Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
nimeingiza kichwa tu😌😌😌😂😂😂😂 jamani wewe, umesoma mada lakini au umesoma kichwa tu basi😃🤒
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣nimeingiza kichwa tu😌😌😌
Una kilo ngapi?Hapana mkuu, mimi sio mvivu
Tuheshimu kila mtu ile ni nature tu mkuu.Ila Mwanamke aheshimike aisee nimeona video jinsi anavyozaa aisee mpaka nimesisimka sana. 😔
Duh yani mabinti wakubwa hivyo mnamwacha afanye shughuli peke yake. Mngekuwa mnamsaidia. Unaamka mapema unamsaidia baadhi ya kazi ndipo unaenda kazini.Natumai wazima wote,.
Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae( Mungu anisaidie niondokane na hii hofu😓🥹🙏), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi..
Huyu mwanamke sielewi hua anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale., Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri ( anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja)..
Haitaishia hapo, Bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time… , Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani,. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa ( Napo ni mara chache sana ).. Sijui hua anapumzika mda gani
Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki , kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka,,..
Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati.. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinung’unika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja,..
Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni., Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishi😓😓😓 ( Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)