Nani yuko nyuma ya mafanikio ya soka Mbeya?

Nani yuko nyuma ya mafanikio ya soka Mbeya?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nchi yetu imejaliwa kuwa na mikoa takribani 30 kwa sasa, na mfumo wa michezo inayosimamiwa na TFF unahusisha mikoa yote ya Tanzania bara, hata hivyo kuna mikoa ambayo huwezi kusikia ina timu inayoshiriki ligi kuu miaka yote.

Ukiacha Dar es Salaam, na timu za taasisi mikoa mingine imekua ikibadilishana, lakini kwa mkoa wa Mbeya ni ngumu sana kuona wamekosa timu inayoshiriki Ligi Kuu.

Kuna wakati wanakuwa nazo mbili hata tatu.

Nini kinawabeba mbeya kisoka?
 
Hadi sasa tuna timu tatu...
1. Mbeya City
2. Mbeya Kwanza
3. Tanzania Prisons

Pale ligi daraja la kwanza (Championship) tunazo mbili....
1. Ihefu
2. Ken Gold

Mipango na mikakati madhubuti ya viongozi (wa mpira) pamoja na wadau wengine mbalimbali mkoani Mbeya ndivyo vimepelekea mafanikio hayo.

Lakini pia, talanta au vipawa vya wanambeya katika soka vinachagiza zaidi mafanikio haya.
Kwa miaka mingi kumekua na vijana wengi sana wenye vipaji vya mpira kutokea Mbeya wameng'ara katika soka la Tanzania.

Mbeya, Morogoro na Kigoma ni miongoni mwa mikoa vinara kabisa katika kutoa vipaji vya soka nchini Tanzania.
 
Wale jamaa wanagonga sana mdudu, kwa asili mdudu anaongeza thinking capacity na antibodies!

Mikoa yote wanayokula mdudu kwa wingi watu wake wamechangamka sana na wako mbele kwa kila kitu. Trust me
 
Mfano jiji la mwanza huwa nawaza ni umasikin au ni ubahili wa wadau tunashndwa kuwa na timu.

Maana kuwa na timu sio mchezo,unaweza jikuta mpaka unatoa hela za ada za watoto kuhudumia timu
 
Ni miaka yote Mbeya kumekuwa na timu nzuri tangu enzi za timu kama Mecco, Tukuyu Stars...

Hali ya kijiografia, body physique ya wanaume wa Mbeya "banyambala", ubishi wa kimaisha wa watu wa Mbeya n.k

Nazikumbuka Tukuyu star na MECCO za Mbeya | JamiiForums Nazikumbuka Tukuyu star na MECCO za Mbeya
 
Back
Top Bottom