Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na kusali pia.Kwakweli wacha niendelee kuwa na subira.. Huenda ikawa tofauti na ninavyowaza
Ngoja nianze weekend hii mkuu.. Ubarikiwe sana kwa ushauri mzuriHapana usiseme hapendi kusaidiwa. Wewe jiongeze na usimuombe kumsaidia. Mfano unawahi kuamka kabla yake anaamka anakuta umrfanya usafi angalau labda.
Yeye anakuta unamalizia usafi anajisemea ngoja sasa niandae tu breakfast akiwa anaandaa breakfast wewe ushachukua nguo upo unafua.
Sio mpaka umuombe. Na sidhani kama atakasirika wewe ukifanya hivyo.
Mimi nimeitazama kwa jicho la mbali sana.Huenda ni kweli unayoyasema aisee🤔🤔🤔
Una miaka mingapi baby Lee?Sawasawa, Asante big ciccy 🌹
What a wise lady🌹.. Mungu akubariki sana aisee, hope ni mama bora sana kwa wanaoMimi nimeitazama kwa jicho la mbali sana.
Ukifika umri wangu utanielewa.
Mama yako hayuko sawa, its not even something to be proud of!
I am 42, nina binti wa early 20's been married for almost 18 yrs before now, so hiki ninachokwambia kifanye kazi!
Your mother might be living a hell.
Wewe ni mkubwa, msogelee zaidi ya kuona ni sawa na kujifikiria unatakiwa kuwa kama yeye ukiwa a mother !
Hata wewe hupaswi kuwa hivyo kwa watoto wako!
Pamoja.Ngoja nianze weekend hii mkuu.. Ubarikiwe sana kwa ushauri mzuri
Ukikuta mama mwenye gubuHapana usiseme hapendi kusaidiwa. Wewe jiongeze na usimuombe kumsaidia. Mfano unawahi kuamka kabla yake anaamka anakuta umrfanya usafi angalau labda.
Yeye anakuta unamalizia usafi anajisemea ngoja sasa niandae tu breakfast akiwa anaandaa breakfast wewe ushachukua nguo upo unafua.
Sio mpaka umuombe. Na sidhani kama atakasirika wewe ukifanya hivyo.
Kabisa, hakuna tuzo hapo na haitawahi kuwepo.Halafu kuwa mama hakuna formula kwamba lazima uishi kama alivyoishi mamako
Ukiwa na pesa utaweka wasaidizi wa kutosha na wewe utaishi utakavyo
Hakuna tuzo ya mtesekaji bora mwaego
Huku anakukosoa kwamba hujui kitu. 🤣🤣Ukikuta mama mwenye gubu
Unamaliza kufanya usafi anakuja anarudia upya 😀
Acha uvivu, kwetu TANZANIA hatunaga watu wavivu.Natumai wazima wote,.
Iko hivi, kila siku zinavyoenda ndivyo ambavyo naogopa kuja kuitwa mama hapo baadae (Mungu anisaidie niondokane na hii hofu😓🥹🙏), hiii inatokana na lifestyle ambayo namwona mama yangu anaishi.
Huyu mwanamke sielewi huwa anapumzika mda gani, yeye ndie mtu wa mwisho kulala kila siku. Yaani hawezi kulala kama kuna mtu bado hajaingia nyumbani, na anahakikisha kila mtu amekula amelala anafunga milango ndipo na yeye alale. Na hata akiingia kulala halitapita nusu saa anapita tena vyumba vyote kuhakikisha mmefunga madirisha, mmeshusha neti na mmejifunika vizuri (anaweza akaamka hata mara 4 kwa usiku mmoja).
Haitaishia hapo, bado kuna sisi ambao inabidi asubuhi tuende kazini na wengine shuleni, wanaoamka usiku kusoma na wanaoamka kusali, kila mtu anamtajia mda wake wa kumwamsha hajawahi kukataa wala kupitiliza kutuamsha, always anakua on time.
Sijawahi kushuhudia ni saa ngapi ameamka ila kila tukiamka asubuhi tayari tunamkuta akiwa macho, kashafanya usafi na kashapika chai tunakunywa tunamwacha Nyumbani. Hatujawahi kuona au kushuhudia akilala mchana, Labda itokee anaumwa (napo ni mara chache sana ). Sijui hua anapumzika mda gani
Hajawahi kuishi na msaidizi wa kazi maisha yake yote, lakini hakuna aliyewahi kufua, kudeki, kupika, kuosha vyombo wala kufagia. Sio kwamba hatutaki kumsaidia Hapana, ni kwamba hatujawahi kuona uwanja ukiwa mchafu, vyombo vichafu na mda wowote ukirudi nyumbani unakuta chakula tayari na usafi wote ushafanywa na nguo zote ziko kambani zinakauka.
Licha ya hayo yote vilevile bado hajawahi kuacha kwenda kazini na shughuli zake nyingine zote za ujasiriamali hajawahi kuacha kufanya, hajawahi kuacha kwenda kwenye jumuiya wala kanisani hata jumapili moja, na kwenye dharura zote iwe hospitali au kikao chochote atakachohitajika mzazi awepo basi ni yeye ndio atakuwepo tena kwa wakati. Na sijawahi kumwona akilalamika, akinung’unika wala akimlaumu mtu kwamba hakuna anayemsaidia kazi hata siku moja.
Haya maisha yake yananiogopesha na yananifanya niogope hata kuwaza jinsi nitakavyoishi na watoto wangu huko mbeleni. Sometimes i wish ningekua wakiume labda ningeishi tu kama baba yangu anavyoishi😓😓😓 (Em assume mtu anafanya haya maisha yake yote)