Tresor Mandala
JF-Expert Member
- Aug 20, 2010
- 40,905
- 86,203
Hamuwezi kufanana hata iwejeKuzaa nitaweza ila kufanya na kuishi kama anavyoishi ndio naogopa
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hamuwezi kufanana hata iwejeKuzaa nitaweza ila kufanya na kuishi kama anavyoishi ndio naogopa
Hakuna mfupa uliomshinda fisi, hakuna pembe za ndovu zilizomshinda tembo, hakuna mkia wa ngo'mbe uliomshinda ngo'mbe kwa tafsiri hiyo hutashindwa kulea watoto wako mwenyewe kila jambo ukilianza unashangaa kumbe ni rahisi hivi, ila hapo ni kwakuwa umeweka nadharia nyingi sana kwa kuangalia mama yako anavyofanya ila ukianza kufanya wewe majukumu ya malezi utashangaa mwenyewe ni rahisi hivyo mwili utakua unafanya tu hakuna kitakachokushinda.Sidhani kama nitaweza mkuu, labda nisiwe nakazi nyingine. Yaani niwe tu mama wa nyumbani
Anza kwanza mambo mengine yatajiseti yenyewe tu , mimi siku ya kwanza kutoka home nilienda kulewa mpaka sa nane za usiku nikiwa na miaka 18 tu , nikaona kurudi home nita nyongwa nikatokomea ndio ukawa mwanzo wangu wa kujitegemea mpaka sasa.Kuishi mwenyewe sidhani kama nitaweza aisee, siwezi🥹
Nimescreenshoot hii comment,, huenda nina hofu tu 🤔🤔Hakuna mfupa uliomshinda fisi, hakuna pembe za ndovu zilizomshinda tembo, hakuna mkia wa ngo'mbe uliomshinda ngo'mbe kwa tafsiri hiyo hutashindwa kulea watoto wako mwenyewe kila jambo ukilianza unashangaa kumbe ni rahisi hivi, ila hapo ni kwakuwa umeweka nadharia nyingi sana kwa kuangalia mama yako anavyofanya ila ukianza kufanya wewe majukumu ya malezi utashangaa mwenyewe ni rahisi hivyo mwili utakua unafanya tu hakuna kitakachokushinda.
Chukulia umekamata ujauzito Sasa hivi pah Mungu akakubariki na mapacha wanne unaanza nao wakiwa wachanga kabisa unahisi hutaweza kuwatunza?
Ulikua na ujasiri, hata hivyo ni kwasababu mtoto wakiume ndiomaana ilikua rahisi.. Sisi kwetu wakike kutoka hadi itokee umeolewa au unafanya kazi mkoa mwingine tofauti na nyumbani.,.. So nadhani bado nitaendelea kuwepoAnza kwanza mambo mengine yatajiseti yenyewe tu , mimi siku ya kwanza kutoka home nilienda kulewa mpaka sa nane za usiku nikiwa na miaka 18 tu , nikaona kurudi home nita nyongwa nikatokomea ndio ukawa mwanzo wangu wa kujitegemea mpaka sasa.
Yanazoeleka na utaona kawaida, na utaona Fahari kutumia nguvu zako kuhudumia damu yako.Inapendeza sana sana sana. Lakini hayo majukumu yanaogopesha kipenzi😓
Ila kweli , bora ubaki tu mpka ukuwe vizuri , kwa sababu hata wengi wanaotoka kwenda kupanga wanaishi kwa nguvu ya ma sponsor tu .Ulikua na ujasiri, hata hivyo ni kwasababu mtoto wakiume ndiomaana ilikua rahisi.. Sisi kwetu wakike kutoka hadi itokee umeolewa au unafanya kazi mkoa mwingine tofauti na nyumbani.,.. So nadhani bado nitaendelea kuwepo
Ukikua utaachaNatumai wazima wote,.
Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae( Mungu anisaidie niondokane na hii hofu😓🥹🙏), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi..
Huyu mwanamke sielewi hua anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale., Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri ( anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja)..
Haitaishia hapo, Bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time… , Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani,. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa ( Napo ni mara chache sana ).. Sijui hua anapumzika mda gani
Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki , kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka,,..
Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati.. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinung’unika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja,..
Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni., Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishi😓😓😓 ( Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)
[emoji12][emoji12]Nasubiria ushuhuda tu mengine yabaki historia, hakuna jambo gumu la kumshinda binadamu limitations tunajiwekewa wenyewe kwa kuamini au kwa kujinenea siweziNimescreenshoot hii comment,, huenda nina hofu tu [emoji848][emoji848]