila siku Sabaya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa madawa ya kulevya hatujaona yalivyoteketezwa so mzigo bado upo au umeshaingia kitaa
 

Mkuu una uhakika kuwa hivyo ulivyotaja havijapigiwa kelele?
 
Yani kuna watu wanaona watanzania milion 60 ni wajinga sana wameifanya nchi kama ya kwao na ukiongea chochote unashughulikiwa.
 

Ni suala la kugawana majukumu, wengine Sabaya wengine bomba la mafuta. Hata hivyo hiyo 2017 Magufuli ndio alikuwa rais na alishamaliza wizi wote. Kama raia mwema wanamuongelea Sabaya tu, ni juu ya habari leo na uhuru kushikia bango hilo la bomba la mafuta.
 
Bomba La Kigamboni La Moto Sana Lile Litaunguza Watu Bila Shaka,Kila Mmoja Analinda Ugali
😀😁😂😃😄😅😆
 
Hapo hata waziri mkuu hasemi kamwachia mkuu wa mkoa kule hakugusiki na hakuna anayeinua mdomo kupasemea hapo

Usishangae kukuta ni deal la huyo huyo waziri Mkuu, au ulikuwa ni mradi wa jiwe ndio maana alikuwa hataki uhuru wa vyombo vya habari, ili aendelee kutupiga vizuri. Huoni hilo jambo halizungumziwi kwa aibu iliyopo, maana wananchi wakijua waliokuwa wanajifanya wazalendo ndio waliokuwa wanatupiga, hasira itazidi.
 
Mkuu una uhakika kuwa hivyo ulivyotaja havijapigiwa kelele?

Havijapigiwa kelele sana kama tunavyoona kwenye mabando mpaka wakalegeza.. na kwenye ushuru wa magari, kodi, vyakula n.k kama tungeamua wote kuwa kitu kimoja kulalamikia naamini wangelegeza.


Tena tushukuru sana huyu Mama kutuongoza..naimani kila kitu atakiweka sawa ikiwa pamoja na kupitisha katiba mpya. Tumuombee uzima.
 
Jamaa bado unaangaika na marehemu tu? tuko awamu ya sita tena hii bado hujachoka tu kumtajataja Magufuli? maana naona unalazimisha hii mada azungumziwe Magufuli ambaye ameshajifia na hana tena cha kufanya ila wewe bado unataka tuendelee kulalamika tu kwa maiti.
 

Tunamuongelea Mussolin mpaka leo, itakuwa huyo dictator pori.
 
Tunamuongelea Mussolin mpaka leo, itakuwa huyo dictator pori.
Hata Nyerere anazungumziwa ila hatuwezi kukaa tu kuanza kulalamika tu Nyerere alikosea hili na kuharibu lile wakati tuna nafasi ya kurekebisha hayo mambo. Sasa wewe bado unataka tuendelee kuzungumzia huo utawala wa awamu ya tano
 
Hata Nyerere anazungumziwa ila hatuwezi kukaa tu kuanza kulalamika tu Nyerere alikosea hili na kuharibu lile wakati tuna nafasi ya kurekebisha hayo mambo. Sasa wewe bado unataka tuendelee kuzungumzia huo utawala wa awamu ya tano
Nani amekulazimisha kumjadili dhalimu boss?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…