Kuna dada mmoja nae ilimtokea,katoka zake kunywa huko kajilewea....arudi home...sasa njia aliyopita mbele kuna uwanja wa Mpira wa miguu,,naona akaona isiwe shida sana kuzunguka usiku huu wakati hakuna mechi uwanjani...akaamua kupita katikati ya uwanja....si ndo akaona kundi la mbwa....yeye anasema hawakumbwekea wala kumkimbiza ila kitendo cha kuona kundi kubwa la mbwa akaingiwa uoga akaokota jiwe kuwabonda....anasema alisikia kilio cha mbwa mmoja tu nadhani ndo jiwe Iilimpata....then mbwa wale wakasambaratika...na yeye akapita salama salmini....kafika home kalala,Mara kaanza kusikia maumivu ya mkono,akavumilia mpaka asubuhi ....kuamka akakuta mkono umeumuka na umeota magamba ya nyoka.Wakati anasimulia alikuwa tayari kazunguka kote bila kupona....nasikia alikufa baadae yule dada